Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 22 December 2014

SHOGA ELTON JOHN AFANYA HARUSI NA 'MUMEWE' DAVID FURNISH

Elton John na mpenziwe David Furnish
Msanii Sir Elton John alitarajiwa kufunga ndoa yake rasmi na mcheza filamu David Furnish jana Jumapili.

Kulingana na gazeti la The Independent nchini Uingereza, Elton John mwenye umri wa miaka 67 atafunga ndoa na mpenziwe wa miaka 20 katika nyumba yao ya Windsor ,na wote wawili wataweka picha ya harusi yao kwa instagram.
Wapenzi hao wa jinsia moja ndio wa kwanza kuunganishwa mwaka 2005 lakini wanataka kuimarisha uhusiano wao zaidi miaka tisa baadaye, baada ya sheria za ndoa za jinsia moja kuhalalishwa nchini Uingereza.
Msanii Elton john
''Tulikuwa na sherehe kubwa tulipounganishwa kiraia lakini tutafanya harusi,'' Elton John alikiambia chombo cha habari cha Sky News mapema mwaka huu.
''Nadhani ni vizuri kuchukua fursa ya sheria hizi mpya ili kusheherekea. Tuna bahati sana katika taifa hili kuweza kupata fursa kama hii''.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment