Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 27 December 2014

KOREA KASKAZINI YAMTUSI OBAMA

Rais Barrack Obama wa Marekani amefananishwa na tumbili wa msitu wa Tropiki
Korea kaskazini imeilaumu Marekani kutokana na mataizo ya mtandao ambayo yameikumba siku chache zilizopita.
Tume ya taifa ya ulinzi nchini Korea Kaskazini inasema kuwa Marekani inavuruga mifumo ya mitandao ya nchi hiyo huku ikimfananisha Rais wa Marekani Barack Obama na tumbili wa misitu ya tropiki mbali na kumshutumu kwa kuhusika katika kuonyeshwa kwa filamu yenye utata inayojulikana kama The Interview.

Filamu ya the Interview ambayo Rais Obama alishinikizwa ionyeshwe
Filamu hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Sony ambayo ni ya ucheshi inayoonyesha kuuawa kwa kiongozi wa korea kaskazini Kim Jong Un.
Korea kaskazini imekana kuhusika kwenye uhalifu wa mtandao dhidi ya kampuni ya Sony uliosababisha kampuni hiyo kusitisha maonyesho ya filamu hiyo.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment