Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 24 December 2014

MSD SASA KUFUNGUA MADUKA YA DAWA HADI MITAANI

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa nchini (MSD), Cosmas Mwaifani 
Na Andrew Msechu na Hadija Salum, Mwananch
Dar es Salaam. Bohari ya Dawa nchini (MSD) inatarajia kuanzisha maduka ya dawa katika maeneo yote ya nchi kwa ajili ya kurahisisha usambazaji wa dawa na vifaa tiba.
Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati wa pili wa miaka sita unaoanzia 2014 hadi 2020 kwa ajili ya kuhakiisha dawa na vifaa tiba vinapatikana kwa urahisi nchi nzima hadi ngazi ya vituo vya afya.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifani alisema mpango huo utakaosimamiwa na ofisi zao za kanda ni sehemu ya mkakati wa kujipanga katika misingi ya kujiendesha kibiashara.
“Ifikapo Januari 30, 2015 bohari itatekeleza mabadiliko makubwa yenye lengo la kuhakikisha dhima ya kuwezesha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba vyenye ubora kwa bei nafuu kwa Watanzania wote inatekelezwa kwa vitendo,” alisema.
Alisema maduka hayo yatafanya kazi saa 24 na kuuza dawa kwa bei nafuu iliyo chini ya bei ya soko na yatatoa huduma kwa watu binafsi na waliopo chini ya utaratibu wa Bima za Afya watakaokuwa wameandikiwa vyeti vya dawa na vifaa tiba.
Mwaifani alifafanua kamba maduka hayo yatatoa huduma hizo kwa hospitali zote za binafsi na za Umma pamoja na maduka yote ya dawayatakayohitaji kununua dawa kwa bei ya jumla.
Amesema hatua hiyo itaongeza wigo wa bohari kusambaza dawa na kuiondoa katika mfumo wa sasa wa kutoa dawa kwa mahitaji maalumu, hivyo kuboresha huduma za afya zinazotolewa katika hospitali na vituo vya afya vilivyosajiliwa kutoa huduma za afya na kuipunguzia Serikali mzigo wa kuchoma dawa zilizopita muda wake.
Katika hatua nyingine, alisema MSD inatarajia kuanzisha utaratibu wa kutumia wazalishaji wa ndani wa dawa na vifaa tiba ili kuepuka gharama ya zaidi ya Dola100 milioni za Marekani inazotumia kwa mwaka kuagiza asilimia 85 ya dawa na vifaa hivyo nje ya nchi.  
Amesema kutokana na hali hiyo kiwango cha upatikanaji wa dawa nchini kimekuwa chini ya asilimia 85 na kuigharimu fedha nyingi kutunza dawa kwa muda mrefu kutokana na kufidia muda mrefu wa miezi tisa ya tahadhari kufidia muda mrefu unaotumika kuanzia manunuzi hadi kufikisha dawa hizo nchini.
Amesema zipo dawa na vifaa tiba ambavyo vinaweza kuzalishwa hapa nchini kwa gharama ndogo au kutumia malighafi zipatikanazo hapa hapa hivyo mchakato wa kuwapata washirika katika mradi huo utafanyika kupitia mzabuni atakayetangazwa rasmi.
CREDIT: MWANANCHI

1 comment:

  1. Wazo zuri lakini linahitaji mpango muhsusi Sana ili litkelezeke.kwa upande Fulani nashangaa kwanini walifikiri kuliweka katika mpango kazi wao.
    Biashara ya dawa Ni ya ajabu,Kuna maslahi makubwa binafsi yanahusika na Pia maslah ya multinationals.mafanikio ya mpango huo ni threat kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo, dawa zalipa Sana.kuna wakati ilikua karibu by 40% ya investment sababu ya demand,he maduka ya bei nafuu si yatahujumiwa, AMA MSD wenyewe watafungua mianya ya rushes kwa wafanyakazi husika, na je katika uchumi wa soko,je haitakua ni kuharibu mtiririko wa soko huria?

    ReplyDelete