Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 30 December 2014

WALIOHUSIKA ESCROW WASIFUMBIWE MACHO-ASKOFU


Na Hastin Liumba, Tabora
SERIKALI imeshauriwa kuwa makini na watendaji wake wanaojali kujinufaisha badala ya kutatua kero zinazowakabili wananchi.

Askofu Paul Meivukie wa kanisa la TAG jimbo la Tabora alisema hayo katika mahojiano maalumu na mwandishi wa gazeti hizi yaliyofanyika katika kanisa la Kitete Christian Center mara baada ya kumalizika kwa ibada.



Akizungumzia sakata la fedha zilizochotwa katika akaunti ya ESCROW Askofu Meivukie alisema kiongozi yeyote anayepewa dhamana ya kuongoza wizara au idara yoyote ya serikali yupo kwa niaba ya wananchi hivyo anapaswa kuwa mwadilifu na kuwa na hofu ya Mungu.

'Naomba serikali iwe makini sana na watendaji wasio waadilifu…..ijenge utamaduni wa kutofumbia macho ufisadi au wizi wa aina yoyote ile wa mali za umma unaofanywa na baadhi ya watendaji”.alisema.

Aidha Askofu Meivukie amewataka wakristo wote wakiwemo watumishi wa serikali, taasisi binafsi, wafanyabiashara na wanafunzi kuendelea kujishusha zaidi mbele za Mungu na kujiepusha na mambo yote yaliyochukizo kwake ili wazidi kumpendeza naye aendelee kuwabariki.

Naye Askofu Agustino Dedu wa kanisa hilo toka jijini Tanga amewakumbushwa waumini wa kanisa hilo kumtumaini Bwana Yesu katika maisha yao yote kwa kuwa alikuja duniani ili wanadamu wote waokolewe.

Aidha alisema Yesu Kristo alikidhi vigezo vyote vya kuitwa mkombozi wa ulimwengu kwa sababu hata kabla ya kuzaliwa kwake ilishatabiriwa kuwa atazaliwa mtoto mwanamume katika mji wa Bethlehemu na jina lake ataitwa Yesu au Emanuel yaani Mungu pamoja nasi na huyo atakuwa ni mkombozi wa ulimwengu.

‘Wakristu hatuna budi kumtumaini Yesu kwa kuwa alitolewa kwa ajili yetu ili tuokolewe, tuwe huru na dhambi, tuwe na nguvu za kuendelea kumshinda mwovu shetani, na zaidi ya yote tuishi maisha matakatifu ya kumpendeza’, aliongeza.

No comments:

Post a Comment