Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 24 December 2014

WAFUGAJI WA NGORONGORO, LONGIDO NA MONDULI WALIA NA MABADILIKO TABIA YA NCHI

Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny5 Blog
Monduli: WAFUGAJI kutoka  Wilaya za Ngorongoro ,Longido na Monduli wameeleza kuanza kukumbwa na athari za matokeo ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi.


Wakizungumza katika  kongamano la jamii  za kifugaji zinazoishi katika nyanda kame lililoandaliwa na  shirika la  Haki kazi Catalyst   na  taasisi ya kimataifa ya mazingira na maendeleo (IIED)  viongozi wa jamii hiyo walisema kuwa  tayari wameanza  kukosa mvua za kutosha katika maeneo yao

“ Joto limekuwa kali sana, mvua hazitabiriki ,tunashindwa kujua misimu tuliyozea,wakati mwingine mvua kubwa inanyesha kiasi cha kuleta hofu na mafuriko  makubwa tofauti na siku za nyuma ,hali hii ni ishara kuwa hali ya siku zijazo ni tete”alisema  Martalo. 

Diwani wa viti maalum kutoka Wilaya ya Ngorongoro Tina Timan alisema kuwa  kwa sasa wanawake wa jamii hizo wanasafiri umbali kutafuta maji kufuatia vyanzo vya maji kukauka kufuatia hali ya ukame.

Tina aliongeza kuwa migogoro ya ardhi na sera mbalimbali zinawaweka wafugaji katika hatari zaidi ,maeneo yao yanachukuliwa na kugeuzwa hifadhi na mengine kupewa wawekezaji tunaomba katika mikakati hii hili nalo litazamwe.

Esupat Ngulupa kutoka Longido alisema kuwa miaka michache iliyopita wafugaji walipoteza idadi kubwa ya mifugo baada Wilaya hiyo kukumbwa na ukame uliodumu  kwa muda mrefu.

Alisema kuwa jamii pamoja na viongozi wa kisiasa  ilishiriki kikamilifu katika kongamano hilo na kutoa mawazo na uzoefu,  kutafakari kwa pamoja sera na dira ya maendeleo ya taifa katika kuondoa umaskini na jitihada za taifa katika kukabili mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi. 

Aidha Morindat aliongeza kuwa washiriki pia walijadili kwa undani masuala ya msingi juu ya dhana na Sayansi ya mabdiliko ya hali ya hewa na tabia Nchi pamoja na   Mifumo ya wafugaji iliyopo na inayopotea katika kuhimili mabadiliko mbalimbali yanayotokea.

Sera na sheria za nchi na jinsi inavyowezesha ama kutowezesha mifumo hiyo ya kijamii kufanya kazi na mabadiliko makubwa ya kiuchumi duniani faida na athari zake kwa mifumo ya Kijamii.

No comments:

Post a Comment