Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 25 December 2014

MALECELA ASULUHISHA MGOGORO WA SUDAN KUSINI

Waziri Mkuu mstaafu John Malecela 
Na Mussa Juma Mwananchi
Arusha. Viongozi waliogawanyika na kuanzisha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ndani ya chama tawala cha Sudan People Liberation Movement (SPLM), Sudan Kusini wamekubaliana kuwajibika ili kurejesha amani na utulivu nchini humo.
Mwenyekiti wa kuwezesha mazungumzo ya amani ndani ya chama hicho, Waziri Mkuu mstaafu John Malecela alisema hayo jana baada ya viongozi hao kumaliza mazungumzo.
“Tulikuwa na mazungumzo ya siku mbili kuhusu mgogoro ndani ya nchi hiyo yanayoratibiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kiasi kikubwa yameendelea kwa amani na utulivu,” alisema.
Alisema wajumbe wa makundi hayo, wameeleza kutambua kwamba amani ya kudumu italetwa na wao wenyewe kwa sababu waliteseka kuitafuta.
Alisema wamesema wapo tayari kuwajibika ili kurejesha amani ya nchi yao.
Hata hivyo, Malecela alisema mwelekeo unatarajiwa kupatikana katika kikao kitakachoanza Januari 5 mwakani ili kujua ni lini watasaini makubaliano rasmi.
Awali, akisoma taarifa ya pamoja iliyosainiwa na viongozi wa makundi mawili yanayopingana, Akol Paul Kordil na Duer Tul Duer, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mazungumzo, Balozi Hassan Kibelloh alisema makundi hayo yanaamini mazungumzo yao yatazaa amani.
“Wajumbe wameshukuru CCM na mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete kwa kuwezesha mazungumzo yao ya kusaka amani,” alisema.
Alisema pia wajumbe wametiwa moyo na hatua ambazo zimefikiwa katika kurejesha umoja.
Mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini chini ya CCM yalianza Oktoba 12 mwaka huu, mbele ya Rais Kikwete makundi yanayopingana yalisaini mpango wa kuanza mazungumzo ya amani ndani ya SPLM Arusha.
Makubaliano hayo, yalishuhudiwa pia na Rais Sudan Kusini, Salva Kiir na hasimu wake, Riek Machar aliyekuwa Makamu wa Rais.
Miongoni mwa maazimio ya awali ya mazungumzo hayo ni pamoja na kuendelea na majadiliano ili kuondoa tofauti ndani ya chama hicho kwa kujadili chanzo cha mgawanyiko na kufikia maridhiano.
Pia makundi hayo, yalikubaliana kuhakikisha mapigano yanasitishwa ili wananchi wa Sudani Kusini waishi kwa amani.
Sudan Kusini, ilijitenga na Sudan mwaka 2011 na kuwa nchi huru, lakini hata hivyo Desemba mwaka jana chama tawala kiligawanyika na kuzua vita ndani ya nchi hiyo.
CREDIT: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment