Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 23 December 2014

MOHAMMED ALI ALAZWA HOSPITALI



BINGWA wa zamani wa ndondi za uzani wa juu duniani, Mohammed Ali amelazwa hospitalini baada ya kuugua maambukizo ya mapafu.

Ali mwenye umri wa miaka 72 na ambaye ana ugua ugonjwa wa Parkinson anadaiwa kuwa hali yake si mbaya sana.

Msemaji wa bondia huyo mkongwe alisema ugonjwa huo uligunduliwa mapema.

Hata hivyo msemaji huyo, hakutoa maelezo zaidi na kutaka haki ya faragha ya familia ya bondia huyo kuheshimiwa.

Ali alipatikana na ugonjwa wa Parkinson mwaka 1984, miaka mitatu baada ya kustaafu katika masumbwi.

Alionekana hadharani katika sherehe moja Septemba mwaka huu nyumbani kwake Louisville, Marekani wakati wa kutoa tuzo za kibinadamu za bondia huyo.

No comments:

Post a Comment