Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 22 December 2014

WAMILIKI WA BAA WAIFURAHIA KAMPENI YA TUTOKE NA SERENGETI


WAMILIKI WA BAA WAIFURAHIA KAMPENI YA TUTOKE NA SERENGETI
Ni takribani mwezi mmoja sasa tangu kampeni ya miezi mitatu ianze ambapo mpaka sasa imevutia wateja wengi katika droo za kila wiki.

Wakati kampeni ikielekea kuwa ya aina yake has katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka, kampuni ya SBL imeweza kutembelea baa tofauti tofauti ndani na nje ya jiji la Dar es Salaam na kuongea na mameneja wa baa na wafanyakazi juu ya kampeni inayoendeleana walikuwa na maoni yafuatayo.


“kwa kiasi kikubwa promosheni hii imeongeza unywaji wa bia ya Serengeti Premium Lager katika baa hii. Mauzo ya chupa ya Serengeti yameongezeka zaidi tofauti na kipindi cha nyuma,” alisema Bwana. Limo- meneja wa baa ya Hawaii iliyoko Kimara Baruti Dar es salaam. Akieleza juu ya uelewa wake juu ya promosheni  inayoendelea, Bwana. Limo alisema kwamba “Ninachofahamu ni kwamba baada ya kununua bia ya Serengeti, unaangalia chini ya kizibo na mteja anaweza pata bia ya bure. Pia Punguzo la Shs. 300 katika kila chupa ya bia, kushinda fedha taslim pamoja na Limo bajaji ni baadhi ya vitu ambavyo wateja wanaweza kujishindia,” aliongeza.

Kwa upande mwingine Bwana. Kavishe, Meneja wa baa iliyoko Uhuru Garden-Buguruni alionekana kuwa na uelewa zaidi juu ya promosheni hiyo na kuongeza kuwa imeongeza mapato kwenye bar yake kutokana na wateja kuiagiza kwa wingi. Akieleza juu ya uelewa wake juu ya promosheni hiyo, Bwana. Kavishe alisema “ninachojua ni kwamba, unaponunua bia ya Serengeti angalia chini ya kizibo na utapata nafasi ya kujishindia bia za bure, bajaji na punguzo la bei ya bia”.
Baa ya mwisho kutembelewa ilikuwa ni ile ya Kambarage iliyoko Kihonda Morogoro ambapo kaunta ya baa hiyo ilisheheni bia chapa ya Serengeti Premium Lager, jambo lililoashiria kwamba eneo hilo linawapenzi wengi wa bia hiyo.

“Tunajivunia kwamba mshindi wa kwanza wa Tutoke na Serengeti alitoka katika baa hii. Amekuwa mtumiaji mzuri wa bia ya Serengeti kutoka katika baa hii mpaka siku anatangazwa mshindi” alisema Bwana. Johnston, Maneja wa baa hiyo. Kwa mtazamo wake anaamini kwamba ili watu waweze kushinda wanatakiwa kushiriki mara kwa mara kama alivyofanya  Rukia .

Tutoke na Serengeti ni kampeni ya miezi mitatu ambayo ilizinduliwa rasmi na kampuni ya SBL pamoja na B-Pesa mwezi uliopita na washindi wamekuwa wakizawadiwa zawadi mbalimbali kila baada ya droo inayofanyika kila wiki SBL- Chang’ombe chini ya uangalizi wa  bodi ya michezo ya bahati nasibu Tanzania.

Zaidi ya kuwazawadia washindi zawadi mbalimbali kama vile Limo Bajaj, pesa taslim, bia za bure pamoja na punguzo la bia la shilingi 300, promosheni hii pia imelenga katika kutangaza utalii wa ndani kwa kuwapeleka wapendanao katika mbuga mbalimbali za wanyama zilizoko nchini ambapo kampuni ya SBL hulipia gharama zote kuanzia   malazi, chakula,  na burudani nyingine katika kipindi chote mabacho wapenzi hao.


Ili kushiriki katika promosheni hii, mshiriki anatakiwa awe na umri wa zaidi ya miaka 18, anunue bia ya Serengeti Premium Lager na aangalie chini ya kizibo ambapo atakuta namba ambazo zinatakiwa zitumwe  kwenda 15317 kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno. Kadiri mteja anavyoshiriki zaidi, ndivyo anavyojiweka katika nafasi ya kushinda. 

No comments:

Post a Comment