Meneja wa Bia ya Serengeti, Rugambo
Rodney (katikati) akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa
kuchezesha bahati nasibu ya shindano la
Tutoke na Serengeti, linaloendeshwa na kampuni hiyo, ambapo Bw. Hassan Mfaume
ameibuka mshindi katika Shindano hilo, kulia ni Msimamizi toka bodi ya michezo
ya kubahatisha, Abdallah Hemedy na kushoto ni Auditor kutoka Pricewater House
Coopers Ltd, Golder Kamuzora hafla hiyo imefanyika makao makuu ya Serengeti
jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Bia ya Serengeti, Rugambo
Rodney akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kuchezesha
bahati nasibu ya shindano la “Tutoke na
Serengeti” linalo endeshwa na kampuni hiyo, ambapo Hassan Mfaume ameibuka
mshindi katika shindano hilo, kulia ni msimamizi toka bodi ya michezo ya
kubahatisha, Bw. Abdallah Hemed.
MKAZI WA MABIBO AIBUKA MSHINDI KWENYE MTOKO WA “TUTOKE NA SERENGETI ”
03rd
Dec 2014, Dar es Salaam
Kampuni ya SBL leo imemzawadia Bwana: Hassan Mfaume mkazi wa Mabibo ziara ya kwenda
kutembelea hifadhi ya taifa ya Serengeti iliyolipiwa na kampuni hiyo mara baada
ya kuibuka mshindi wa droo ya Tutoke na Serengeti iliyofanyika leo makao makuu ya
SBL yaliyopo Chang’ombe jijini Dar es
Salaam.
Akiongea kwa njia
ya simu Bwana Hassan ambaye alikua kikazi Mwanza alionekana kushangazwa na kushitushwa
baada ya kusikia taarifa kwamba amekuwa mshindi. Aliishukuru kampuni ya SBL kwa
kile alichokiita zawadi murua ya kipindi hiki cha sikukuu.
Hii imekuja wiki
moja tu baada ya Rukia Almasi, ambaye ni Mama wa nyumbani na mkazi wa Kihonda-Morogoro
kutuzwa ushindi wa Limo Bajaj katika kampeni hii inayoendelea.
Akiongea baada ya droo iliyoshuhudiwa na waandishi
wa habari pamoja na Bwana. Abdallah Hemedi mwakilishi wa bodi ya michezo ya bahati
nasibu Tanzania, Bwana Rugambo Rodney-Meneja Chapa wa bia ya Serengeti Premium
Lager alisema Bwana Hassan ameshinda safari ya watu wawili iliyolipiwa gharama zote
ikimaanisha kwamba anaruhusiwa kwenda na mwenza wake na SBL watagharamia kila kitu
kuanzia malazi, usafiri pamoja na vivutio mbalimbali.
Rodney aliwasihi watanzania waendelee kushiriki
kwani zawadi za kushindaniwa zipo nyingi. Aliongeza kwamba kampuni imelenga katika
kuinua utalii wa ndani ikiwa ni njia mojawapo ya kurudisha sehemu ya faida kwa wateja
wake baada ya mafanikio mazuri yaliyopatikana katika mwaka husika.
Kampeni ya Tutoke na Serengeti
wameungana na B-Pesa wataalam wa teknolojia mpya ambao hivi karibuni wamezindua
mfumo mpya wa usafirihaji wa fedha. B-Pesa watahusika pia katika kusambaza fedha
kwa washindi mbalimbali kote nchini kupitia simu za mkononi.
No comments:
Post a Comment