Tarehe:
01/12/2014
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
BASATA Arts Centre
Tel. 2863748/2860485
Fax: 0255- (022) – 286 0486
Ilala Sharif Shamba
P.O. Box. 4779, Dar es Salaam
E-mail:basata06@yahoo.com
PONGEZI KWA MSANII NASSIB ABDUL AKA
DIAMOND KWA KUSHINDA TUZO TATU ZA CHOAMVA14
Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) kama msimamizi na mratibu wa sekta ya Sanaa nchini
linapenda kutoa pongezi za dhati kwa Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nassib
Abdul maarufu kama Diamond kwa kushinda tuzo tatu kwa mkupuo za CHOAMVA
zinazoendeshwa na kituo maarufu cha luninga cha Channel 0 chenye makao makuu
yake Afrika Kusini.
Tuzo
alizoshinda Diamond ni pamoja na Most Gifted East African Artist, Most Gifted
Afro Pop video na ile ya Most Gifted New Comer.
Kushinda
kwa Diamond katika tuzo hizo kubwa barani Afrika na kuwashinda wasanii wengine
wenye ‘majina makubwa’ ni ishara kwamba muziki wetu unakubalika ndani na nje ya
Tanzania.
Baraza
linatoa wito kwa wasanii na wadau wote wa muziki kuzidisha ubunifu, bidii na
weledi katika kazi wanazozifanya ili wasanii wengi zaidi waweze kuchomoza
katika tuzo na majukwaa mbalimbali ya kimataifa kwa lengo la kujitangaza na
kukuza soko la kazi zao kimataifa.
Aidha,
Baraza linaendelea kuwakumbusha na kuwasisitiza wadau wa muziki na Sanaa kwa ujumla
hususan wakuzaji Sanaa (mapromota) kuendelea kujenga mazingira rafiki kwa
wasanii wetu kufanya kazi kwa ubora na weledi lakini pia kwa upendo na furaha
ili kujenga daraja zuri kwa wasanii wengi zaidi kung’ara kwenye ngazi za
kimataifa.
Ni
imani ya Baraza kwamba, ushindi huu wa kihistoria wa Diamond utakuwa chachu kwa
wadau wote wa Sanaa nchini hususan wasanii katika kujituma na kuhakikisha
hawaridhiki na mafanikio waliyonayo.
Ni
matumaini ya Baraza kwamba wasanii na wadau wote wa Sanaa wataendelea kutambua
umuhimu wa kufuata sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji sekta sambamba na kutambuliwa
na Serikali.
Sanaa
ni kazi, tuipende na kuithamini
Godfrey
Mngereza
KAIMU KATIBU MTENDAJI
No comments:
Post a Comment