Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 30 August 2014

KUBENEA AELEZA SABABU ZA KUSHTAKI BUNGE LA KATIBA


Ndugu waandishi wa habari,
Natumaini mna taarifa kwamba tangu Ijumaa iliyopita, nimefungua shauri Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam, kupinga kinachofanywa na Bunge Maalum la Katiba. Shauri hilo, limesajili kwa Na.28 la mwaka 2014.

Katika kesi hiyo, nimeomba Mahakama Kuu itoe tafsiri sahihi juu ya mamlaka ya Bunge Maalum la Katiba, chini ya kifungu cha 25 (1) na (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ya mwaka 2011.

Aidha, nimewasilisha maombi madogo nikiomba Mahakama kutoa zuio la muda la kusimamisha Bunge Maalum la Katiba, wakati tukisubiri uamuzi wa kesi ya msingi. Maombi ya zuio yamepangwa kutajwa tarehe 4 Septemba na kesi ya msingi itatajwa 15 Septemba 2014.

Ndugu waandishi wa habari,
Tangu kuripotiwa kufunguliwa kwa shauri hili mahakamani, yapo mengi yaliyosemwa. Wapo walionipongeza na kunifariji. Wapo walionitia moyo na kuniomba nisirudi nyuma. Wapo walionidhihaki na kunikatisha tamaa. Wapo walionitisha.

Lakini wapo walioahidi kuniombea kwa Mwenyezi Mungu ili jambo hili kubwa nililolifanya kwa maslahi ya taifa langu, niweze kulifikisha mwisho nikiwa mzima na mwenye amani.

Ninafahamu jukumu hili nililolibeba ni zito sana. Linaweza likasababisha baadhi ya watu kukosa posho ikiwa mahakama itaridhia ombi langu la usitishaji wa Bunge la Katiba. Linaweza kunitenganisha na baadhi ya ndugu na marafiki zangu. Linaweza kuhatarisha hata maisha yangu.
Lakini kwa kuwa maisha yangu hayajawahi kuwa salama kwa zaidi ya miaka tisa sasa; nimesema Mungu ndiye atakayenilinda.

Ninajua kuwa kesi hii, inaweza kusababisha gazeti langu la ----------- ambalo limefungiwa kwa muda usiojulikana na watawala kwa kuitumia sheria katili ya magazeti, linaweza lisifunguliwe kabisa. Hii ni kwa sababu, waliofungia ----------- ndiyo haohao niliowashitaki.
Hata hivyo, nimesema niko tayari kwa lolote. Nitakabaliana nalo kwa kadri Mwenyezi Mungu atakavyoniongoza.

Ndugu waandishi wa habari,
Nimefungua shauri hili kwa kusukumwa na uzalendo wangu na kulinda heshima ya wananchi wa Jamhuri ya Muungano waliotoa maoni yao mbele ya Tume ya Rais ya Mabadiliko ya Katiba, nami nikiwamo.

Nimefungua shauri hili baada ya kujiridhisha kuwa wananchi waliowengi, kutoka makundi mbalimbali – serikalini hadi chama tawala – wanakiri kuwapo tatizo katika tafsiri ya sheria kuhusu mamlaka ya Bunge Maalum la Katiba. 

Baadhi ya walioko bungeni wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samwel Sitta, wanasema wanaweza kufanya lolote katika rasimu. Wanaweza kufuta rasimu; kubandua sura yote na wanaweza kubandika sura mpya.

Siyo hivyo tu: Wanaweza hata kukusanya maoni upya kutoka makundi mbalimbali. Kazi hii, ndiyo inayofanyika sasa bungeni.
Lakini wapo wanaoamini kuwa Bunge Maalum la Katiba, halina mamlaka ya kufanya kazi ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Halina uwezo kukusanya maoni upya.

Bunge Maalum la Katiba, haliwezi kunyofoa moyo wa rasimu ya katiba kama ilivyowasilishwa na mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, waziri mkuu mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba na kuleta kitu kipya ambacho hakikutokana na wananchi; na ambacho kimekusanywa kinyume cha sheria.

Nimekwenda mahakamani baada ya kumuona Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema akishindwa kwenda mahakamani kuomba tafsiri ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Badala yake, Jaji Werema amempotosha rais kuwa hana mamlaka ya kusimamisha mchakato wa Katiba.

Sheria inayosimamia mchakato wa katiba mpya ni sheria tofauti na sheria nyingine katika nchi. Sheria nyingine zote zinasimamiwa na vyombo vya serikali. Hii inasimamiwa moja kwa moja na wananchi.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano inayotumika sasa, haina kifungu chochote kinachoruhusu kutungwa katiba mpya. Wabunge wote wa Bunge la Muungano ambao sasa wamefanywa wajumbe wa Bunge la Katiba, akiwamo Werema, waliapa kulinda katiba iliyopo na kuitetea. Rais wa Jamhuri ya Muungano ameapa kulinda katiba iliyopo.

Lakini kwa kuwa Bunge la Jamhuri liliridhia kutunga katiba mpya kwa kutumwa na wananchi – siyo kwa kutumwa na katiba iliyopo – rais anayo mamlaka mapana ya kusimamisha mchakato huu.

Rais anaposimamia mchakato huu, hafanyi hivyo kama rais binafsi. Anatekeleza matakwa ya wananchi ambao wote kwa umoja wao, wamempa yeye mamlaka yao kusimamia raslimali, ulinzi na usalama wa mali za raia wa Jamhuri ya Muungano.

Kwahiyo, ni ujuha kuacha mabilioni ya shilingi ya wananchi kuteketea, kisha watawala wakadai kuwa “rais hana mamlaka ya kusimamisha mchakato wa katiba mpya.” 

Kutokana na mgongano huo, kama mwananchi wa Jamhuri ya Muungano nimewasilisha malalamiko yangu mahakamani kwa nguvu ya Ibara ya 26 (2) ya Katiba inayosema: “Kila mtu ana haki, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria, kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi ya katiba na Sheria za nchi.”

Suala zima la maoni ya wananchi haliwezi kuachwa mikononi mwa watu wachache. Mamlaka ya kutafsiri sheria za nchi, hawezi kuachwa mikononi mwa Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalum la Katiba wala chombo kingine kilichojinyakulia mamlaka hayo kinyemela.
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri, Ibara ya 107 A (1), “mamlaka yenye kauli ya mwisho ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa ni mahakama.”

Kwa msingi huo, iwapo tafsri yangu ni sahihi, kinachofanywa na Bunge la Katiba sasa, ni uvunjaji wa Sheria Na. 83 ya mwaka 2011, inayounda Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kuanisha majukumu yake na Bunge la Katiba.

Kama tafsiri yangu ni sahihi, kinachofanywa na Bunge Maalum la Katiba, ni kuvunja Katiba. Hakikubaliki.
Hivyo basi, kupitia kwenu, nichukue nafasi hii, kuwaomba wananchi wote wanaolitakia mema taifa letu, kusimama pamoja nami katika kusaidia taifa kupata katiba inayoheshimu maoni ya wananchi.

Ninawashukuru wote waliofariji; wanaonitia moyo na walioahidi kuniombea katika hili. Ninawaomba waniunge mkono kwa hali na mali. Nchi hii ni yetu sote.

Saed Kubenea,
Mkuregenzi Mtendaji,
HHP Limited.


HILI NDILO TAMKO LA JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA KUHUSU KATIBA MPYA



JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA

TAMKO LA JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA

Sisi, wajumbe wa Jukwaa la Wakristo Tanzania, tuliokutana tarehe 27 hadi 28 Agosti, 2014, Dar es salaam , tumepata fursa ya kutafakari, kujadili na kujielimisha kwa kina yaliyomo katika Rasimu ya pili ya Katiba na mjadala unaoendelea katika Bunge Maalum la Katiba. Baada ya mjadala wa kina, tunatoa tamko letu kama ifuatavyo:

Tunaipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo ilikusanya Maoni ya WANANCHI kuhusu mabadiliko hayo na kutuletea Rasimu yenye maoni mengi ya Watanzania bila kujali dini zao, upande wa Muungano walikotoka, hali zao za kimaisha, jinsi na kabila. 

Pia tunaipongeza Tume kwa kuandaa nyaraka na kumbukumbu mbalimbali kama Randama, Nyaraka zenye maoni ya wananchi, picha, tafiti mbalimbali na hata orodha ya watu walioshiriki kutoa maoni katika Tume. Tume pia iliweza kuandaa Tovuti iliyokuwa na kumbukumbu za Tume na Maoni yote yaliyotolewa. Kazi hii ni ushahidi kuwa Tume iliandaa Rasimu kwa weledi na kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kwa kuzingatia maoni ya WANANCHI.

Tume imedhihirisha kuwa, ilitenda KIZALENDO na, kwa mantiki hiyo, wajumbe wote bila kujali vyama vyao, dini zao na upande wa Muungano walikotoka, waliweza kujadili kwa uwazi na kweli na mwisho wakaridhiana katika kila Ibara iliyopendekezwa. Hili linatufundisha kuwa Katiba ni MARIDHIANO na si jambo la maslahi ya kisiasa, bali ni suala la maslahi ya WANANCHI.

Tunaamini kuwa kila Mjumbe wa Kamati ya kukusanya maoni ya WANANCHI aliheshimu kiapo chake na hivyo kufanya kazi waliyokabidhiwa kwa uaminifu na uadilifu na ya kwamba hawakushawishiwa au kupokea rushwa kutoka kwa kundi, dini au chama chochote cha siasa wakati wa zoezi hili.

Baada ya Tume kuwasilisha Rasimu kwenye Bunge Maalum la Katiba, Taifa likaanza kushuhudia “uasi wote na uovu wa wanadamu wapingao kweli kwa uovu” (Warumi 1:18). Katika mijadala ya Bunge Maalum la Katiba (BMK) yakaanza kujitokeza mambo mengi yasiyo ya maslahi kwa WANANCHI, na ukiukwaji wa sheria na kanuni. Mambo kadhaa yanadhihirisha hili:

Tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilifungwa bila sababu za msingi kutolewa wakati mchakato unaendelea. Hali hii imefanya zile nyaraka na kumbukumbu zilizoandaliwa kwa ajili ya rejea na kuwezesha mjadala wa Rasimu ya Katiba kuendelea katika mwanga na ufahamu wa nyaraka hizo kutowezekana kabisa. Kwa sababu hiyo, tumeona Bunge Maalumu la Katiba likiendelea kupotosha takwimu na taarifa mbalimbali ambazo WANANCHI hawawezi kuzipata kwa ajili ya kuoanisha baina ya kinachojadiliwa Bungeni na kilichomo katika Rasimu na viambatanisho vyake vyote. Tunajiuliza jambo hili limefanywa na nani na kwa maslahi ya nani? 

Bunge la Katiba limeshindwa kusimamia Kanuni kama ambavyo zilipendekezwa na kuridhiwa na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba. Kushindwa huku kusimamia kanuni kumesababisha vurugu ndani ya Bunge Maalumu na kumekwamisha matarajio ya wananchi kupata Katiba bora ya nchi yetu. Matumizi ya ubabe na wingi wa Wabunge wa Chama Tawala (CCM), badala ya Kanuni za Bunge na maridhiano, kumefanya mchakato wa Katiba kuhodhiwa na Chama Tawala dhidi ya maslahi ya WANANCHI.

Mijadala katika Bunge Maalumu la Katiba imekuwa ya kejeli, matusi, vitisho, ubabe na kupuuza hata kupotosha maoni yaliyotolewa na Wananchi kwa Tume. Hali hii imelifanya Bunge Maalumu la Katiba kupuuzwa na hivyo kupoteza heshima na hadhi yake. Matokeo yake baadhi ya wajumbe wa Bunge la Katiba wakaamua kususia vikao vya bunge na wengine kuendelea, bila kukumbuka kuwa KATIBA NI MATOKEO YA TENDO LA MARIDHIANO NA SI SUALA LA MASLAHI YA KIKUNDI CHA WATU WACHACHE.

Hatua iliyofikiwa ni dhahiri, Mjadala wa BMK unaoendelea umeondoa kwa kiasi kikubwa maoni yaliyotolewa na wananchi kuhusu muundo wa Muungano, kupunguza mamlaka ya Rais, uwajibikaji na uwajibishwaji wa wabunge, ukomo wa ubunge, n.k., na kuwezesha maoni na maslahi ya Chama Tawala kwa uongozi wa kikundi cha wanasiasa wachache wasio na uaminifu na uadilifu wa kutosha kuwekwa kama mapendekezo ya Katiba mpya kwa nia ya kulinda maslahi binafsi au ya makundi na kuhalalisha ukiukwaji mkubwa wa sheria, kanuni na maadili ya uongozi bora. 
Baada ya kujadili na kuona haya na mengine mengi, Jukwaa la Wakristo Tanzania lina maoni yafuatayo; 

1. Kwamba Serikali (Wizara ya Katiba na Sheria) irudishe tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na nyaraka zake zote kwa ajili ya wananchi kuendelea kuona kazi waliyoifanya, kujifunza na kujadili Rasimu ya Katiba kwa uwazi.

2. Kwamba maoni ya wananchi hayawezi kufutwa na kudharauliwa na Chama Tawala. Hivyo basi, Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea lijadili na kuboresha tu maoni yaliyomo katika Rasimu ya Katiba na sio kufanya mabadiliko katika Katiba ya mwaka 1977.

3. Kwamba mchakato wa Katiba usimamishwe ili kupisha majadiliano, maelewano na maridhiano muafaka, uchaguzi mkuu na wa serikali za mitaa. Na mabadiliko ya Katiba ya 15 ya mwaka 1977 yafanyike kuwezesha chaguzi kufanyika kwa uwazi na haki. Pia, kuweka kifungu kitakacholinda Rasimu ya pili na kumtaka kiongozi ajaye kuendelea na mchakato wa Katiba.

4. Kwamba baada ya Bunge Maalum la Katiba kuanza shughuli zake tena, Mwenyekiti wa Bunge hilo afanye kazi kwa mujibu wa kanuni na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba badala ya kutumia ubabe na kiburi cha wingi wa wajumbe wa Chama cha Mapinduzi katika Bunge la Katiba.

5. Kwamba wananchi waendelee kusoma na kujadili maoni yaliyoko katika Rasimu ya pili ya Katiba, na kufuatilia kitakachokuwa kinajadiliwa kwenye Bunge la Katiba ili kuwawezesha kupiga kura ya maoni wakiwa na uelewa wa kutosha kabisa kuhusu ni nini kipo kwenye “Katiba inayopendekezwa”. Wananchi pia wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwa nia ya kuwawezesha kupiga kura ya maoni.

6. Kwamba tunaomba Tume ya Mabadiliko ya Katiba ihuishwe na kupewa mamlaka kisheria ili kuiwezesha kujibu maswali yanayojitokeza na kutoa ufafanuzi kwa Bunge Maalumu la Katiba na wananchi kwa jumla hadi Katiba Mpya itakapokamilika na kukabidhiwa rasmi.

Jukwaa la Wakristo Tanzania na Watanzania wote wanaoitakia nchi yao mema, tunakuomba Mheshimiwa Rais kwamba AMANI ya nchi yetu sasa imo mikononi mwako hasa katika kipindi hiki cha kuandikwa kwa Katiba Mpya. Tunakuomba uahirishe mchakato unaoendelea ili uepushe ishara za aina mbalimbali za kuanzisha sintofahamu nchini mwetu na hali yoyote inayoweza kuathiri vibaya mshikamano, umoja na amani ya Taifa letu. 

Ifahamike kuwa WANANCHI wa Tanzania wako juu ya Wajumbe wa Chama cha Mapinduzi. Kwa mantiki hiyo, tunakuomba uepushe WANANCHI wa Tanzania kuhamasishwa kukikataa Chama cha Mapinduzi kwa kuwa tu Chama hicho kimeyapuuza na kimekataa Maoni yao waliyotoa kwa dhati baada ya kuaswa na kuhimizwa kufanya hivyo na viongozi wa nchi.

“Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wafanye yasiyowapasa. Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya, wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutabakari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, wasio na ufahamu, wenyekuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema; si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao”. (Rejea Warumi 1: 28-32)

IKUMBUKWE KUWA RASIMU YA PILI YA KATIBA NI WARAKA HALALI NA RASMI NA NDIYO MAWAZO YA WATANZANIA NA TUNAHIMIZA KUWA KATIBA NI YA WANANCHI NA INAHITAJI MARIDHIANO NA SIO UBABE.

Imetolewa leo Agosti 28, 2014
Na MKUTANO WA JUKWAA LA WAKRISTO
Tanzania Episcopal Conference (TEC)
The Council of Pentecostal Churches of Tanzania (CPCT)
Christian Council of Tanzania (CCT) 
The Seventh Day Adventists (SDA)

TAHADHARI PICHA ZINATISHA: AJALI YA KIPANYA ILIYOUA 10 MBEYA



Mungu uwarehemu, lakini ajali hizi mpaka lini jamani?

PHOTO CREDIT: WANABIDII

MATESO, UKATILI NA UNYAMA KWA WAISLAMU WANAOTUHUMIWA KWA KESI YA 'UGAIDI'


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kumb: 21 / 1435 AH Ijumaa, 26th Shawwal 1435 AH 22/08/2014 CE
MATESO, UKATILI NA UNYAMA KWA WAISLAMU WANAOTUHUMIWA KWA KESI YA ‘UGAIDI’ NI KUTOKANA NA UISLAMU WAO
وَمَا نَقَمُوا مِنْهُمْ إِلاَّ أَنْ يُؤْمِنُوا بِاللَّهِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ (البروج:
“Nao hawakuona baya lolote kwao ila tu kwa kuwa wamemuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa” (TMQ 85:8)
Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki inalaani kwa nguvu zote mateso, unyama, udhalilishaji na ushenzi mkubwa wanayofanyiwa ndugu zetu Waislamu wakiwemo masheikh, maustadh na wanaharakati wa Kiislamu walioko katika kesi inayodaiwa ya ugaidi, kama walivyoeleza wenyewe karibuni mahkamani jijini Dar es-Salaam na kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Sisi katikaHizb tunaweka bayana kwamba: mateso, unyama, ukatili na ushenzi wanaotendewa ndugu zetu Waislamu hao na wengineo ni kwa sababu tu ya Uislamu wao na si vyenginevyo. Kwa sababu kimsingi sheria ya kibaguzi inayoitwa ya ‘ugaidi’ imelazimishwa na Marekani kwa ajili ya kuwadhulumia Waislamu. Hizb inauliza kwa kinywa kipana pale viongozi wa kanisa akiwemo Mchungaji Mtikila ambaye mara kwa mara huwekwa korokoroni, kuhojiwa na Polisi hadi kufungwa jela. Jee kuna siku yoyote aliwahi kufanyiwa ushenzi, mateso na unyama kama wanaofanyiwa ndugu zetu hao Waislamu ?
Tunasema tena, vitendo hivi vya mateso na dhulma ambavyo hufanyiwa Waislamu na vikosi maalumu kwa agizo la Marekani sio mwanzo Tanzania wala sio mwisho. Bali vimeenea duniani kote kuanzia katika kambi za mateso za Marekani za Guntanamo, Balgram, Abu Ghuraib nk.
Aidha, mateso yaliyotajwa mahkamani hapo na Waislamu hao ni machache kuliko halihalisi ilivyo. Hususan kwa ndugu zetu waliobambikiziwa kesi kama hizo wakiwemo Waislamu wenzetu wa Arusha, Mwanza, Kenya nk.
Mateso haya hutendwa kupitia vikosi maalum vinavyosimamiwa na Marekani vinavyoitwa ati vya kupambana na ugaidi ambavyo licha ya kukosolewa, kukashifiwa, kufedhehewa na kulaumiwa vikali hadharani kwa uovu wao kama ilivyofunua taarifa ya tarehe 18/08/2014 ya Mashirika ya Utetezi la Haki za binadamu kwa kikosi cha ATPU cha kupambana ugaidi nchini Kenya.
http://hizb-eastafrica.com/swa/index.php?option=com_content&view=article&id=1470%3Aje-hamuogopi-mungu-mkakomeka-na-maovu-yenu&catid=30%3Akwa-vyombo-vya-habari&Itemid=127
Pamoja na fedheha hizo za hadharani kutoka kwa taasisi zao wenyewe, bado vikosi hivi vinaonekana kujigubika uziwi na kuendeleza maovu, dhulma, mateso na udhalilishaji wa wazi kwa Waislamu.
Vitendo hivi ni miongoni mwa dalili nyingi za kudhihirisha udhaifu na fedheha kubwa kwa mfumo wa kibepari. Kwanza, kutokuwa na muundombinu thabiti wa ukusanyaji ushahidi, kama kuna ushahidi kamwe katika kesi na badala yake kutegemea utesaji. Pili, dhihirisho la kukosekana uzito shauri/ kesi husika kiasi cha vikosi hivi kumalizia chuki na ghadhabu zao kwa watuhumiwa kwa kuwatesa. Kwa kuwa wana yakini hakuna kesi itakayoendelea. Tatu, dhana ya kitoto na ndoto za mchana za bwana wao Marekani na mfumo wake wa wa kikafiri wa kibepari kudhani ati kuwatesa Waislamu kutawatisha Umma wa Kiislamu waache na waogope uwajibu wao wa kuhubiri na kutangaza dini yao ya haki. Marekani na vikosi vyake vinavyoitwa vya kupambana na ugaidi wanaelea katika ndoto za mchana na kugubikwa na ujinga wa kutojua historia wakidhani kuwa Uislamu utamalizika kwa kuteswa Waislamu. Lau ingekuwa ndoto yao hiyo ndio uhalisia, basi Uislamu leo usingetajwa kamwe katika uso wa ulimwengu. Na nne, ni kushindwa watetezi wa mfumo wa kibepari kutetea mfumo wao kwa hoja na dalili. Badala yake katika kutapatapa na khofu ya kumalizika mfumo wao huwa hawana namna ila kutesa Waislamu. Kwa kuwa kimaumbile ubepari hauwezi na hautoweza kujitetea kwa hoja za kidini wala za kiakili. Kimsingi umezaliwa kwa ajili ya kufa! Na punde InshaaAllah utatupwa katika jalala la kihistoria. Kwa kuwa hauna manufaa kwa ubinaadamu zaidi ya madhila na kushindwa juu ya kushindwa.
Umeshindwa ubepari katika siasa ukidai kuna demokrasia kumbe ni nidhamu ya udanganyifu na matajiri. Hudai katiba itokane na watu kumbe tayari wana katiba yao mfukoni, umeshindwa kiuchumi kwa kuongeza msururu wa makodi na umasikini, huku makampuni ya kibepari yakipora rasilmali kwa baraka za wanasiasa waovu na mikataba ya udanganyifu, umeshindwa katika upande wa kijamii kwa kupitia fikra chafu za ‘uhuru’ (freedoms) kwa kuongeza maovu na mabalaa mbali mbali kwa mwanadamu kuanzia ulevi, zinaa, kupigia debe vitendo viovu vya ushoga, usagaji nk.
Na vitendo hivi vya utesaji na udhalilishaji Waislamu katika mchakato wa kisheria ni kushindwa kuliko dhahiri kukosekana kinachoitwa utawala wa sheria na udhaifu katika taasisi za mahkama za kusimimia haki na sheria. Ajabu na aibu kubwa! wanashindwa hata kusimamia sheria walizozitunga kwa mikono yao ! Basi nini cha kutarajia kutoka mfumo huu zaidi ya damu na machozi !
Baada ya yote hayo Hizb inawasisitiza Waislamu kuendelea kuulingania Uislamu wao bila ya khofu wala woga kwa njia ya Mtume SAAW ambayo haihusishi utumiaji wa nguvu wala mabavu. Pia wafedhehi kila aina ya vitendo vya dhulma wanavyotendewa Waislamu, na kuachana na michakato yote ya siasa za kikafiri za kidemokrasia , zikiwemo katiba zake na chaguzi zake. Kwa kuwa ni haramu na zaidi ndio zinazodhamini kupatikana watawala wanaosaidia kudhuru Waislamu.
Aidha, tunawafariji ndugu zetu na Waislamu jumla kwa madhila haya na mengineyo. Lakini pia tunawapa Waislamu bishara ya ushindi wa Umma wetu chini ya kivuli cha dola tukufu ya Kiislamu ya Pili ya Khilafah Rashidah. Dola hiyo haitosahau dhulma hata yenye ukubwa wa punje ya hardali aliyotendewa Muislamu ila itamhukumu dhalimu. Na lau madhaalimu wataondoka duniani kabla ya kurejea dola hiyo. Pia hawatosalimika wala kunusurika na adhabu ya Muumba ambae kamwe hajawasahau, hasahau wala hatosahau na dhulma yao.
وَلاَ تَحْسَبَنَّ اللَّهَ غَافِلاً عَمَّا يَعْمَلُ الظَّالِمُونَ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمْ لِيَوْمٍ تَشْخَصُ فِيهِ الأَبْصَارُ (إبراهيم: 42
“Na wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na yale watendayo madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatakapokodoka macho yao.” (TMQ 14: 42
Masoud Msellem
Naibu Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb-ut Tahrir Afrika Mashariki
Tovuti Rasmi ya Hizb ut- Tahrir
www.hizb-ut-tahrir.org
Tovuti ya Afisi ya Habari
www.hizb-ut-tahrir.info

AFRIKA KUSINI YALAANI MAPINDUZI LESOTHO

Jeshi la Lesotho

Wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Afrika Kusini inasema matukio ya himaya ya mfalme wa Lesotho, kusini mwa Afrika, yanaelekea kuwa ni mapinduzi.
Msemaji wa wizara ya mashauri ya nchi za nje alieleza kuwa nchi yake haitakubali mabadiliko ya serikali ya Lesotho kinyume cha katiba.
Hapo awali waziri mkuu wa Lesotho, Tom Thabane, aliiambia BBC ameondoka Lesotho baada ya kutishwa kuwa atauwawa.Alitoa wito kwa kamanda wa jeshi la Lesotho awaamrishe wanajeshi wake warudi kambini.
Aliongeza kusema kuwa hatua za jeshi zimeifanya serikali isiweze kufanya kazi, na ni sawa na mapinduzi.
Lakini jeshi la Lesotho limekanusha kuwa limejaribu kupindua serikali.
Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg anasema hali sasa imekuwa shuwari katika mji mkuu, Maseru.
Lesotho ni nchi iliyozungukwa kabisa na Afrika Kusini na inaitegemea sana Afrika Kusini kwa ajira na pato.
BBC/SWAHILI

NAWAKUMBUSHA TU: NYERERE ALIWAAMBIA MALECELA NA KOLIMBA WAJIUZULU, WAKAGOMA!


Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM (hayati) Horace Kolimba akisalimiana na (hayati) Baba Mtakatifu Papa John Paul II wakati kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki Duniani alipozuru nchini Tanzania Oktoba 1990.


Kosa kubwa la Rais (na ni kosa kubwa), ni kule kukubali kushirikishwa kosa, badala ya kuwafukuza wale waliomshauri ashiriki kosa lao. Waziri Mkuu aliposhindwa kupinga hoja ya Utanganyika alipaswa kujiuzulu; lakini aliposhindwa kufanya hivyo, na badala yake akamshauri Rais naye akubali kuwa geugeu, Rais angemfukuza pale pale na kuteua Waziri Mkuu mwingine. Rais hakufanya hivyo; na badala yake Rais naye akakubali kweli kuwa geugeu na kushiriki kosa la washauri wake.
Lakini kosa hilo la Rais, pamoja na ukubwa wake wote, haliwezi kufuta kosa la awali la washauri wake na hoja ya kuwataka wawajibike kwa kosa hilo. Na sasa wanalo kosa la nyongeza Ia kumfikisha Rais katika hali ngumu na ya fedheha; na kuiingiza nchi yetu katika mabishano ya chuki zinazoweza kuigawa. Pengine inafaa niseme kwamba inashangaza na kutisha kidogo kuona kuwa kujiuzulu kwa Waziri ye yote kunafanywa kuwa ni jambo la kuvutana au kubembelezana. Ndugu Ali Hassan Mwinyi aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani katika Serikali ya Muungano. Makosa fulani yalifanyika katika Wizara yake. Hakuwa ameyafanya yeye; yalikuwa yamefanywa na watendaji fulani walio chini ya Wizara yake. Alilazimika kubeba lawama, akajiuzulu. Nadhani kuna wengine waliolazimika kujiuzulu kutokana na mkasa huo huo.
Wala kubadili Waziri Mkuu si jambo la ajabu. Ndugu Rashidi Mfaume Kawawa alikuwa Waziri Mkuu wangu kwa muda mrefu. Hakuwa amefanya kosa lolote; lakini nilitaka kumbadili na kuteua Waziri Mkuu mwingine. Nilimwita, nikamwambia hivyo. Tukakaa pamoja, mimi na yeye, tukashauriana na kukubaliana ni nani anafaa kushika nafasi yake. Nikamteua hayati Edward Moringe Sokoine: Najua kuwa watu wa aina ya Rashidi Kawawa ni adimu sana duniani, hawazaliwi kila siku; lakini hata hivyo ni jambo la kushangaza kidogo kwamba viongozi wetu wa Mageuzi, hata bado hatujafa, wanaona kuwa ni kosa kuwakumbusha kuwa vyeo walivyo navyo ni dhamana. Wanadhani kuwa uwaziri ni usultani: ukisha kuwa sultani utakufa sultani! Nadhani wanakosea.
Nchi hii imewahi kung'oa masultani wa kila aina. Tukianza kuvumilia masultani wa kuchaguliwa tutapanda mbegu ya masultani wa kuzaliwa.
Narudia: kumbadili Waziri, hata Waziri Mkuu, si jambo la ajabu. Anaweza kujiuzulu, anaweza kufukuzwa, na nchi isitikisike. Lakini huwezi kumtikisa Rais wa nchi bila kuitikisa nchi yenyewe. Ni vizuri jambo hili likatamkwa wazi wazi na likaeleweka sawa sawa. Maana watu wengine wananong'ona nong'ona kuwajibika kwa Rais kana kwamba ni jambo la mchezo mchezo tu. Kulazimika kumchukulia hatua Rais wa nchi ni mkasa na balaa kwa nchi yoyote ile. Ndiyo maana tunatakiwa kuwateua na kuwachagua marais wetu kwa uangalifu mkubwa; na ndiyo maana wakisha kuchaguliwa, wanatakiwa wajiheshimu na kuwa waangalifu sana. Ni jambo muhimu kabisa, kwa kweli la kufa na kupona, kufanya kila jitihada ili kujenga na kuimarisha utaratibu na mazoea ya kuchagua na kubadili Rais wa Nchi yetu kwa njia ya kupigiwa kura, baada ya Rais anayetoka kumaliza kipindi chake kimoja au viwili kwa mujibu wa Katiba. Utaratibu mwingine wo wote haufai, na ni lazima tufanye kila lililo ndani ya uwezo wetu kuuzuia. Mnapolazimika kuutumia, ni jambo la kufanyaje, si jambo la kurukia.
Katika suala hili Iililotufikisha hapa tulipo, watu wa kuwajibika ni Waziri Mkuu, kwa sababu zilizoelezwa kwa kirefu kabisa; na Katibu Mkuu wa CCM kwa sababu hizo na zaidi, maana yeye ndiye aliyekuwa Kiongozi na Mchochezi wa chini chini wa hoja ya Utanganyika. Waziri Mkuu alisarenda ili wenzake, wakiongozwa au kuchochewa na Katibu Mkuu, wasije wakamwacha katika mataa.
Waheshimiwa wawili hawa walikwisha kuambiwa kuwa watamsaidia Rais wao kama wakijiuzulu. Aliyewaambia ni mimi, kwa niaba ya Rais. Katika kikao cha mwisho nilichofanya na Rais kabla ya kuondoka Dodoma kuelekea Dar es Salaam, nilimwarifu kuwa nimeufikisha ujumbe wake kwa Washauri wake waheshimiwa. Nilimwambia kwa mdomo na kwa maandishi, kwamba nilihisi kuwa viongozi hao watafanya mshikamano wa kukataa kujiuzulu. Kama watafanya hivyo, nilisema, tatizo litakuwa lake. Lakini kwa sababu tatizo halitakuwa lake kama Ali Hassan, bali litakuwa lake kama Rais Mwinyi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mimi kwa upande wangu sitakubali liishie hapo. Na kama nilivyohisi, kweli walifanya mshikamano na mkakati wa kukataa kujiuzulu na Rais akawakubalia! Nimeambiwa kuwa ama wao wenyewe au wajumbe wao, walitoa kwa Rais sababu mbili kubwa "za kukataa kujiuzulu”:
(i) Kwanza, Waziri Mkuu akijiuzulu katika hali hii, na Rais akalazimika kuteua Waziri Mkuu mwingine kwa kufuata Katiba ya sasa, ati Wabunge, hasa wale "55" watakataa kumpa kibali Waziri Mkuu mpya huyo! Wabunge hawa sasa wanatumiwa kama chaka la kufichia madhambi ya kila mila! Mimi katika ujinga wangu nilidhani kuwa tatizo moja la Rais katika uhusiano wake na Wabunge, linatokana na kutokuwa na Waziri Mkuu aliyechaguliwa kwa utaratibu mpya; na akapata kibali cha Wabunge.
Kumbe Rais akijaribu kusahihisha hali hii ya sasa, ili achague Waziri Mkuu atakayetaka kibali chao, Wabunge hao hao, hasa "Kikundi cha 55", watamgomea kwa kutaka kuwaondolea Saulo wao aliyekwisha kuona mwangaza! Naendelea kuwa Toma!
(ii) Sababu ya pili ya kukataa kujiuzulu: Waheshimiwa wahusika waliyanong'oneza Magazeti, na Magazeti yakatangaza, kwamba ujumbe wa kuwanong'oneza wajiuzulu ulifikishwa kwao na Mwalimu Nyerere: ati wakijiuzulu, itaonekana kuwa Mwalimu Nyerere anaendesha nchi kichini chini kutoka Butiama.
Mtu ye yote aliyesoma maelezo haya mpaka hapa atatambua kuwa sikuwa na sababu ya kusita kwenda kuwanong'oneza waheshimiwa hawa ujumbe wa Rais. Nataka wajiuzulu, kwa sababu nilizozieleza. Katika masuala ya nchi mimi si mpole kama Rais Mwinyi, ndiyo maana tulikubaliana nikamfanyie kazi hiyo. Lakini kisiasa mtu mbaya wako hakunong'onezi kujiuzulu: hupiga baragumu! Pengine anayekunong'oneza kujiuzulu anakutakia mema, na unaweza kujidhuru mwenyewe kwa kufanya ukaidi.
Inawezekana kabisa kwamba Ndugu AIi Hassan Mwinyi, Waziri wa Mambo ya Ndani aliponong'onezwa alijiuzulu hakushangilia. Lakini sina hakika kama angekuwa hapo alipo leo, kama baada ya kunong'onezwa hivyo angetafuta hila za kutojiuzulu. Nchi yetu bado changa; bado inajenga misingi na mazoea yatakayowaongoza viongozi wetu katika kutuongoza, na wananchi wetu katika kuwahukumu viongozi wao. Jitihada za kujaribu kusaidia kujenga maadili ya viongozi wetu lazima ziendelee.
Waziri Mkuu si mpishi wa Rais, hala tuseme kuwa maadamu Rais mwenyewe anayapenda mapishi yake, sisi wengine tusipoyapenda si kitu. Waziri Mkuu ni Mpishi Mkuu wa Tanzania nzima. Kama hatupendi mapishi yake, au kuanza kutupakulia vyenye sumu, au kachoka, au kashindwa kupika, ni wajibu wetu kumwambia mwajiri wake ateue mpishi mwingine.
Narudia: sababu peke yake nilizoambiwa za kutojiuzulu kwa viongozi wahusika ni hizo mbili nilizozitaja. Lakini sikusikia wala sijasikia kwamba ama wao wenyewe au wajumbe wao, walimwambia Rais kuwa hawastahili kujiuzulu au kufukuzwa ikiwa watakataa kujiuzulu. Na hilo ndilo muhimu; mengine yale ni hila tu za kuwatia watu kiwi na kiinimacho.


REJEA: NYERERE, J.K.; UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA (1994)

BAVICHA NJOMBE WAMPIGIA CHAPUO MBOWE


TAMKO LA VIJANA NCHINI KUMSIHI MWENYEKITI FREEMAN MBOWE AGOMBEE TENA NAFASI HII YA UENYEKITI WA CHAMA CHETU.

Tamko hili ni la vijana wote wa CHADEMA nchi nzima. Linasomwa hapa mbele ya hadhara hii kwa niaba ya vijana hao ambao wanayo hamu kubwa ya kumuona Mwenyekiti Freeman Mbowe akiwania tena nafasi hiyo ili akiongoze chama kwa miaka mingine mitano.
Vijana wa CHADEMA kwa moyo mmoja, kwa ari kubwa na dhamira njema kabisa ikichochewa na mapenzi makubwa kwa chama chetu kinachobeba matumaini ya Watanzania, tumeamua kuwaunga mkono Wazee wa Kigoma ambao walituwahi katika kumchukulia fomu Mwenyekiti Mbowe ili kumshawishi na kumuomba agombee tena.

Kama vijana bado tunaona haja ya kumtaka Mh Freemani Aikael Mbowe kuendelea kukilea chama na kukiongoza hadi tutakapo fikia malengo ya kushika dola kwani msukumo wetu ni uhalali wake kuongoza lakini pia mafanikio makubwa ambayo yameendelea kuonekana katika juhudi zake kama mwenyekiti wa CHADEMA hadi sasa.

Sisi vijana ndani ya Chama chetu tumekuwa tukitafakari sana kipindi hiki ambacho chama kinapitia katika wakati mgumu kutokana na juhudi kubwa za serikali kuhujumu demokrasia na kujenga hofu kwa wanachadema, pamoja na uwepo wa wengi wenye nia ya kukiongoza chama bado tunahitaji weledi na ujasiri wa Mheshimiwa Mbowe kuwa Mwenyekiti wetu hadi hapo tutakapofikia malengo yetu makubwa ya kushika dola na kuwakomboa watanzania kutoka katika serikali ya kidhalimu ya sasa.

Hadi tunafikia kutoa tamko hili tunatambua Uongozi ni utumwa lakini pia tunatambua sana Mheshimiwa Freeman Mbowe amekuwa akifanya kazi za chama kwa kujituma na hivyo ni haki yake kuhitaji msaada kwa sasa ili pia apate fursa ya kupumzika, lakini kama vijana bado tuna uhitaji mkubwa wa kuona chama kinazidi kung’ara hadi kufikia malengo ya kuwakomboa watanzania, hivyo tumefikiri kwa kina kama vijana na kuona kuna haja ya kutoa wito kwa Mwenyekiti wetu wa Chama Mheshimiwa Freeman Mbowe kuona umuhimu wake kwa sasa katika kipindi hiki ambacho chama kinapita katika misukosuko ya kushambuliwa na watawala kwa visa vya kutaka waendelee kubaki madarakani, pamoja na kutambua haki yake ya kutokugombea nafasi hiyo, lakini kama vijana ambao tumekuwa inspired na kuingia katika harakati hizi za siasa na tumejikuta tukishiriki katika kutetea maslahi ya umma, tunaona ni sahihi kabisa kwa mheshimiwa Mbowe kusikia kilio chetu na kuweza kukubali kuingia katika kinyang’anyiro cha kugombea nafasi hiyo ya uenyekiti wa chama ili aweze kuifikisha chadema tunaponuia ifike kwa maana ya kushika dola.

Sisi vijana tunarejea rekodi kubwa ambayo mwenyekiti wa chama chetu ameivunja katika utendaji wake uliotukuka ndani ya CHADEMA hususani mafanikio makubwa tuliyonayo sasa kwa chama kusambaa nchini kote, ongezeko la wabunge na madiwani, katika chaguzi za mwaka 2005 na 2010 lakini pia ustahimilivu wa chama kama taasisi ya kisiasa pamoja na mafanikio haya ndio msukumo wetu kuhitaji uwepo wake kama mwenyekiti wetu kwani pamoja na kelele za watawala kudai CHADEMA kitakufa ifikapo 2015 lakini aliendelea kuwa kiongozi imara huku chama kikizidi kuimarika kila kona ya nchi.

Tunatoa wito kwa vijana wote kote nchini wenye nia na mapenzi ya dhati watafakari yote yaliyofanywa kwenye uongozi wa mwenyekiti Mbowe na wapime kwa busara iliyojaa hekima kwa mustakabali wa chama chetu.

Vijana wa CHADEMA kwa sasa tunasema “kwa CHADEMA,Mbowe anatosha kwa sasa” 

Emmanuel Masonga,
Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Njombe.

Kny; Vijana wa CHADEMA nchi nzima.

WAKURUGENZI WIZARA YA MALIASILI WAPANGULIWA!

Tembo wakipambana na Fisi. Matukio kama haya ni kivutio kikubwa kwa watalii kwenye mbuga na hifadhi zetu.

Dar es Salaam. Serikali imefanya mabadiliko makubwa ya wakurugenzi wanane wa Wizara ya Maliasili na Utalii akiwamo aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Wanyamapori, Paul Sarakikya ambaye amehamishiwa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (Tawiri).
Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na baadhi ya wakurugenzi waliohusika katika uteuzi huo, zinaeleza kuwa mabadiliko hayo yalifanyika hivi karibuni na barua za kutekeleza majukumu yao mapya walipewa juzi.
Hata hivyo, Waziri wa wizara hiyo, Lazaro Nyalandu alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema atalizungumzia Jumatatu ijayo.
Taarifa kutoka ndani ya wizara hiyo, zilieleza kwamba barua ya mabadiliko hayo imeandikwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -Utumishi, George Yambesi.
Akizungumza na gazeti hili jana Yambesi alisema, “Taratibu za uteuzi wa wakurugenzi ndani ya wizara ziko wazi kwamba zinafanywa na katibu mkuu wa wizara hivyo (Maimuna Tarishi) hivyo naomba mtafuteni yeye.” Hata hivyo Tarishi hakuweza kupatikana kuzungumzia mabadiliko hayo.
Katika mabadiliko hayo, aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Wanyamapori, Profesa Alexander Songorwa amepelekwa kuwa Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Afrika, Mweka na mkurugenzi mpya ameteuliwa kuwa Herman Keraryo aliyekuwa mkurugenzi msaidizi wa idara hiyo.
Aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori, Profesa Jafari Kidegesho amepelekwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (Sua).
Dk Charles Mulokozi aliyekuwa Kaimu Mkuu Msaidizi Matumizi Endelevu Wanyamapori anabaki katika nafasi hiyo na Julius Kidede amepelekwa Ngorongoro kupangiwa majukumu mengine ya kazi.
Mkuu wa Kitengo Kidogo cha Migogoro cha Wanyamapori ameteuliwa David Kanyata na Faustine Masalu akiteuliwa kuwa Mkurugenzi Uzuiaji Ujangili nchini, awali alikuwa Mkuu wa Kikosi cha Kuzuia Ujangili Kanda ya Mashariki- Dar es Salaam.
Kwa upande wake Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa akizungumzia mabadiliko hayo, alisema kubadilishwa kwa wakurugenzi hao ni jambo zuri lakini haliwezi kuleta ufanisi endapo Ikulu itaendelea kuingilia utendaji wa wizara hiyo.
“Bado watendaji wa juu wanaingilia utendaji kazi wa wizara, katika hotuba yangu bungeni nilipendekeza wakurugenzi hao kuchukuliwa hatua jambo ni jema, lakini bado wizara hii ina matatizo lukuki ambayo ili kuyamaliza kunahitajika kufanyika kwa ushirikiano wa wadau wote,” alisema Msigwa ambaye ni Mbunge wa Iringa Mjini kupitia Chadema.
Akizungumzia uteuzi huo, Keraryo alisema ameupokea kwa furaha na kuahidi kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na kanuni zinavyomtaka kutenda.
“Nimejipanga kuendeleza mazuri aliyoacha(Profesa Songorwa), nitatekeleza majukumu yangu kwa kuzingatia kanuni na sheria na kama kutatokea mengine hiyo itakuwa nje ya uwezo wangu,” alisema Keraryo
Utekelezaji wa Operesheni
Mabadiliko haya yanatokea mwaka mmoja, tangu mawaziri wanne kung’olewa katika nafasi zao kutokana na Operesheni Tokomeza Ujangili kukumbwa na kashfa ya kukiuka haki za binadamu.
Mawaziri hao ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David Mathayo.
Mbali na mawaziri hao, Kamati ya Bunge Desemba 22 mwaka jana ilipendekeza Serikali kuwawajibisha watendaji waliozembea kwenye Operesheni hiyo.
Mei 2 mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete aliunda Tume ya Uchunguzi, kuhusu vitendo vilivyotokana na Uendeshaji wa Operesheni hiyo.
Rais aliunda Tume hiyo kwa mujibu wa kifungu cha tatu cha Sheria ya Uchunguzi Sura ya 32.
Sakata lilivyoanza
Februari 24 mwaka huu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alitangaza kuubadili uongozi wa Idara ya Wanyamapori ya Wizara hiyo ikiwa ni utekelezaji wa mapendekezo ya Kamati Teule ya Bunge ya kuitaka Serikali kuwawajibisha watendaji waliohusika na uzembe huo.
Nyalandu alisema Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Profesa Songorwa alitangaza kumwondoa katika nafasi hiyo kutokana na tuhuma za uzembe na ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa Operesheni Tokomeza Ujangili.
Waziri huyo alimteua Paul Sarakikya kukaimu nafasi hiyo huku akimwondoa Profesa Jafari Kidegesho katika nafasi ya Mkurugenzi Msaidizi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori na kumteua Dk Charles Mulokozi kukalia kiti hicho.
Pia, alimteua Julius Kibebe kuwa Mkurugenzi Msaidizi Uzuiaji – Ujangili nafasi ya aliyekwenda kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Wanyamapori.
Katika mabadiliko hayo, Nebbo Mwina aliendelea kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo, Utafiti na Takwimu huku Herman Keiraryo anaendelea kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Uendelezaji wa Wanyamapori.
Warudishwa kazini
Mei mwaka hu, agizo la Waziri Nyalandu la kuwasimamisha kazi vigogo hao lilitenguliwa baada wakurugenzi hao kurejeshwa katika nyadhifa zao.
Taarifa kutoka ndani ya wizara hiyo zilieleza kwamba watendaji wote waliokuwa wamesimamishwa kazi walirejeshwa na katibu mkuu wa Wizara hiyo, Maimuna Tarishi jambo lililozua mvutano baina ya Nyalandu na Tarishi kutokana na kupingana kwa maauzi.

RASIMU YA WARIOBA YABAKI MIFUPA


Dodoma. Kamati za Bunge Maalumu, zimekamilisha kazi ya kujadili na kuchambua Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, huku ikiwa imefanyiwa mabadiliko makubwa tofauti na ilivyokuwa awali.
Wajumbe wanatarajiwa kuanza kukutana kama Bunge zima kuanzia Jumanne ijayo, Septemba 2, 2014 wakati kamati zitakaposoma taarifa zake baada ya kufanya uchambuzi wa sura 15 za Rasimu ya Katiba kwa zaidi ya wiki tatu, huku yakitarajiwa mabadiliko makubwa.
Mabadiliko yaliyofanywa yameondoa mambo makubwa yaliyokuwa yakiifanya rasimu hiyo kuonekana mpya, hivyo sasa baadhi ya wachambuzi wa mambo wanaiona rasimu kama ‘Katiba ya 1977 iliyofanyiwa marekebisho.’
Mwelekeo wa kubadili karibu misingi yote muhimu iliyojengwa na tume iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba akiwa mwenyekiti, ilianza baada ya kuwekwa kando kwa mfumo wa muungano wa Serikali tatu uliopendekezwa na badala yake kurejea katika muundo wa sasa wa serikali mbili.
Uamuzi huo uliathiri mtiririko na muundo mzima wa sura na ibara za rasimu hiyo, kwani sasa wajumbe wa Bunge Maalumu walilazimika kutengeneza Katiba yenye mwelekeo wa serikali mbili na siyo tatu tena zilizokuwa zimependekezwa na tume.
Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad aliwahi kuliambia gazeti hili kwamba mwelekeo wa uchambuzi wa rasimu kwa sura hizo 15, lazima ufuate kile ambacho kamati zilikiamua katika uchambuzi wa awali wa sura ya kwanza na ya sita.
Miongoni mwa mambo ambayo yameachwa baada ya kurejesha mfumo wa serikali mbili ni muundo wa uongozi wa juu wa nchi hususan nafasi ya Makamu wa Rais, muundo wa Bunge la Jamhuri, kupunguzwa mamlaka ya Rais, uwajibikaji na uwajibishwaji wa wabunge na ukomo wa ubunge.
Kadhalika, habari kutoka ndani ya kamati zilisema suala la kuwekwa kwa maadili ya uongozi kwenye Katiba nalo lilizua mjadala mkali kutokana na baadhi ya wajumbe kutaka liondolewe kwa maelezo kwamba linapaswa litajwe kwenye sheria na siyo Katiba.
Mambo ya muungano
Miongoni mwa mambo ambayo kuna kila dalili kwamba yatabadilika ni Bunge Maalumu kuongeza mambo ya muungano kutoka saba yaliyopendekezwa na tume na huenda idadi yake ikazidi 22 yaliyomo kwenye Katiba ya sasa.
 Uchunguzi wa gazeti hili uliofanywa katika baadhi ya kamati za Bunge hilo na kuthibitishwa na baadhi ya wenyeviti wake, umebaini kuwa yapo mapendekezo ya mambo ya muungano kuongezwa, tofauti na mtazamo wa awali kwamba yangepungua kama moja ya njia za kuondoa kero za muungano.
Tume ya Jaji Warioba ilipendekeza mambo saba tu kwenye orodha ya muungano chini ya mfumo wa Serikali tatu, mfumo ambao hata hivyo ni dhahiri umeshawekwa kando na Bunge Maalumu na kurejesha muundo wa serikali mbili.
Mambo yaliyopendekezwa na tume hiyo ambayo yapo kwenye sura ya 17 ya Rasimu ya Katiba inayohusu masharti ya mpito ni pamoja na Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Uraia na Uhamiaji.
 Mengine ni Sarafu na Benki Kuu, Mambo ya Nje, Usajili wa Vyama vya Siasa na Ushuru wa Bidhaa na mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na Mambo ya Muungano.
 Mapendekezo hayo yaliyaacha nje mambo mengine 15 yaliyopo kwenye Katiba ya sasa ambayo ni polisi, mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari, mikopo na biashara ya nchi za nje, utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano, bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu na leseni ya viwanda na takwimu.
Pia yamo elimu ya juu, maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya motokaa na mafuta ya aina ya petroli na aina nyinginezo za mafuta au bidhaa na gesi asilia, Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania, usafiri na usafirishaji wa anga, utafiti, utafiti wa hali ya hewa na  Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano.
 Baadhi ya wenyeviti wa kamati za Bunge Maalumu wamesema kuna kila dalili kwamba baadhi ya mambo yaliyoachwa yatarejeshwa huku kukiwa na mtazamo kwamba mengine yanaweza kuongezwa kutoka nje ya orodha ya sasa.
 Mwenyekiti wa Kamati Namba Tano, Hamad Rashid Mohamed alisema orodha iliyopo kwenye Rasimu ya Katiba ina upungufu mkubwa kwani imeacha mambo mengi ya msingi yenye sura ya muungano.
“Mathalani huwezi kuzungumzia kwamba usalama ni suala la muungano halafu ukaacha mambo ya anga, au ukaacha suala la mitihani, yaani Baraza la Mitihani limeachwa pia suala la utafiti nalo huwezi kuliacha, kwa hiyo orodha itaongezeka,” alisema Mohamed.
Mwingine ni Mwenyekiti wa Kamati Namba Sita, Stephen Wassira alisema kuna mambo mengi ya muungano yaliyotajwa kwenye Rasimu ya Katiba lakini hayako katika orodha iliyowekwa kama moja ya nyongeza kwenye rasimu hiyo.
“Ngoja nikwambie kwamba mambo hayo yataongezeka, hilo halina ubishi na kamati yangu tulijadili kidogo na kesho (leo) tutakutana kumalizia. Ukisoma vizuri ibara kwa ibara, utagundua kuwa kuna mambo mengi kama vile Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ambayo ni chombo cha muungano hata ukiangalia muundo wake,” alisema Wassira.
Alitaja mambo mengine kuwa mahakama ya juu inayopendekezwa kuanzishwa lakini haimo kwenye orodha pamoja na masuala ya elimu ya juu na utafiti.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Kamati Namba nne, Christopher Ole Sendeka alisema kuna kazi kubwa ya kutazama upya orodha ya mambo ya muungano na kwamba suala la usalama wa anga ni moja ya mambo hayo.
Naye Mwenyekiti wa Kamati Namba Moja, Ummy Mwalimu alisema, licha ya kwamba kamati yake haikujadili suala hilo lakini orodha hiyo inaweza kuongezeka kwani kuna mambo mengi yameachwa.
“Leo tulikuwa tunaangalia suala la fedha na kuna mambo ukichuguza humo yanagusa sehemu zote mbili, sisi hatukujadili sehemu hiyo kutokana na kwamba haikuwa kwenye orodha ya kazi tulizopewa ila nadhani tukipata fursa bungeni lazina mambo hayo yaangaliwe,” alisema Mwalimu.
Kamati nyingine ambayo haikujadili suala hilo ni namba tatu ambayo mwenyekiti wake, Dk Francis Michael alisema orodha ya mambo ya muungano iko kwenye sura ya 17 ambayo haikuwa sehemu ya kazi za kamati.

XAVI ALONSO ATUA BAYERN MUNICH

Bayern Munich yamsajili Xavi Alonso kwa miaka 2
Kiungo wa Uhispania Xabi Alonso ameafikiana mkataba wa miaka miwili na klabu ya ujerumani Bayern Munich .
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32 amekubali kuondoka Real Madrid katika misimu mwili ijayo.
Xavi alitokea Liverpool alipojiunga na Real Madrid mwaka wa 2009 na alikuwa ameongeza muda wa miaka 2 katika mkataba mpya aliotia sahihi mwezi Januari Bernabeau .
Hata hivyo haijabainika ni kwanini anaondoka kutoka kwa mabingwa wa ligi kuu ya Ulaya.
Bayern yaandika mkataba wa miaka 2 na Xavi
Aidha kiungo huyo alikuwa ametangaza kustaafu soka ya kimataifa jumatano baada ya kuichezea Uhispania katika mechi 114.
Xavi anatarajiwa kuwahutubia waandishi wa habari ijumaa baada ya kupita uchuinguzi wa siha huko bayern hapo jana(alhamisi).

kiungo huyo ambaye ameshinda kombe la dunia na Uhispani huko Afrika Kusini mwaka wa 2010 alitokea Real Sociedad kabla ya kujiunga na Liverpool 2004 alipoisaidia kushinda ubingwa wa bara ulaya mwaka huo.
BBC/SWAHILI

KENYA YATEKETEZA KILO 370 ZA HEROINE

Maafisa wa usalama nchini Kenya walinasa meli kwa jina Amin Darya mwezi uliopita
Serikali ya Kenya imeharibu shehena ya mihadarati aina ya Heroine iliyokuwa imenaswa katika bahari hindi huko Mombasa mwezi mmoja uliopita.
Hii ni baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutangaza hapo jana kuwa shehena hiyo itaharibiwa na kuzamishwa baharini na meli iliyokuwa imeibeba.
Maafisa wa jeshi la wanamaji walilipua shehena hiyo na kukasikika mlipuko mkubwa baharini kisha meli hiyo ya kigeni aina ya MV Al Noor ikazamishwa.Uharibifu huo wa kilo 370 za heroine ya gharama za ya zidi ya dola milioni 16 za Marekani ulifanyika mwendo wa saa kumi saa za Afrika Mashariki umbali wa maili kumi na nne baharini kutoka katika bandari ya Mombasa.
Walioshuhudia uharibifu huo walijumuisha maafisa wakuu wa polisi nchini Kenya, wale wa kitengo cha kukabiliana na mihadarati, wakuu wa idara za ujasusi wa mataifa kumi na tatu waliokuwa Mombasa kuhudhuria mkutano wa usalama na jeshi la wanamaji.
Awali mahakama kuu ya Mombasa ilikataa kutoa agizo la kuharibu meli iliyokuwa imebeba shehena hiyo.
Jaji aliyeisikia kesi hiyo iliyokuwa imewasilishwa na afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma alisema kuwa hakutaka kuonekana kukinzana na mahakama ya chini ambayo ilikuwa imeelekeza tu shehena hiyo ya heroine iharibiwe.
Maafisa wa usalama wakilinda shehena iliyonaswa katika Amin Darya
Akitoa onyo kali kuhusu matumizi ya dawa za Kulevya rais Uhuru Kenyatta alisema kuwa hatakubali Kenya kuwa sehemu ya kusafirisha dawa za kulevya kutoka mataifa mengine.
Si mara ya kwanza shehena ya dawa za kulevya kunaswa Mombasa na hatua hii inaonekana ni moja ya jitihada za kupambana na matumizi ya dawa hizo.

Mji wa Mombasa na maeneo jirani ni baadhi ya sehemu ambazo zimeathiriwa pakubwa na matumizi ya dawa za kulevya hususan kwa vijana ambao wamekabiliwa na uraibu wa dawa hizo na kupata madhara ya kiafya.
BBC/SWAHILI

WANNE WATIWA HATIANI KWA TISHIO LA KUMUUA NYAMWASA

Wawili kati ya sita walioshitakiwa wamefutiwa mashitaka
Wanaume wanne waliokuwa wameshitakiwa kwa kosa la jaribio la kumuua aliyekuwa jasusi wa Rwanda Generali Faustin Kayumba Nyamwasa, nchini Afrika Kusini wamepatikana na hatia ya kosa hilo.
Nyamwasa alipigwa risasi na kujeruhiwa mwezi Juni mwaka 2010 nje ya nyumba yake mjini Johannesburg. .
Nyamwasa alikimbilia nchini Afrika Kusini miezi kadhaa baada ya kukosana na aliyekuwa mshirika wake Rais Paul Kagame.Washukiwa wengine wawili akiwemo aliyekuwa dereva wake Nyamwasa, walifutiwa mashitaka yao na hakimu Stanley Mkhari aliyetoa uamuzi wa kesi hiyo.
Sady Abdou, Hemedi Denengo Sefu, Amani Uriwani, Richard Bachisa, Hassann Nduli na Pascal Kanyandekwe, ndio wanaume sita waliokuwa wameshitakiwa kwa kupanga njama ya kumuu Nyamwasa. Wote walikanusha madai hayo.
Serikali ya Rwanda imekanusha madai ya kuhusika na jaribio la kumuua Nyamwasa.
Hukumu dhidi yao itatolewa tarehe 10 mwezi Septemba.

Mwandishi wa BBC Nomsa Maseko anasema kuwa Nyamwasa alikuwa mahakamani kusikiliza kesi hiyo.
BBC/SWAHILI

UINGEREZA YALIA NA UGAIDI


Waziri mkuu nchini Uingereza David Cameron
Serikali ya Uingereza inasema kuwa matukio yanayoshuhudiwa nchini Iraq na Syria yameongeza tishio la kufanyika kwa mashambulizi ya kigaidi nchini Uingereza.
Kiwango cha tishio hilo kimeongezeka kutoka kuwa kikubwa hadi kibaya zaidi,ikimaanisha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa shambulizi kama hilo ijapokuwa halitafanyika katika siku za hivi karibuni.
Waziri Mkuu David Cameron amesema kuwa kundi la Islamic State ni tishio kubwa kwa usalama wa Uingereza zaidi ya kundi jingine lolote hapo awali.
Tangu kuzinduliwa kwa mfumo mpya wa kuwatahadharisha raia mnamo mwaka 2006,Uingereza imekuwa ikitishiwa na shambulizi la kigaidi kwa takriban miaka minne kwa jumla na tishio hili ni la tatu kwa ukubwa.
BBC/SWAHILI

WAZIRI MKUU WA LESOTHO AKIMBIA MAPINDUZI, AJIFICHA AFRIKA KUSINI

Jeshi la Lesotho

Waziri mkuu nchini Lesotho Tom Thabane ameiambia BBC kwamba amelitoroka taifa hilo baada ya kupata vitisho vya maisha yake.
Akizungumza kutoka nchini Afrika kusini,Bwana Thabane amesema kuwa vitenmdo vya jeshi nchini humo vimesitisha huduma za serikali na kusababisha mapinduzi.
Uchaguzi uliozongwa na utata nchini humo miaka miwili iliopita ulisababisha kuundwa kwa serikali ya muungano isio dhabiti.Awali Ripoti kutoka mji mkuu wa maseru zilizsema kuwa jeshi lilizingira makao makuu ya polisi na kuzuia matangazo ya radio pamoja na mtandao wa simu katika mji mkuu wa Maseru.
Licha ya mazungumzo ya kuleta amani mnamo mwezi Juni ,hali ya wasiwasi ilitanda huku majirani wa taifa hiilo wakionya dhidi ya mbinu yoyote isio ya kikatiba.

Taifa hilo limezungukwa na Afrika kusini na hutegemea sana jirani yake kwa masli asli pamoja na nafasi za kazi.
BBC/SWAHILI

JEWS FORCED FROM GUATEMALA VILLAGE

Members of San Juan La Laguna's indigenous communityThe indigenous community says its rights must be respected

Some 230 members of an Orthodox Jewish group have begun leaving a village in western Guatemala after a bitter row with the local indigenous community.
The Lev Tahor members were asked to leave San Juan La Laguna after meetings with elders of the Mayan community.
The elders accused the Jews of shunning the villagers and imposing their religion and customs.
The Lev Tahor had settled in the village six years ago as the group searched for religious freedom.
'Self-defence'
Over the last several days they were seen packing their belongings on lorries in preparations for the departure from the village, about 150km (90 miles) west of the capital Guatemala City.
"We are a people of peace and in order to avoid an incident we've already begun to leave," Lev Tahor member Misael Santos told the AFP news agency.
"We have a right to be there, but they threatened us with lynching if we don't leave," he added.
Lev Tahor members prepare to leave San Juan La Laguna on a busThe Lev Tahor are now hoping to find a place to live somewhere else in Guatemala
Lev Tahor members, who practise an austere form of Judaism, also complained that they received threats that water and electricity would be cut if they stayed on.
Meanwhile, the village elders said the Jewish members "wanted to impose their religion" and were undermining the Catholic faith that was predominant in San Juan La Laguna.
"We act in self-defence and to respect our rights as indigenous people. The (Guatemalan) constitution protects us because we need to conserve and preserve our culture," Miguel Vasquez, a spokesman for the elders council, said.
The Lev Tahor said it hoped to settle elsewhere in Guatemala.
Many of the Jewish group members had been living in the village for six years but some had arrived earlier this year from Canada after a row with the authorities.
BBC