Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Sunday, 2 March 2014
RC AWATAKA WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI KAMWE WASISAMBAZE KWA MAKUSUDI
Na Mwandishi wa Brotherdanny5.blog, Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha magesa mulongo amewataka baadhi ya wagonjwa wanaoishi na virusi vya Ukimwi kuhakikisha kuwa wanaishi kwa kufauta masharti ya wataalamu wa afya lakini pia kuachana na dhana ya kuambukiza magonjwa hayo kwa makusudi hasa kwa wale ambao bado hawana maambukizi.
mulongo aliyasema hayo wakati akiongea kwenye uzinduzi wa chanjo kwa kina mama wajawazito mpango ambao unatekelezwa chini ya Shirika la EGPAF.
Alidai kuwa kwa sasa wapo baadhi ya wagonjwa ambao wanatumia mwanya huo kuwajerui wale ambao hawana ugonjwa jambo ambalo sio jema kwenye jamii.
alifafanua kuwa wagonjwa hao wanapaswa kuhakikisha kuwa wanafuta taratibu za wataalamu wa afya lakini pia wahakikishe kuwa kamwe hawaongezi idadi ya wagonjwa zaidi
"jamani ni lazima tufike mahali tuwe na tabia ya uzalendo lakini pia tuhakikishe kuwa tunajiengua kwa kusababisha mtikisiko kwenye taifa kwa ajili ya makusudi tuawalinde wale ambao hawana na wala makusudi kamwe hayawezi kutusaidia sisi bali yanachangia sana kutuangamiza," aliongeza Mulongo.
Naye mganga mkuu wa mkoa wa arusha Frida Mokiti alisema kuwa pamoja na jitiada mbalimbali ambazo zinaendelea kufanyika lakini bado kasi ya maambukizi kwa mkoa wa Arusha ipo juu sana.
Mokiti alifafanua kuwa mkoa umeweza kuweka mikakati mbalimbali ya kupambana na ugonjwa huo ingawaje nao wagonjwa nao wanatakiwa kuepukana na kusambaza kwa makusudi bali wanatakiwa kuchukua tahadhari tena kwa haraka sana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment