Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 26 March 2014

NDANDA YAANDALIWA MAPOKEZI MAZITO


Na Jumanne Juma, Mtwara

Kamati tendaji ya Chama cha Soka mkoani Mtwara (MTWAREFA) jana ilikutana kujadili jinsi ya kuipokea ya timu ya Ndanda FC iliyotinga Ligi Kuu baada ya kumaliza mashindano ya ligi daraja ya kwanza juzi.
Timu hiyo ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Polisi Dar es Salaam na kufikisha pointi 28 ikiwaacha African Lyon kwa pointi moja baada ya Lyon kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Green Warriors ya jijini Dar es Salaam pia.
Kikao hicho kilichofanyika katika hoteli ya Peninsula mjini hapa kiliitishwa na Mwenyekiti wa MTWAREFA Athumani Kambi chini ya kamati tendaji.

Wakazi katika baadhi ya maeneo mbalimbali ya mjini Mtwara jana walionekana kushangilia kwa nguvu huku wakiimba na kusema Ndanda Isembwire kwa lugha Kingoni (ikiwa na maana ya Ndanda inasherehekea kwa mbwebwe).

No comments:

Post a Comment