Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 25 March 2014

SERIKALI YAOMBWA KUSAIDIA WATOTO MIFANANO


Na Mwandishi wa Brotherdanny5.blogspot, Arusha

SERIKALI pamoja na wadau mbalimbali wameombwa  kusaidia watoto mfanano (wenyemtindio wa ubongo) katika sekta ya elimu na mahitaji mbalimbali ili nao waweze kupata maendeleo badala ya kunyanyapaliwa.
Rai hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Meneja wa Benki ya NIC, Mbucha Magawa wakati alipokuwa akitoa msaada wa magodoro, Televisheni na king'amuzi, Unga wa Ugali,Sabuni,Mafuta ya Kupikia,Juice kwenye kituo Dymphna Special School kilichopo eneo la Sakina kwa Idd,Jijini Arusha Alisema ikiwa serikali pamoja na wadau mbalimbali wakishirikiana kwa pamoja huduma muhimu kwa watoto wenye mahitaji hayo zitaweza kuwafikia kwenye vituo wanavyolelewa na kupata elimu bila kubaguliwa.
Alisema benki hiyo imetoa msaada huo kwakutambua  kuwa watoto  hao wanamahitaji mbalimbali ambayo ni muhimu ikiwemo elimu,afya na nk ndio maana wameguswa kutoa msaada huo kituoni hapo kwaajili ya kuwasaidia watoto zaidi ya 40 wanaopata elimu kituoni hapo.
Aliomba wadau mbalimbali pamoja na serikali kutambua vituo vya watoto wenye mtindio wa ubongo na kuwasaidia ili wasiweze kutengwa na jamii kutokana na kuwa na ukosefu wa uelewa kwaajili ya matatizo ya ubongo waliyonayo.
"Watoto hawa wanahitaji elimu na mahitaji mbalimbali na wanastahili kusoma kwani wakipewa elimu wanaweza kujihudumia baadhi ya mambo ndio maana Benki ya NIC imeamua kutoa msaada huo na itaendelea kutoa misaada mbalimbali kadri watakavyojaliwa kutoa kwaajili ya watu wenye mahitaji mbalimbali''.
Naye Mmiliki wa Kituo hicho, Mary Kaswendwe alitoa rai kwa wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwabagua watoto hao bali watoe malezi sanjari na watoto wengine ikiwemo kupata huduma za afya na elimu badala ya kuwaficha majumbani na kuwanyika haki mbalimbali ikiwemo haki ya kucheza.
Alisema kituo hicho kilianza mwaka 2002 kikiwa na watoto wachache hadi kufikia 150 ingawa wengine kwa hivi sasa wamemaliza shule na kujiendeleza katika fani mbalimbali ambazo ni za ushonaji,utengenezaji wa bidhaa  mbalimbali zinazotokana na shanga na hivi sasa kituo hicho kinawatoto zaidi ya 40 ambao hutokea maeneo mbalimbali kwaajili ya kupata elimu pamoja na kufundishwa stadi za kazi.
Naye mmoja kati ya watoto wanaopata elimu kituoni hapo, Vicent Osward alishukuru benki hiyo kwaajili ya kuwatambua na kuwapa msaada huo na kutoa rai kwa jamii mbalimbali kusaidia watu wenye mahitaji maalum ili nao waweze kufarijika badala ya kuhisi kutengwa.

No comments:

Post a Comment