Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 20 March 2014

HUYU NDIYE TORONGEY, CHAGUO LA CHADEMA CHALINZE


Pwani. Mathayo Torongey ndiye mgombea mteule wa nafasi ya ubunge kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Torongey ni mkazi wa Kata ya Ubena, Chalinze wilayani Bagamoyo na ni mtoto wa mwisho wa kiume katika familia ya watoto watano wa mama  Maria Torongey ambaye alizaliwa mwaka 1978 katika Kijiji cha Mlenge Kata ya Ubena .
Hata hivyo kwa mila za Kimasai, mgombea huyo pia ni mtoto wa 17 kwa upande wa baba mzazi Mzee Mng’unda Ole Torongey  ambaye ni Mkazi wa Mlenge Kata ya Ubena kwa kuwa mzee huyo katika maisha yake amefuata mila na desturi za kabila la Kimasai ambayo inaruhusu kuoa mke zaidi ya mmoja.
Akizungumzia historia yake, Torongey anadai amezaliwa vichakani kwa msaada wa wakunga wa jadi kwa sababu hakukuwapo  na  vituo vya afya vilivyokuwa vikitoa huduma ya uzazi wakati huo kwenye maeneo ya vijijini.
Kutokana na utamaduni wa kabila la Kimasai, Torongey akiwa mdogo mwenye miaka minane, alikuwa akijihusisha zaidi na ufugaji kwa kushirikiana na familia yake akiwamo baba, kaka na hata mama yake mzazi.
Akiwa na umri huo, Torongey anaelezea kuanza darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Mvomero, Kata ya Turiani  na baadaye alifanikiwa kujiunga na Sekondari ya Mvomero mwaka 1997 na kuhitimu elimu ya kidato cha nne mwaka 2000 shuleni hapo.
Baada ya kuhitimu masomo ya sekondari, Torongey alijikita katika ufugaji na aliweza kumiliki zaidi ya mifugo 100 kijijini kwao, mtaji ambao aliupata kutoka kwa wazazi wake .
Hata hivyo mwaka 2006 alianza kupanuka kibiashara na kufungua maduka mawili ya kuuza nyama maarufu kama bucha kijijini hapo na miaka mitatu baadaye alifungua mengine katika maeneo tofauti mkoani Pwani ikiwamo Chalinze ambako alifungua bucha sita na Bagamoyo mjini bucha tatu.
Pamoja na kujikita katika shughuli hizo, mgombea huyo ni baba wa familia ya watoto wawili na mke mmoja ambaye mpaka sasa anaishi katika Kata ya Ubena, Chalinze.
Kuhusu masuala ya siasa, Torongey anasema alianza kupenda siasa mwaka 1999 baada ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere .
Alisema alivutiwa na siasa kutokana na utaratibu katika majukwaa ya kisiasa zlizoonyeshwa katika vyombo vya habari mbalimbali vya televisheni, ikiwamo misemo yake ya kutopenda ubaguzi, ukabila na msisitizo wa kuwapo amani, umoja na mshikamano.

Hamasa hiyo ilimfanya kugombea nafasi ya mwenyekiti wa tawi kupitia Chadema mwaka 2010 ambapo alifanikiwa kuchaguliwa kuwa kiongozi katika Kata ya Sinza B, Dar  es Salaam mwaka huo.
Baadaye kutokana na utendaji wake mzuri wa kazi, alifanikiwa kupanda na kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Vijana Chadema mwaka 2013 nafasi ambayo anayo hadi sasa anapowania kugombea jimbo hilo la Chalinze.
Matarajio yake kisiasa ni kuwa mwanasiasa mpenda maendeleo na mwenye kutetea wanyonge pasipo kusita kudumisha amani na utulivu wa  Taifa la Tanzania.

Anaimani ya kushinda na uwezo wa kuleta mabadiliko anao.
CHANZO: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment