Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 21 March 2014

MAADHIMISHO YA SIKU YA HALI YA HEWA DUNIANI MACHI 23

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

 
Simu: 255 22 2460735/2460706-8
Faksi:   255 22 2460735/2460700                                                       P.O. BOX 3056
Barua pepe: met@meteo.go.tz                                                            DAR ES SALAAM
Tovuti:  www.meteo.go.tz

Unapojibu tafadhali nakili:
Kumb Na: TMA/3000/5/Vol II                                                     17 Machi, 2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA WADAU WOTE

Yah: Maadhimisho ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani
Tarehe 23 Machi, 2014


Kila mwaka tarehe 23 Machi nchi wanachama wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani hujiunga na kuadhimisha kuzaliwa kwa Shirika hilo lililoanzishwa tarehe 23 Machi, 1950 kulingana na kauli mbiu. Kauli mbiu ya mwaka huu ni ’Ushirikishwaji wa Vijana katika Masuala ya Hali ya Hewa’- ”(Weather and Climate: Engaging Youth)”.

Katika kuadhimisha Siku ya Hali ya Hewa Duniani (WMO), Shirika la Hali ya Hewa linawahamasisha vijana ulimwenguni kote kujihusisha na masuala ya hali ya hewa, ili kupata maarifa na uelewa wa hatua za kuchukua katika kipindi hiki cha mabadiliko ya hali ya hewa duniani. Hatua hii ya WMO ni muhimu kwa ustawi wa kizazi hiki na kijacho ili kujenga jamii imara hapo baadae.
Siku ya Hali ya Hewa Duniani ni siku ya kutafakari Juhudi zinazofanywa na Wanasayansi Duniani katika kufahamisha Dunia kuchukua tahadhari juu ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani na athari zake. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inatoa wito kwa vijana wote kubadilika na kuchukua hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa katika kizazi hiki na kuchukua tahadhari ili kizazi kinachokuja waweze kufaidi dunia yenye mazingira bora zaidi. Vijana wote walioko mashuleni  vyuoni na wajasiriamali  washiriki katika kuokoa dunia kutoka kwenye majanga yaletwayo na mabadiliko ya hali ya hewa. Aidha chachu kubwa ni kuhakikisha vijana wanakuwa mstari wa mbele katika kufuatilia taarifa za hali ya hewa zitolewazo na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini.
Kama ilivyo kwa wanachama wengine, Tanzania inaungana nao kuadhimisha siku hii inayofikia kilele tarehe 23 Machi, 2014 kwa kuwakaribisha wananchi wote kutembelea vituo vya hali ya hewa nchini ili kuona shughuli zitolewazo na Mamlaka kuanzia tarehe 21-23 Machi 2014. Aidha, Mamlaka itambelea na kutoa elimu kwa vijana wa baadhi ya shule na vyuo mbali mbali kupitia ofisi zake zilizopo nchini kuanzia tarehe 19-20 Machi 2014. Kutoa statements/makala  za siku hiyo kwenye magazeti, vipindi kwenye radio, na televisheni kuhusu ushirikishwaji wa vijana katika masuala ya hali ya hewa.

Mamlaka inawatakia maadhimisho mema ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani

’Ushirikishwaji wa Vijana katika Masuala ya Hali ya Hewa’
(Weather and Climate: Engaging Youth)


  IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA                                                      


No comments:

Post a Comment