Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 25 March 2014

NAPE AMNADI RIDHIWANI KIKWETE KWA WANA CHALINZE

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Mkoko wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni za kumnadi kumgombea Ubunge jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete ambapo wananchi hao walielezwa kitendo cha kuzuiwa kupiga kura ni sawa na ubakaji wa Demokrasia na CCM itakula sambamba na wabakaji wa Demokrasia.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye pia ndiye Mratibu wa kampeni za mgombea wa CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete akionyesha kadi Chadema  iliyorudishwa na Ndugu Subira Mrisho ambaye alikuwa mhamasishaji wa Chadema katika kijiji cha Mkoko,pia katika kata ya Msata Katibu Kata wa Chadema amerejea CCM anaitwa Mrisho Issa pamoja na mwananchama mwingine anayejulikana Kassim Msakamali wamerejea CCM
 Katibu wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Shaibu Akwilombe akihutubia wakazi wa kijiji cha Mkoko kwenye mkutano wa kumnadi mgombea wa CCM Ndugu Ridhwani Kikwete.
 Mtela Mwampamba akihutubia wakazi wa kijiji cha Mkoko na kuwasihi wananchi hao kutambua mahusiano ya Tanzania na Chama Cha Mapinduzi.
 Diwani wa Kata ya Msata akiwahutubia wananchi wa kiji cha Mkoko wakati wa kumtano wa kampeni wa kumnadi mgombea wa CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete.
 Katibu wa CCM Wilaya ya Kisarawe Ndugu Zena Mgaya akiwa na Shumia Sharif mjumbe wa mkutano mkuu Taifa kutoka wilaya ya Bagamoyo na pia kiongozi wa kampeni kata ya Msata wakiwa kwenye mkutano wa kampeni za CCM kijiji cha Mkoko jimbo la Chalinze.
 Wananchi wa kijiji cha Mkoko wakionyesha picha za mgombea wao wa Ubunge Ndugu Ridhiwani Kikwete wakati wa mkutano wa kampeni ulofanyika kijjini Mkoko.
 Mapokezi ya katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye katika kijiji cha Mkoko.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahtubia wakazi wa kitongoji cha Madesa wakati wa kupiga kampeni za Ubunge.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahtubia wakazi wa kitongoji cha Madesa wakati wa kupiga kampeni za Ubunge ambapo aliwaambia uongozi si kitu cha kujaribiwa hivyo wananchi wakapige kura kwenye chama kilichokuwa na uzoefu wa siasa na maendeleo kwa jumla.
 Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Kihangaiko wakati wa kampeni za kumnadi mgombea wa CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete. 
Kikundi cha Upendo kikitumbuiza wakati wa mkutano wa kampeni za CCM

No comments:

Post a Comment