Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 20 March 2014

MUONE KIJANA ALIYEMUOA MAMA YAKE MZAZI

Wacongo wanasema: "Mokili ekobaluka", yaani Dunia inabadilika au kugeuka! Kisa cha kijana aliyeamua kuwaacha wake zake watatu, halafu akamuoa mama yake mzazi na kuishi kama mke na mume wakipika na kupakua, hakina bado kinawatatiza Watanzania wengi.
Hayumkini wawili hawa waliwaza nini hata wakafikia uamuzi huo. Kijana alipata wapi ujasiri wa kumtongoza, achilia mbali, kumvulia nguo mama yake ama kuona uchi wa mama yake mzazi?
Mama naye mishipa ya aibu ilimkatika akasahau namna alivyobeba mimba ya kijana wake huyo, akahangaika nayo kwa miezi tisa, akamzaa - iwe kwa nafuu ama kwa taabu - akamlea hata amekuwa mtu mzima. Hivi kweli alithubutu 'kumkaribisha' mwanawe 'mahali alipotokea'?
Iwe ni ushirikina au nini, hakika hili ni jambo la aibu na laana kubwa kwa sababu hata Torati ya Mussa inakataza kwa kuwa hayo ni machukizo kwa Bwana Mungu na ni najisi.
Halafu jamaa alikuwa na wakeze watatu, wazuri, lakini akaona uzuri wao hauwezi kumfikia ule wa mama yake! Laanakum!
Siamini kama dunia ndiyo inayobadilika, naamini kwamba wanadamu ndio tunaobadilika. Hata wanyama, wengi wao, hawawezi kufanya vitendo vya aina hiyo. Sembuse binadamu!?
Hongera dada Hoyce Temu kwa kazi nzuri uliyoifanya.

Daniel Mbega,
Iringa, Tanzania
0715 070109

No comments:

Post a Comment