Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 18 March 2014

NTALIMA: NAOMBA MSAADA MWANANGU AKATIBIWE NJE

Angolwisya Ntalima akimsaidia binti yake mwenye matatizo ya kiafya. Picha na Elias Msuya 

Ni tatizo ambalo limewasumbua wazazi wake kwa muda mrefu sasa, kiasi cha kuomba misaada.
Waswahili husema ‘kuzaa si kazi, bali kazi ni kulea’. Kuzaa ni jambo la kawaida kwa wazazi  ambao hufurahia watoto wao. Kwa wale wanaokosa watoto kutokana na sababu mbalimbali inakuwa balaa kwao.
Mwaka 2006 ilikuwa furaha kwa Angolwisye Ntalima kupata mtoto wa kwanza wa kike aitwaye Vera. Hata hivyo furaha hiyo imekuwa ikiyeyuka kadiri mtoto wao anavyokua hadi sasa amefikisha miaka saba.  Mtoto huyo hadi sasa hawezi kusimama, kuongea, wala kujisaidia bila kupata msaada.
“Awali mtoto huyu alipozaliwa alikuwa na afya njema tu,” anasema Ntallima huku akionyesha picha za utotoni za Vera.
“Tulianza kugundua tatizo lake pale alipokuwa akijifunza kusimama na kutembea akiwa na mwaka mmoja na nusu. Alikuwa akisimama kwa vidole na anakosa mwelekeo na kuanguka vibaya.”
Anasema walimwanzishia matibabu Hospitali ya CCBRT ambako alipewa viatu vya kumsimamishia na kumfanyia mazoezi.

Chanzo cha tatizo
Akizungumzia chanzo cha tatizo hilo, Ntalima anasema inawezekana ni wakati wa kuzaliwa kwani mama yake alionyesha dalili zote za kujifungua, lakini hakupata uchungu.
“Madaktari walimchoma sindano ya uchungu tangu saa sita mchana wakamwambia arudi baadaye. Ilipofika jioni nikampeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako aliongezwa sindano nyingine ya uchungu aliyokaa nayo hadi saa 6:00 usiku. Mwisho wakampeleka kwenye upasuaji ambao ulimalizika saa 8:00 usiku na mtoto alikuwa na hali nzuri,” anasema.
Anataja sababu ya pili akisema inawezekana ni ugonjwa wa degedege alioupata akiwa bado mdogo.
Kuhusu mazoezi waliyopata CCBRT, Ntalima anasema licha ya kukamilika, bado hayakumwezesha mtoto wake angalau kwenda shule.

Mbali na CCBRT, Ntallima anasema aliwahi kumpeleka kituo cha YWCA kilichopo Buguruni Malapa kwenye shule ya wenye mtindio wa ubongo, lakini hakupata nafuu.
“Wakati huo nilikuwa nikiishi Kisarawe, hivyo nilikuwa nikimpandisha gari hadi Gongo la Mboto ambako anachukuliwa na gari la shule, kisha namfuata jioni na kurudi naye Kisarawe. Yalikuwa mateso matupu.
 “Mwaka jana nilimpeleka hadi Iringa ambako kuna kituo cha watoto wenye matatizo kama haya, lakini hali ilizidi kuwa mbaya. Ilibidi nimrejeshe baada ya miezi sita tu,” anasema.
Mbali na hayo anasema mazoezi aliyopatiwa yamemwezesha walau kutambaa kwa kuinama na kupata nguvu. Licha ya kuendelea kutokwa na udenda mdomoni na kushindwa kuongea.
“Unavyoona hali hii ni kwa sababu tuliwahi kumpeleka hospitali kufanya mazoezi, vinginevyo angelemaa kabisa. Watu wanaowafungia ndani watoto kama hawa wanaishia kulemaa moja kwa moja,” anasema.
China kwa ajili ya matibabu
Ntallima anasema alikuwa akipitia mitandao ya intaneti ili kujifunza kuhusu ugonjwa huo na alioona anwani ya Hospitali ya Beijing Shizhentang.
“Wanasema moja kati ya huduma zao ni matatizo ya ubongo na wanaweza kutibu kwa asilimia 70 na ukiwahi inaweza kuzidi. Ndipo nikawasiliana nao na kuwaeleza hali niliyonayo,” anasema.
Anasema hospitali hiyo ilimjibu ikimtaka awape historia ya ugonjwa wa mtoto na matibabu aliyopata na kuambatanisha picha mnato na video ili kufafanua tatizo lake.
“Walinijibu kuwa tatizo alilonano ni la ubongo (cerebral pars). Walisema watachukua uboho wa mifupa na kuuwekea dawa kisha kuurudisha kupitia uti wa mgongo. Walifafanua kwamba mzazi atafundishwa jinsi ya kumwongelesha.
 “Waliopata matibabu hayo wanasema ndani ya wiki tatu, mtoto anaweza kuongezeka kwa angalau nusu nchi na atatamka hadi neno la tatu na nguvu kwenye viungo itarejea.”
Anasema gharama za matibabu hayo ni kubwa na hawezi kuimudu. “Kinachonisumbua ni gharama kwa sababu wao wanataka Dola 27,000 za Marekani (sawa na Sh43 milioni) kwa ajili ya matibabu ya wiki nne, malazi ya mtoto na wasindikizaji na baada ya tiba kuna dawa zenye gharama ya Sh3 milioni,” anasema.

Anasema hadi sasa amefanya jitihada za kuomba msaada kwa ajili ya matibabu ya mtoto huyo.
“Mtoto tumemfungulia akaunti Na 015221931200 katika Benki ya CRDB.

CHANZO: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment