Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 20 March 2014

WAZIRI GHASIA AZINDUA MIRADI YA SHS. 2.1 BILIONI ARUSHA


Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot

WAZIRI wa nchi ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI,Hawa Ghasia amezindua miradi miwili mikubwa yenye thamani ya zaidi ya Shs. 2.1 bilioni katika halimashauri ya wilaya ya Arusha,wilayani Arumeru na kutoa rai kwa halmashauri zote nchini kuiga mfano huo kwa kutumia vizuri  fedha za serikali.
Aidha miradi iliyozinduliwa ni pamoja na kukamilika kwa jengo la utawala lenye ukubwa wa Orofa mbili ambapo ujenzi wake umegharimu kiasi cha Shs. 1,044,064,462.96 pamoja na ununuzi wa mitambo minne ya ujenzi wa barabara yenye thamani ya Shs. 1,196,740,472.
Akizungumza kabla ya kuzindua miradi hiyo ,Ghasia aliipongeza halmashauri hiyo kupitia baraza la madiwani kwa ubunifu uliowezesha kupatikana kwa kiasi hicho cha fedha kupitia miradi yake mbalimbali iliyojiwekea ikiwemo ya ugawaji wa viwanja . 
Waziri huyo alitoa onyo kwa halmshauri zingine ambazo zimekuwa hazitumii vizuri fedha za serikali kwa kubuni miradi ya kutafuna fedha za halamshauri ,kwa kueleza kuwa kwa sasa  serikali ipo makuni na haitazifumbia macho na zitashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
''nawapongeza sana madiwani wa halmashauri yenu kwa kubuni miradi na kutumia vizuri fedha zinazopatikana ingekuwa madiwani wengine wangebuni ziara ya kwenda kujifunza hata matumizi yah ii mitambo ilimradi tu watumie hizo fedha ,ila hapa kwenu hamkufanya hivyo,' 'alisema Ghasia.
Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Felix Lumato, alitaja mitambo mine iliyozinduliwa na waziri ghasia kuwa ni pamoja na Caterpillar Vibratory lenye thamani ya Shs. 187,790,000. Hyundai
Crander Excavater (Shs. 291,600,000), Caterpillar Motor Grader (Shs. 576,380,000) na Lori aina ya Tipper (Shs. 79,380,000).
Alisema mitambo hiyo itasaidia sana kuinua hali ya uchumi kwa halmshauri na wananchi kwa ujumla,ambapo alisisitriza kuwa itakuwa inakodishwa kwa wananchi mbalimbali pamoja na kukarabati miundo mbinu ya barabara katika halmashauri hiyo.
Alisisitiza kwa kuiomba serikali ihakikishe fedha wanazoziomba kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ya maendeleo katika halmashauri zitolewe kwa wakati ili kurahisisha utekelezaji wa miradi hiyo kwa wakati waliojipangia.
Katika hatua nyingine mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi Goodluk Ole Medeye aliitaka serikali kuhakikisha inasaidia kugawanywa kwa wilaya ya Arumeru, vijiji, vitongoji na kata ili kurahisisha huduma kwa wananchi na utekelezaji wa maendeleo.
Alisema hivi sasa katika wilaya hiyo kumekuwepo na changamoto kubwa kwa wananchi kupata mahitaji yao muhimu kutokana na umbali ya maeneo ya huduma kwa kueleza kuwa baadhi ya maeneo yapo mbali sana na huduma za msingi. 

No comments:

Post a Comment