Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 26 March 2014

MKUTANO MKUBWA WA CUF KUDAI NCHI YAO LEO


KUMEKUCHA!! SASA MAMLAKA KAMILI NI LAZIMA KAMA HAKUNA 3 NA MBILI HAZIPO WAZANZIBARI WOTE KUKUTANA KIWANJA CHA DEMOKRASIA 26/3/2014

Haya haya wazanzibari! Kumekucha! La mgambo likilia kuna jambo! Chama cha wananchi CUF kinawatangazia wanachama, wapenzi na wazanzibari wote wa mikoa mitatu ya Unguja, wazalendo na wapenda nchi yao kwa jumla kuhudhuria kwa wingi katika mkutano mkubwa wa hadhara wa aina yake , wa kihistoria utakaofanyika siku ya Jumatano ya tarehe 26/03/2014 katika viwanja vya Demokrasia, Kibanda Maiti kuanzia saa 8:00 barabara za Mchana mpaka saa 12:00 za jioni.
Mgeni rasmi katika Mkutano huo ni Nahodha wa safari ya kuelekea katika mamlaka kamili ya Zanzibar, Simba wa nyika, tishio la vibaraka wauza nchi yetu, kipenzi cha wazanzibari, mwenye uzalendo wa hali ya juu na mapenzi makubwa kwa Zanzibar na wazanzibari, Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF, Alhakiir Maalim Seif Sharif Hamad. Mkutano utaanza saa 8:00 barabara za mchana mpaka saa 12:00 jioni.
Agenda kuu katika mkutano ni jee safari ya kuelekea mamlaka kamili imefikia wapi? Jee Kikwete, CCM na vibaraka wachache wa Zanzibar wataweza kutuondosha katika mstari wa madai yetu? Jee mpango wa CCM wa kumtanguliza Warioba kwa kuvunja kanuni za Bunge la Katiba kwa lengo la Kumleta Kikwete kuponda mapendekezo ya Warioba utafanikiwa kusitisha safari hii ya wazanzibari? Nini wazanzibari wanapaswa kutarajia?
Maswali yote hayo yatapatiwa majibu pamoja na mambo kadhaa muhimu. Hatumwi mototo!
Shime wazanzibari wote kuhudhuria kwa wingi bila ya kukosa!
TUNATAKA NCHI YETU SASA TUMECHOKA TAFRANI!
HAKI!


CHANZO: JAMIIFORUMS

No comments:

Post a Comment