Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 25 March 2014

VYOMBO VYA HABARI VIHAMASISHE VYAKULA ASILIA


Na Mwandishi wa Brotherdanny5.blogspot, Arusha

Vyombo vya habari nchini vimetakiwa kutumia nafasi zao katika kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa utumiaji wa vyakula vya asili ili kuweza kuepukana na magonjwa ikiwa ni pamoja na kuujengea mwili kinga itakayowezesha kupata taifa lenye nguvu na afya bora.
Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa shirika lisilo a kiserikali la Women Development for Science and Technology(WODSTA)Bi. Lyin Ukio wakati akizindua lishe konvivia na kufungua mafunzo ya lishe asili yaliyofanyika jijini Arusha.
Ukio alisema kuwa ulaji wa vyakula vya asili umepotea katika nyingi hivyo vyombo vya habari kwa kushirikiana na shirika la WODSTA wanalojukumu la kuelimisha jamii juu ya ulaji wa vyakula vya asili na kuufanya ulaji huo uwe endelevu.
Aidha alieleza kuwa uhamasishaji wa ulaji wa vyakula vya asili unapaswa uanzie katika ngazi ya kitongoji, kijiji, kata, wilaya, mkoa na hatimaye taifa kwa ujumla kwani vyakula hivyo ni muhimu katika maisha ya kila Mtanzania.
"Tafiti zinaonyesha kuwa kwa asilimia 75 ya watu hudhoofika miili na kupata magonjwa kutokana na ulaji wa vyakula vya kisasa hivyo jamii ya kitanzania inapaswa itambue umuhimu wa vyakula na kuvifufua katika jamii," alisema Ukio.
Kwa upande wake mratibu wa mradi wa bustani elfu moja ulio chini ya shirika la Slow Food International Bi.Hellen Nguya wakati akisoma historia ya mradi huo alisema kuwa shirika la slow food lilianzishwa nchini Italia mwaka 1989 ili kukabiliana na chakula cha haraka kilichopelekea vyakula vya asili kusahaulika.
Nguya alieleza kuwa hivi sas shirika hilo lina zaidi ya wanachama elfu kumi (10,000) kutoka nchi 150 waliojumuika katika vikundi vinavyofanya kazi pamoja ili kulinda na kuhifadhi tamaduni zao.
Alifafanua kuwa filosofia ya slow food kuhusu kilimo,uzalishaji na uunganishaji wa utamaduni wa chakula unatokana na dhana ya chakula bora chenye kuegemea mambo matatu yaani Bora,Safi na Haki huku imani ya wanachama wa slow food ikiwani kila binadamu lazima apate chakula bora, safi na haki.
Aidha alisema kuwa shirika hilo huandaa shughuli nyingi na matukio kote ulimwenguni katika kila ngazi ambapo kila mwaka slow food huadhimisha uhamasishaji wa ulaji wa vyakula vya asili katika ngazi mbalimbali kati ya tarehe 7 hadi 10 mwezi desemba ambapo maadhimisho hayo hujulikana kama Terra Madre (Mama Ardhi).
Alieleza kuwa katika mkoa wa Arusha shirika hilo lilianzishwa mwaka 2004 likiwa na wanachama wasiopungua 20 ambao wameunda Konvivi yaani LISHE, akitoa maana ya konvivia hiyo alisema kuwa ni mtandao wa wanachama waliojumuika katika vikundi vidogo wanaofanya kazi kwa pamoja ili kulinda na kuhifadhi tamaduni zao kuhusu chakula.
Hata hivyo kufuatia umoja huo katika nchi ya Tanzania kuna konvivia 6 na zaidi ya konvivia 1300 kote ulimwenguni ndizo uti wa mgongo wa slow food ambapo kuna bustani 8 za shamba darasa chini yamradi bustani elfu moja  wa slow food katika Afrika ambazo ni Themi (WODSTA),Patandi(IKUSURA),Patandi shule yamsingi,Nambala shule ya msingi, Ndatu (KICHALIMPINDA), Ngurdoto (UMANGU), Makumira (WATOTO
OUNDATION) pamoja na Maji ya chai (TMEGA/ALFAJIRI) vyote vikiwa jjijini.

No comments:

Post a Comment