Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 20 March 2014

NMB YAMWAGA MISAADA


Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot,Arusha
BENKI ya NMB kanda ya kaskazini,imetoa msaada wa kompyuta 20 kwa wanafunzi wa shule ya msingi Emaoi, iliyopo Arumeru, mkoni hapa, baada ya kupokea maombi ya uhitaji, zitakazo wasaidia kuboresha elimu na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi hao.
Msaada huo umekabidhiwa mwishoni mwa wiki na meneja wa benki hiyo, Vick Bishubo, kwa mkuu wa shule hiyo,James Ndossi,ambaye aliishukuru benki hiyo na kueleza kuwa msaada huo umekuja wakati mwafaka na utasaidia kwa wanafunzi kuboresha elimu kwa kufundishwa somo la Tehama ambalo hapo awali halikuwa likifundishwa shuleni hapo.
Meneja Bishubo alieleza kuwa Benki ya NMB inatambua umuhimu wa elimu hapa nchini na katika sera zake moja wapo ni kutoa kipaumbele katika nyanja mbalimbali ikiwepo elimu na imekuwa ikifanya hivyo katika shule mbalimbali hapa nchini kwa kuwarejesha faida kidogo kwa jamii, inayoipata kwa kuzingatia uhitaji.
''Tunazingatia uhitaji katika kusaidia jamii,na kipaumbele chetu ni pamoja na kutoa msukumo wa elimu kwa kusidia vifaa mbalimbali,tunafanya hivyo kwa kuzingatia faida kidogo tunayoipata kwa kuirudishia jamii''alisema meneja Bishubo.
Aidha, aliwataka wananchi mbalimbli kuendelea kuiunga mkono benki hiyo kwa kufungua akaunti ikiwemo kuwafunguliwa watoto ili kuiwezesha benki hiyo kujiendesha kwa  faida,ili sehemu ya faida hiyo itarejeshwa na kuisaidai jamii katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo.
Naye Diwani wa kata ya Olmotony,iliyopo katika shule hiyo, David Kinisi alimweleza meneja huyo kuwa katika kata hivyo kunajumla ya shule za msingi tatu ,ambapo kwa ujumla zinakabiliwa na changamoto ya upungufu wa wastani wa madawati madawati 300 kila moja.
Alisema suala la Kompyuta ni muhimu sana kwa maendeleo ya mwanafunzi kujifunza hasa katika kipindi hiki cha teknolojia ya kisasa, kwani kutazidisha uelewa kwa wanafunzi,ila aliiomba benki hiyo na wahisani wengine kuona umuhimu wa kusaidiaa suala la madawati.
''Mwaka jana NMB imetupatia madawati 80 katika kata yangu ila shule bado zinakabiliwa na upungufu wa madawati zaidi ya 1000 ,tunachoomba benki isichoke kutusaidia bado tunachangamoto kubwa ,tunashukuru sana na kutupatia kompyuta hizi ni muhimu sana kwa maendeleo ya shule zetu na zitaongeza bidii ya kujifunza''alisema Diwani.
Aliongeza kuwa katika shule tatu za msingi zilizoko katika kata hiyo ambazo ni Emaoi,Olmotony na Olkonerei zinaupungufu wa nyumba za walimu 63 hali ambayo inasababisha kutokuwa na walimu wa kutosha kutokana na mazingira magumu ya kuishi kwa walimu hao.
Naye mmoja wa wanafunzi hao,Jackson Mollel wa darasa la tano aliishukuru benki hiyo kwa kuwawezesha kuwapatia kompyupa kwani alisema  hakuwahi kutumia kompyuta ila kwa sasa anaamni zitamwezesha kujifunza zaidia na kumwongezea bidii ya kusoma.

No comments:

Post a Comment