Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 20 March 2014

MABILIONEA WENYE UMRI MDOGO DUNIANI

Bilionea Mark Zuckerberg

KUFIKIA kiwango cha utajiri wa Dola 1 bilioni siyo mashindano, lakini baadhi wanafikia hapo haraka na kwa urahisi tu. Kati ya mabilionea 1,645 walioko kwenye orodha ya Forbes, 31 wana umri wa chini ya miaka 40. Kundi hilo haliwahusishi vijana matajiri wa Google, Sergey Brin na Larry Page, ambao tayari wamekwishavuka miaka 40.
Katika orodha ya mwaka huu 2014, yupo bilionea mdogo zaidi mpya. Perenna Kei, binti ambaye hajulikani sana, amempiga kumbo muasisi mwenza wa Facebook Dustin Moskovitz ambaye alikuwa bilionea mdogo zaidi.
Akiwa anatokea Hong Kong, Kei ana asilimia 85 kwenye kampuni ya Logan Property Holdings kupitia kwenye kampuni kadhaa pamoja na mfuko wa familia. Baba yake, Ji Haipeng, ndiye mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo ambayo imeandikishwa kwenye Soko la Hisa la Hong Kong, ambayo ilianza kuuza hisa zake mwezi Desemba 2013.
Mabilionea 39 wadogo waliomo kwenye orodha ya mwaka 2014 wana utajiri wa pamoja wa Dola 115.7 bilioni. Wafanyakazi wa Facebook, wakiwemo Sean Parker, Mark Zuckerberg na Jan Koum wa WhatApp – wana asilimia 42 ya kiasi hicho. Koum, ambaye ni mpya kufuatia Facebook kuamua kuinunua WhatsApp, ana utajiri wa Dola 6.8 bilioni. Aliiuza kampuni yake hiyo ya mtandaoni kwenye kampuni ya Menlo Park, ya California kwa Dola 19 bilioni katika hisa na fedha taslimu mwezi Februari 2014.
Matajiri ‘watoto’ 13 kwenye orodha hiyo wanatokea Marekani. Ifuatayo ndiyo orodha kamili kwa mwaka 2014:

1: Perenna Kei & familia
Umri: 24
Utajiri: Dola 1.3 bilioni
Taji la bilionea mdogo kabisa duniani linakwenda kwa Bi. Perenna Kei, ambaye ana asilimia 85 kwenye kampuni ya Logan Property Holdings kupitia kwenye kampuni kadhaa pamoja na mfuko wa familia. Baba yake, Ji Haipeng na ndiye mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Logan Property Holdings. Zamani akijulikana kwa jina la “Ji Peili,” Kei siyo mkurugenzi mtendaji kwenye kampuni hiyo, ana shahada  katika uchumi na fedha kutoka Chuo Kikuu cha London.

Umri: 29
Utajiri: Dola 6.8 bilioni
Dustin Moskovitz

Kwa sasa siye bilionea mdogo duniani, Dustin Moskovitz atatimia miaka 30 mwaka huu. Rafiki mkubwa wa Mark Zuckerberg waliyekuwa wakiishi chumba kimoja, Moskovitz alisaidia kuanzishwa kwa mtandao wa kijamii wakitokea kwenye bweni lao katika Chuo Kikuu cha Harvard, akiacha chuo baada ya miaka miwili na kufanya kazi ya kudumu kama mwajiriwa wa tatu wa Facebook. Aliachana na Facebook mwaka 2008 na kuanzisha Asana, kampuni ya software ambayo inawasaidia watu kuboresha kazi zao katika miradi. Alioa mwaka jana kwa mpenzi wake wa miaka mingi Cari Tuna.

3: Mark Zuckerberg
Umri: 29
Utajiri: Dola 28.5 bilioni
Facebook imetimia miaka 10 mwaka huu na hakuna aliyekuwa anasherehekea kwa nguvu kama Mtendaji Mkuu Mark Zuckerberg. Baada ya kuinusuru kampuni yake katika kipindi kigumu cha IPO Mei 2012, Zuckerberg ameisaidia kampuni hiyo kutoka Menlo Park, California kuendelea kupaa. Hisa za Facebook zimepanda hadi kufikia 130% kwa mwaka jana tu hadi kufikia katikati ya Februari mwaka huu. Hii imefanya utajiri wake uongezeke mara mbili pamoja na kutoa hisa 18 milioni mwishoni mwa Desemba. Aliuza zaidi ya hisa 41 milioni na kupata mbadala wa hisa 60 milioni katika kipindi hicho hicho.

4: Anton Kathrein, Jr
Umri: 29
Utajiri: Dola 1.35 bilioni
Anton Kathrein, Jr. ni uzao wa nne kuongoza kampuni ya familia ya Kathrein-Werke AG– ”kampuni kongwe na kubwa zaidi ya uzalishaji wa antenna duniani,” kwa mujibu wa wavuti ya kampuni hiyo. Kampuni hiyo pia inatengeneza antenna za radio na TV, satellite na mfumo wa mawasiliano na vifaa vinginevyo ulimwenguni. Kampuni hiyo ina vituo 18 duniani, wafanyakazi 6,800 na pato la Dola 1.8 bilioni kwa mwaka 2012 ilianzishwa na babu yake Kathrein mwaka 1919. Anton Sr aliiongoza kampuni hiyo kuanzia mwaka 1972 hadi 2012 alipofariki.

5: Drew Houston
Umri: 30
Utajiri: Dola 1.2 bilioni

Young and wealthyMvumbuzi wa Dropbox na Mtendaji Mkuu Drew Houston ni kijana mgeni katika orodha hii ya mabilionea. Amejiunga na klabu ya mabilionea mwaka huu baada ya kampuni yake yenye makao makuu San Francisco kuongeza mtaji mwezi Januari wenye thamani ya Dola 10 bilioni.  Houston alianzisha Dropbox kwa kushirikiana na Arash Ferdowsi mwaka 2007. Houston alianza ucheza na kompyuta tangu akiwa na miaka 5 na akaendelea hivyo hadi shuleni.

Umri: 30
Utajiri: Dola 3.8 bilioni
Japokuwa alionekana kwa mara ya kwanza kwenye orodha ya mabilionea ya Forbes akiwa na miaka nane, Albert von Thurn und Taxis, prince wa 12 katika familia ya kifalme, alirithi rasmi utajiri mwaka 2001. Rasilimali zake ni pamoja na majengo, sanaa na hekta 36,000 za miti nchini Ujerumani, mmoja ya misitu mikubwa barani Ulaya. Bado hajaoa na anaishi katika hekalu la familia mjini Bavaria, katika eneo la Schloss Emmeram, na anapenda kuendesha magari yaendayo kasi.

7: Scott Duncan
Umri: 31
Utajiri: Dola 6.3 bilioni
Scott Duncan ni mmoja wa mabachela wakongwe wa Texas na mmoja wa warithi wanne mradi mkubwa wa bomba la nishati uliojengwa na marehemu baba yao, Dan Duncan. Utajiri wake umeongezeka kwa Dola 1.2 bilioni kulinganisha na mwaka uliopita katika bei ya hisa ya Enterprise Products Partners. Baba yake, ambaye alikuwa tajiri mkubwa kuliko wote jijini Houston, alifariki mwaka 2010 akiwa na umri wa miaka 77.

8: Eduardo Saverin
Umri: 31
Utajiri: Dola 4.1 bilioni
Mvumbuzi mwenza wa Facebook Eduardo Saverin, ambaye alizaliwa nchini Brazil, amekuwa akiishi nchini Singapore tangu alipoukana uraia wake wa Marekani mwaka 2012.

9: Yang Huiyan
Umri: 32
Utajiri: Dola 6.9 bilioni
Mwanamke tajiri kuliko wote nchini China, Yang Huiyan ni makamu mwenyekiti wa kampuni ya uendelezaji majengo ya Country Garden. Alipewa sehemu ya mali za baba yake kwenye kampuni ya Country Garden kabla ya kampuni hiyo kuanza kuuza hisa mwaka 2007, mwaka ambao pia aliingia kwenye orodha ya Forbes akiwa Mchina tajiri kwa kumiliki Dola 16 bilioni.

10: Fahd Hariri
Umri: 33
Utajiri: Dola 1.2 bilioni
Fahd Hariri ndiye mtoto wa mwisho wa kiume wa Waziri Mkuu wa Lebanon, Rafik Hariri. Alipata shahada ya uhandisi katika Chuo Kikuu cha Ecole Spéciale d’Architecture de Paris mwaka 2004. Wakati inaripotiwa kwamba hajawahi kukanyaga ardhi ya Beirut tangu baba yake alipouawa mwaka 2005, anaendelea majengo ya makazi huko kwa heshima ya baba yake.

Umri: 33
Utajiri: Dola 2.7 bilioni
Marie, 33, pamoja na ndugu zake Emmanuel, 43, na Jean-Michel, 46, walirithi kampuni kubwa ya maziwa Ufaransa ya Lactalis, wazalishaji wa maziwa ya Président brie pamoja na siagi za aina mbalimbali, maziwa na mtindi. Wote kwa pamoja wanamiliki asilimia 100 ya kampuni hiyo ambayo babu yao aliianzisha katika miaka ya 1930.

12: Sean Parker
Umri: 34
Utajiri: Dola 2.4 bilioni
Mwezi Juni 2013, muasisi wa Napster na rais wa zamani wa Facebook Sean Parker alimuoa mwimbaji Alexandra Lenas katika sherehe ya kifahari iliyofanyika kwenye msitu wa Big Sur, California. Harusi hiyo iligharimu Dola 4.5 milioni.
Mabilionea wengine wadogo, umri na utajiri wao kwenye mabano ni: Julia Oetker (Miaka: 35 na Utajiri: Dola 1.65 bilioni); Robert Pera (Miaka: 35 na Utajiri: Dola 2.7 bilioni); Ayman Hariri (Miaka: 35 na utajiri wa Dola 1.2 bilioni); Naruatsu Baba (Miaka 36 na utajiri wa Dola 2.2 bilioni); Yvonne Bauer & family (Miaka 36 na utajiri wa Dola 3.5 bilioni); Lawrence Ho (Miaka 37 na utajiri wa Dola 3 bilioni); Yoshikazu Tanaka (Miaka 37 na utajiri wa Dola 1.6 bilioni); Alejandro Santo Domingo Davila & family (Miaka 37 na utajiri wa Dola 11.1 bilioni); Jack Dorsey (Miaka 37 na utajiri wa Dola 2.2 bilioni); Jan Koum (Miaka 38 na utajiri wa Dola 6.8 bilioni).
Wengine ni Nicholas Woodman (Miaka 38 na utajiri wa Dola 1.3 bilioni); Chase Coleman, III (Miaka 38 na utajiri wa Dola 1.6 bilioni); Yusaku Maezawa (Miaka 38 na utajiri wa Dola 1.25 bilioni); Rahel Blocher (miaka 38 na utajiri wa Dola 2.9 bilioni); John Arnold (Miaka 39 na utajiri wa Dola 2.9 bilioni); Jon Oringer (Miaka 39 na utajiri wa Dola 1.35 bilioni); Liu Qiangdong (Miaka 39 na utajiri wa Dola 2.7 bilioni); Ryan Kavanaugh (Miaka 39 na utajiri wa Dola 1 bilioni); na Miriam Blocher (Miaka 39 na utajiri wa Dola 1.1 bilioni).
Chanzo: Forbes 

No comments:

Post a Comment