Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Sunday, 2 March 2014
POLISI ARUSHA LAWAMANI KWA UJAMBAZI
Na Mwandishi wa Brotherdanny5.blog, Arusha
JESHI la polisi mkoani Arusha limeingia lawamani likituhumiwa kumuua kwa kumpiga risasi daktari wa kitengo cha ukimwi katika hospitali ya Selian,Japhet Mtingala alimaarufu Banda(48) mkazi wa Ekenywa wilayani Arumeru kwa kumhusisha na tukio la ujambazi,ambapo watu wengine watatu waliouawa wakidaiwa kupanga njama ya kupora fedha katika kituo cha mafuta.
Aidha inadaiwa kuwa,daktari huyo aliuawa wakati akipeleka dawa ya kurefusha maisha ARV's kwa mgonjwa aliyekuwa katika bar ya Pama iliyopo katikati ya jiji baada ya kukubaliana wakutane hapo.
Tukio la kuuawa kwa watu hao lilitokea Februali ,21 mwaka huu,majira ya saa 1.30 usiku katika bar ya Pama iliyopo katikati ya jiji na kuthibitishwa na kamanda wa polisi mkoani Arusha ,Liberatus Sabas akidai ni majambazi waliokuwa wakipanga kwenda kupora.
Sabasi aliwaeleza waandishi wa habari kuwa majambazi hao walikuwa
watano huku mmoja akifanikiwa kutoroka akiwa na silaha aina ya SMG na
kufanikiwa kupata silaha moja aina ya bastola ikiwa na risasi kadhaa .
Kamanda alionyesha mfuko mmoja aliodai ulikuwa umesheheni risasi.Hata hivyo taarifa zilizoelezwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake katika kitengo hicho cha ukimwi ,waliutambua mfuko huo kwamba ndio uliokuwa ukitumiwa na marehemu kubebea dawa za ARV's alizokuwa akiwapelekea wagonjwa wasio na uwezo wa kufika hospitalini.
Kwa mujibu wa kaka wa marehemu,Joel Samweli,alisema familia imejipanga kushughulikia suala hilo,kupitia vyombo mbalimbali vya kisheria ili haki ipatikane ,kwani alisisitiza mdogo wake hakuwa na chembe ya ujambazi wa aina yoyote.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mazishi ya marehemu Banda,Samwel alilitupia lawama jeshi la polisi mkoani hapa,kwa kutokuwa makini kutambua walengwa wa uhalifu, badala yake askari wake waliamua kuwafyatulia risasi bila kuwa na maelekezo sahihi ya wahusika.
''Baada ya mazishi familia itakaa na kukubaliana chakufanya,kwani huu ni uonevu na utumiaji mbaya wa silaha,pale hapakuwa na majibizano ya risasi wala kujeruhiwa kwa askari kama alivyosema kamanda wa polisi,askari wale walikuwa na uwezekano wa kuwakamata na kubaini wahalifu na sio kuwamiminia risasi,' 'alisema Samweli.
Akitoa salamu kwa niaba ya hospitali ya Selian,dkt David Mlaki alieleza kusikitishwa na tukio hilo la kuuawa kwa muuguzi huyo na kubainisha pasipo shaka kuwa marehemu hakuwa akijihusisha na matukio ya ujambazi na kwamba wamepoteza maisha akitoa huduma ya dawa kwa mgonjwa.
''Kwa kweli tukio hili limetusikitisha sana ,hatuna la kusema tunamwachia mungu, ndio muweza wa yote,hatuna budi kushukuru kwa kila jambo,ila marehemu Banda ametuachia pengo kubwa kwani alikuwa mtu muhimu katika huduma ya ukimwi kwa muda mrefu''alisema Mlaki.
Taarifa zaidi zimethibitika kuwa marehemu Banda,aliondoka kazini(Selian) majira ya saa 11.30 jioni akiagana na mtumishi mwenzake(jina linahifadhiwa) kuwa anapeleka dawa kwa wagonjwa aliokuwa amewasiliano nao kwenye simu.
Habari zinadai kuwa kabla ya kufika eneo la tukio Banda alipitia sehemu nyingine kutoa dawa kwa mgonjwa mwingine na ulipofika muda huo ndipo alipoenda katika eneo la tukio na kukutana na mgonjwa wake ambaye alikuwa mwanamke .
Taarifa zinasema kuwa mwanamke huyo alimkaribisha marehemu katika meza moja wapo aliokuwa amekaa yeye na watu kadhaa huku mwanamke huyo akionekana kuwafahamu zaidi watu hao na kumtambulisha kwao.
Baada ya utambuzi huo dakika chache askari polisi walivamia na kuzingira meza hiyo na kuwataka wajisalimishe,ambapo ilidaiwa kuwa mmoja wa watu hao alichomoa bastola kwa lengo la kuwafyatulia askari
hao ,ndipo askari hapo walianza kuwamiminia risasi maeneo mbalimbali huku marehemu Banda akipigwa risasi kadhaa na kufumua kichwani na mdomo.
Mwili wa daktari huyo umezikwa na mamia ya wakazi wa maeneo mbalimbali katika shamba lake kijijini kwake na ameacha mke,aitwaye Agnes Japhet,na watoto wanne ,ambao ni Felister ,Scolla,Justine na Miriamu,huku mmoja wa watoto wake akisomeshwa kwa ufadhili wa mwandishi wa habari wa kampuni ya The Guardian, mkaoni Arusha, Cyinthia Mwilolezi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment