Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday, 2 March 2014

DC AONYA KUWAPELEKA WATOTO NJE YA NCHI


NA MWANDISHI WETU, ARUSHA

Watanzania wametakiwa kuondokana na dhana ya kuwapeleka watoto wao nje ya nchi kwa ajili ya kuweza kupata elimu jambo ambalo hata kwa shule za Tanzania wana uwezo huo wa kuboresha zaidi elimu.

Asilimia kubwa ya Watanzania wanadhani kuwa kumpleka mtoto au mwanafunzi nje ya  nchi ndio kumjenga jambo ambalo halina hata ukweli ndani yake.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo wakati akiongea na umoja wa wamiliki wa shule na vyuo binafsi kwa mkoa wa Arusha (TAMONGSCO) mapema jana Jumamosi.

Mongela alisema kuwa dhana hiyo imeshapitwana wakati na hivyo wananchi wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanaboresha shule zao na hivyo kuweza kutoa fursa.

Aisha alisema kuwa fedha ambazo wanazitumia nje ya nchi zingeweza kusaidia baadhi ya shule katika michango na hivyo basi wanatakiwa kuwa wazalendo.

Amedai kuwa mzalendo wa nchi ni pamoja na kuhakikisha kuwa kwanza unatoa vipaumbele kwa vitu ambavyo vipo ndani ya nchi lakini pia unaweza kuvipenda.

"Pendeni sana shule za hapa tanzania kwani zipo baadhi ambazo kwa kweli zinatoa elimu kwa wakati sana na zinafaa kuliko zile za nje ya nchi, nakama mkiziboresha basi nanyi mtapata hata wanafunzi wenyewe kutoka nje ya nchi na kwa hali hiyo mtakuwa mmenda sanjari na soko la nchi za EAC'aliongeza Mongela.

Naye Mwenyekiti wa umoja huo Ester Lema alisema kuwa pamoja na kuwa wana uwezo wa kuwasiaida wananchi kupunguza tatizo la kwenda nje ya nchi lakini bado wanakabiliwa na changamoto nyingi.

Ester alitaja changamoto ambazo wanakabiliana nazo kuwa ni pamoja na kodi kubwa ambayo wanatozwa, lakini hata riba ambayo inatolewa na asasi mbalimbali za kifedha.

No comments:

Post a Comment