Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 30 October 2015

MPIRA WA MAGONGO

KOCHA VARENTINA QUARANTA AKIWA KATIKA MOJA YA MICHEZO YA TANZANIA HUKO AFRIKA KUSINI

Kocha wa timu ya mpira wa magongo Varentina Quaranta amesema anaamini timu za Tanzania zitafanya vizuri katika michezo iliyobaki katika mashindano ya kuwania kufuzu michuano ya Olympic ya mwaka 2016 ambayo yatafanyika mjini Rio de Janeiro, nchini Brazil, licha ya kufanya vibaya katika michezo yao ya awali.

HAWA NDIO WABUNGE 264 WA BUNGE LA 11 LA JAMHURI YA MUUNGANO

Na Daniel Mbega 

Hii ndiyo orodha ya wabunge wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliotangazwa baada ya matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25, 2015. Orodha hii ni katika mpangilio wa mikoa:

Arusha
Arumeru Magharibi: Gibson Ole Mesiyeki (Chadema)
Arumeru Mashariki: Joshua Nassari (Chadema)
Karatu: Wille Qulwi Qambalo (Chadema)
Longido: Onesmo Ole Nangole (Chadema)
Monduli: Kalanga Julius Laizer (Chadema)
Ngorongoro: William Tate ole Nasha (CCM)
* Jimbo la Arusha Mjini uchaguzi umeahirishwa kufuatia kifo cha mgombea wa ACT-Wazalendo Estomih Malla.

Dar es Salaam
Ukonga: Waitara Mwita Mwikwabe (Chadema)

UCHAGUZI MKUU 2015: HUKU VILIO, KULE VICHEKO!

 
 Steven Wassira - Nje
Abbas Mtemvu - Nje
 Zitto Kabwe - Ndani
Bonna Kaluwa - Ndani


Na Daniel Mbega

UCHAGUZI mkuu umekwishapita, matokeo yametangazwa na tunashuhudia vilio na vicheko kutoka sehemu mbalimbali nchini – iwe kwenye udiwani, ubunge na hata urais.
Ingawa Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda viti vingi vya udiwani na ubunge, lakini binafsi nasema kimeshindwa vibaya kwa sababu safari hii tumeshuhudia ikipoteza halmashauri takriban 19 huku wapinzani wakizoa viti vingi vya ubunge kuliko ilivyowahi kutokea tangu kuanza kwa uchaguzi mkuu wa vyama vingi mwaka 1995.

MAMIZ GRAND RESORT INAKULETEA MIAKA 18 YA FM ACADEMIA WAZEE WA NGWASUMA NA NGOMA ZAO MPYA

MO DEWJI FOUNDATION YATANUA MBAWA, YASAIDIA UBORESHAJI WA KITUO CHA FURAHINI MKOANI K’NJARO

User comments
Baadhi ya vijana hao wakiwa darasani wakifurahia masomo wanayopatiwa ya kujiandaa na elimu ya sekondari katika kituo hicho cha Furahini mkoani Kilimanjaro.
Na Mwandishi wetu
TAASISI ya misaada ya Mo Dewji Foundation imekubali kufadhili mradi wa kituo cha mafunzo cha vijana cha Furahini (FYLC) wenye lengo la kuboresha upatikanaji wa elimu katika kijiji cha Kisangara mkoani Kilimanjaro.

MKWASA AITA 28 STARS KUIVAA ALGERIA

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Charles Boniface Mkwasa leo ametangaza kikosi cha wachezaji 28 watakoingia kambini Jumapili jioni kujiandaa na mchezo dhidi ya Algeria Novemba 14 jijini Dar es salaam, na marudiano kufanyika Novemba 17 nchini Algeria.

TWIGA KUCHEZA NA MALAWI NOVEMBA 7

Twiga Stars
Timu ya Taifa Tanzania ya Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars) inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Wanawake ya Malawi Novemba 7, 2015 jijini Dar es salaam.

KIPINDI KIPYA CHA DANGA CHEE KURINDIMA CHANNEL 10 KILA ALHAMISI SAA NNE USIKU

SIKILIZA WALICHOKISEMA STANSLAUS MABULA NA EZEKIEL WENJE BAADA YA MATOKEO NYAMAGANA

Stanslaus Shing'oma Mabula akiongea na wanahabari usiku wa kuamkia jana Octoba 27,2015 muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi wa Ubunge Jimbo la Nyamagana (CCM).

NMB MOSHI WATOA POLE KWA WAGONJWA HOSPITALI YA RUFAA YA KCMC.

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB katika matawi ya Nelson Mandela na Mawenzi wakiwasili katika hosptali ya rufaa ya KCMC.

STARS KWENDA ALGERIA NA FASTJET

Taifa Stars

Timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, inatarajiwa kusafiri na ndege ya binafsi ya kukodi ya shirika la Fastjet kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaochezwa Novemba 17 mjini Algiers.

CAF WAAMURU ZFA IONDOE MASUALA YA MPIRA MAHAKAMANI


Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) leo hii limeamuru Kamati ya muda inayoongoza Chama cha Mpira Zanzibar (ZFA) iondoe mahakamani mashatka yote dhidi ya uongozi halali wa ZFA.

TFF YAWAPONGEZA WABUNGE, MADIWANI

Rais wa TFF, Jamal Malinzi
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), limetuma salamu za pongezi kwa viongozi wa mpira wa miguu nchini waliochaguliwa kuwa wabunge na madiwani katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015.

KAMPUNI YA NDEGE YA FASTJET KUISAFIRISHA TIMU YA TAIFA STARS KWENDA ALGERIA

 Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu timu ya taifa Taifa Stars kwenda nchini, Algeria kwa mchezo utakaofanyika Novemba 17 mwaka huu.

NEC YATOA TAMKO KUHUSU UCHAGUZI WA RAIS NA WABUNGE WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji mstaafu Damian Lubuva (kulia) akitangaza matokeo ya Urais 2015 kwa baadhi ya majimbo ambayo yamekamilisha matokeo hayo katika ukumbi wa Mwalimu. J.K Nyerere jana jijini Dar es salaam. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mkuu Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid.

UN TANZANIA STATEMENT ON TANZANIA GENERAL ELECTIONS

IMG_5569
UN Resident Coordinator, Alvaro Rodriguez.
Dar es Salaam, 29 October 2015: The United Nations is following very closely the Tanzanian general elections of 25 October and congratulates the president elect. We congratulate Tanzanians for exercising their democratic rights in a peaceful manner.

Saturday 24 October 2015

UJUMBE WA BLOGGERS: TUPIGE KURA, TUPOKEE MATOKEO KWA AMANI NA UTULIVU, KUNA MAISHA BAADA YA UCHAGUZI

Bendera na ramani ya Tanzania
JUMAPILI ya Oktoba 25, 2015, Tanzania inafanya Uchaguzi Mkuu wa madiwani, wabunge pamoja na kumpata Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Uchaguzi ni nini? Zipo tafsiri mbalimbali lakini mojawapo na iliyo wazi ni kwamba, hii ni njia ya kidemokrasia inayotumiwa na watu katika kuchagua viongozi wa kuwaongoza kwa kipindi fulani kwa mujibu wa Katiba au utaratibu waliojiwekea wenyewe.

DED IGUNGA AELEZEA MAELEKEZO YA NEC


Na Hastin Liumba, Tabora

MKURUGENZI wa halmashauri ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora na msimamizi wa uchaguzijmbo la Manonga na Igunga Rustika Turuka ametoa ufafanuzi wa maekelezomapya ya uchaguzi.

ASKARI POLISI KILIMANJARO WAFANYA ZOEZI KUJIANDAA NA ZOEZI LA UCHAGUZI

Baadhi ya viongozi wa ngazi ya Juu Katika jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika maandalizi ya mazoezi.

NDESAMBURO ASEMA ALIYEKUWA MEYA WA MANISPAA YA MOSHI, JAFARY MICHAEL NDIYE ANAWEZA KUVAA VIATU VYAKE

Mbunge anayemaliza muda wake, Philemon Ndesamburo akimuombea kura mgombea Ubunge wa jimbo la Moshi mjini Jafary Michael (Chadema) katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya Manyema mjini Moshi.

SABABU 5 ZA KUMCHAGUA MAGUFULI HIZI HAPA!

Dk. John Magufuli (CCM) .
Na Daniel Mbega
ILIKUWA miezi, wiki na sasa zimesalia siku tu kabla Watanzania hawajaamua kumchagua rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Oktoba 25, 2015.

SERIKALI YAFAFANUA UKOMO WA MADARAKA YA RAIS NA MAWAZIRI

Serikali yafafanua ukomo wa madaraka ya rais na mawaziri.

Serikali yafafanua ukomo wa madaraka ya rais na mawaziri.

ikulu
Serikali imetoa ufafanuzi kuhusu ukomo wa madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwisho wa uhai wa Baraza la Mawaziri kwa kadri Tanzania inavyoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu unaofanyika Jumapili, Oktoba 25, mwaka huu, 2015.

MKE WA MTIKILA AMUOMBA KIKWETE KUUNDA TUME YA KUCHUNGUZA KIFO CHA MUMEWE

1.Mke wa marehemu Mch.Mtikila (katikati) GEOGEA MTIKILA akizungumza na wanahabri pichani hawapo.
Mke wa marehemu Mch. Mtikila, Georgia Mtikila (katikati) akizungumza na wanahabari. Hapawapo pichani.

KAJALA AMLIZA MUMEWE JELA

KajalacropHarusiKajala na mumewe siku ya ndoa.kajalaStaa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’
Baada ya kuenea kwa madai kuwa staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ amepangishiwa bonge la mjengo na kigogo mmoja (jina kapuni), mumewe Faraji Agustino anadaiwa kulizwa na vitendo vya mkewe huyo vinavyomuumiza akiwa jela.

MAGUFULI AMALIZA KAZI!

Na Richard Bukos, Pwani
MGOMBEA Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, (pichani) amemaliza kazi huku akitarajia kumwaga sera za mwisho katika Viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam kabla ya kesho kuhitimisha fainali kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

LOWASSA AJIMALIZA MWENYEWE, ASHINDWA KUJIBU MASWALI YA BBC


Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa.
Na Hamida Hassan
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa, (pichani) ameshindwa kujibu maswali aliyoulizwa na Mwandishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Zuhura Yunus, kuhusu ahadi yake ya elimu bure hadi chuo kikuu pamoja na namna atakavyopambana na ufisadi.

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI SHAURI LA MITA 200

Wakili wa upande wa mlalamikaji, Peter Kibatala (wa kwanza kulia) akiketi kusikiliza shauri hilo kutoka kwa majaji (hawapo pichani).

TIMU YA MAGONGO YA TANZANIA KUANZA KIBARUA CHA KWANZA NA ZIMBAMBWE

Timu ya taifa ya mpira wa magongo ya wanawake kesho inacheza mechi yake ya kwanza ya ufunguzi dhidi ya
zimbambwe itakayopigwa nchini Afrika kusini,katika mashindano kuwania kufuzu michuano ya Olympic ya mwaka 2016 ambayo itafanyika mjini Rio de Janeiro, nchini Brazil.

MAGUFULI AFUNGA KAMPENI ZAKE DAR KWA KISHINDO, AELEKEA MWANZA

magufuli akimwaga sera jangwani leo (2)
Dk. Magufuli akimwaga sera kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kwenye Viwanja vya Jangwani jana Ijumaa.
JK akimnadi Magufuli (1)JK akimnadi Magufuli (2)
Mwenyekiti wa CCM, Dk. Jakaya Kikwete akimnadi mgombea urais wa CCM, Dk. Magufuli jana Ijumaa.
JK na Magufuli wakikumbatiana
Dk. Jakaya Kikwete na Dk. Magufuli wakikumbatiana wakati wa mkutano wa leo.
Mama salma Kikwete kushoto na Mama Janeth Magufuli wakibadilisha mawazo wakat mkutano ukiendelea
Mama Salma Kikwete (kushoto) na Mama Janeth Magufuli wakibadilisha mawazo wakati mkutano ukiendelea.
JK akimnadi Jerry Slaa wa jimbo la Ukonga
JK akimnadi Jerry Silaa ambaye ni Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ukonga kwa tiketi ya CCM.
JK akimnadi Mgombea ubunge wa Kibamba dkt Fenella Mkandalla
JK akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kibamba (CCM), Dk. Fenella Mkangara.
MGOMBEA Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli jana Ijumaa alimaliza kampeni zake jijini Dar es Salaam kwa kumwaga sera zake katika Viwanja vya Jangwani kabla ya kesho kuhitimisha kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Baada ya kufunga kampeni zake, leo hii Dk. Magufuli ataelekea kijijini kwake huko Chato mkoani Geita kwa ajili ya kupiga kura yake keshokutwa.
(PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL, JANGWANI)

MTOTO HATUMWI DUKANI LEO . NI KATIKA UFUNGAJI WA KAMPENI ZA CCM JIJINI MWANZA.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Pichani) amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya shughuli ya kufunga kampeni za Uchaguzi Mkuu kitaifa kwa upande wa Chama hicho inayotarajiwa kufanyika hii leo katika Uwanja wa CCM Kirumba yamekamilika.

TUJIEPUSHE NA KURA ZA LIWALO-NA-LIWE!

Ikulu ya Tanzania

Na Mkimbu Lukule
Tangu kuanza harakati za uchaguzi Tanzania kumekuwa na tambo nyingi za kuwanadi wagombea.  Kila kundi likitaka mgombea wao ang’ae dhidi ya mwenzake.  Zimekuwepo mbinu na hadaa nyingi katika kufanikisha malengo haya ya kisiasa.
Wapo ambao wamekuwa wakifanya kampeni zao kwa kutoa ahadi lukuki ambazo zinalenga katika kuwaaminisha wananchi kuwa wakichaguliwa wataibadilisha nchi kwa haraka na kuifanya ifike katika kilele cha maendeleo.

Friday 23 October 2015

SERIKALI YASAINI NA KAMPUNI YA ASHOK LEYLAND MKATABA WA UNUNUZI WA MAGARI KWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA, JIJINI DAR

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima (kulia), Makamu wa Rais wa Kampuni ya Kutengeneza Magari ya ASHOK LEYLAND ya nchini India, Bhimasena Rau wakisaini Mkataba wa ununuzi wa magari kwa ajili ya matumizi ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambavyo ni Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, jijini Dar es Salaam.  

JESHI LA POLISI MBEYA LAPIGA MARUFUKU KWENDA KUPIGA KURA UKIWA UMEVAA SARE ZA VYAMA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi.

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya limetoa rai kwa wafuasi wa vyama vishiriki katika uchaguzi mkuu Octoba 25 mwaka huu kujiepusha kufika katika kituo cha kupigia kura wakiwa wamevaa nguo zenye picha za wagombea, maneno au nembo ama rangi za chama cha siasa.

MKURUGENZI WA MAKAMPUNI YA APEX GROUP AOMBA WANANCHI KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU KATIKA UCHAGUZI MKUU


Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Apex Group na Mwanaharakati,  Joseph Mhonda (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu amani na utulivu kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika kesho nchini kote. Kulia ni Ofisa Habari wa Makampuni hayo, Pipino Sudi.

NMB MOSHI WATOA KIFUNGUA KINYWA KWA WATEJA WAO.

Baadhi ya wateja wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela ,Moshi mjini wakipata kifungua kinywa katika tawi la Benki hiyo leo asubuhi.

UNESCO YAHAMASISHA UJUMBE WA AMANI #UCHAGUZIMKUU2015

Peace Message 2 (1)

Dk Shein Afunga Mkutano wake wa Kampeni Kisiwani Pemba

Vijana Kisiwanin Pemba wakiingia katika viwanja vya Gombani kuhudhuria Mkutano wa Ufungaji wa Kampeni ya CCM ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein.

JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA LATOA MSIMAMO WAKE JUU YA SUALA LA MITA 200 BAADA YA KUPIGA KURA.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi Charles Mkumbo akiongea na Waandishi wa Habari Ofisini kwake jana ambapo alitoa msimamo wa jeshi hilo juu ya suala la wananchi kubaki mita 200 kutoka vilipo vituo vya kupigia kura baada ya kupiga kura siku ya jumapili Octoba 25,2015 ikiwa ni siku ambayo Watanzania watashiriki katika zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Kuwachagua Wawakilishi wao kuanzia ngazi ya Madiwani, Wabunge na Rais.

NICHAGUENI KESHO KUTWA KWA KURA NYINGI NIWALETEE MAENDELEO JIMBO LA MBAGALA

Soud Rajab.
Na Dotto Mwaibale

MGOMBEA ubunge Jimbo la Mbagala kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Soud Rajab (pichani kushoto), amewaomba wananchi wa Jimbo la Mbagala wamchague ili aweze kuwaletea maendeleo waliyoyakosa kwa muda mrefu.

Rajab alitoa maombi hayo kwa wananchi hao Dar es Salaam jana wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wake wa kampeni wa lala salama kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika nchi nzima keshokutwa.