Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 6 December 2014

CHAMA CHA SERIKALI ZA MITAA KUGOMEA UCHAGUZI MKUU 2015 MPAKA KILIPWE BILIONI 17/=

Waziri Mkuu Mizengo Pinda

Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (Talgwu), kimetishia kutoshiriki Uchaguzi Mkuu wa 2015, kama haitalipwa deni lake na serikali la Sh. bilioni 17 ifikapo Desemba 31, mwaka huu.


Hatua hiyo imekuja baada ya serikali kushindwa kulipa deni la malimbikizo ya mishahara, likizo, matibabu na masomo ambapo ilitakiwa kukilipa Talgwu zaidi ya Sh. bilioni 24.

Katika mchanganuo wa deni hilo Talgwu kimesema hakijalipwa zaidi ya Shilingi bilioni tano za uhamisho, Shilingi bilioni sita, matibabu na likizo, zaidi ya Shilingi bilioni tano, masomo na posho na Shilingi bilioni nne kwa ajili ya matumizi mengine.

Naibu Katibu Mkuu wa Talgwu Taifa, Njaa Kibwana, alisema chama kimechukua maamuzi magumu kutokana na serikali kukidhiaki.

Aidha, kimesema endapo serikali itapuuza maamuzi hayo haraka iwezekanavyo, kitawashawishi na kuwaelekeza wanachama wake nchi nzima wenye idadi zaidi ya 61,000 kutoshiriki uchaguzi mkuu wa 2015.

Alifafanua mlolongo wa deni hilo ni kutoka mwaka 2007 hadi 2009, ambalo serikali kupitia Waziri Mkuu Mizengo Pinda, iliahidi kulilipa ndani ya miezi mitatu.

Alisema deni hilo sio kitu kigeni kwa serikali kwani uongozi wa chama umeshakutana na kufanya mazungumzo ndani ya mwaka mmoja na miezi saba, bila hatua zozote kufanyika.

Alisema kwa sasa serikali imefika hatua mbaya kwa kugeuza deni kama sehemu ya siasa kutoa ahadi zisizotekelezeka kwa kukataa kulipa watumishi wa serikali za mtaa wakati inajua wazi wakigoma athari  zake ni kubwa zaidi kutokana na huduma zote za kijamii zitasimama.

Mwenyekiti Wanawake Taifa Talgwu, Dk. Angelina Samike, alisema serikali kupitia deni hilo limekitia chama dosari hasa uongozi kutokana na wanachama wake kutokuwa na imani kama suala hilo linashughulikiwa.

Kadhalika, Talgwu kilikaa na viongozi wa juu wa serikali akiwamo Pinda, kupitia Kamati ya Utendaji Taifa (KUT), Oktoba mwaka huu na maazimio yao yalitakiwa deni hilo liwe limeshalipwa lakini hawaoni juhudi zozote zilizochukuliwa.

Alisema kauli za kukinzana baina yao na serikali zimewasababishia wanachama kuvunjika moya kiutendaji na kujipanga kugoma kufanya kazi hivyo jitihada za haraka zinatakiwa kunusuru hali hiyo.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment