Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Wednesday, 5 March 2014
WAFANYABIASHRA WENGI HAWANA UELEWA WA MASOKO YA HISA
Na Mwandishi wa Brotherdanny5.blog, Arusha
IMEELEZWA kuwa asilimia kubwa ya wafanyabiashara wadogo wanashindwa kujiunga na masoko mbalimbali ya hisa hapa nchini kwa kuwa hawana uelewa wa masoko hayo.
Pia bado wafanyabiashara ambao ni wajasiriamali wanakabiliwa na uelewa mdogo juu ya masoko hayo ya hisa jambo ambalo ni kikwazo kwa maendeleo ya Uchumi wa Nchi.
Hayo yameelezwa na John Mongela ambaye ni mkuu wa wilaya ya Arusha kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo wakati akifungua mkutano baina ya wajasiriamali wa mkoa wa Arusha pamoja na wadau wa soko la hisa la Dar es Saalam (DSE).
Mongela alisema kuwa uwepo wa masoko ya hisa hapa nchini ni mzuri sana lakini bado baadhi ya wajasirimali hawana uelewa wa kutosha na hivyo ni jukumu kwa wadau wenyewe kuhakikisha kuwa wanawasaidia wafanyabaishara hao wakubwa kwa wadogo waweze kufikia malengo yao ya uhakika.
Mbali na hayo Mongela alisema kuwa pia masoko hayo ya hisa yanatakiwa kuwapatia wajasiariamli njia mbambali ambazo zitaweza kuwasaidia kukuza na kuimarisha uchumi wa nchi ya Tanzania.
"Kama tukiwawekea utaratibu mzuri hawa wajasiriamali lakini pia wafanyabiashara wadogo basi mitaji itaongezeka na wataweza kujiendesha wao wenyewe na hivyo uchumi wa nchi nao utaweza kuimarika kwani uwezo huo upo kabisa," aliongeza Mongela.
Naye Mwanasheria wa soko hilo la hisa la Dar es saalam. Mary Muniwasa alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa wafanyabishara wadogo na wa daraja la kati wameanzisha rasmi dirisha la kukuza ujasiriamali kwa malengo ya kuboresha uchumi wa nchi.
Mary alifafanua kuwa mpango huo tayari umeshaanza na utaweza kuwanufaisha wajasiriamali wote lakini pia utaweza kuboresha hata mitaji ya biashara zao kwani uzoefu unaonesha kuwa asilimia kubwa ya wajasiriamali wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mitaji.
Aliwataka wafanya biashara wote hapa nchini kuhakikisha kuwa wanatumia vema dirisha hilo la kukuza ujasiriamali kwa maslahi ya kuboresha uchumi na maendeleo ya Nchi ya Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment