ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENCY(ACT TANZANIA)
MABADILIKO NA UWAZI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Jumatatu, 03 Machi 2014, Dar es Salaam
1. Utangulizi
Ndugu wana habari,
Naomba
nichukue fursa hii kuwashukuru kwa kuitikia wito wa kuhudhuria mkutano
wetu, ambao ni wa kwanza tangu chama chetu kianzishwe. Tunatambua na
kuheshimu kazi yenu kama mhimili wa nne wa dola, na leo tunaomba
kuzungumza na watanzania kupitia kwenu.
Lengo
kuu la mkutano huu ni kukitambulisha kwenu chama kipya cha siasa
kinachoitwa Alliance for Change Tanzania (ACT Tanzania) na kuwaombeni
kukitambulisha chama hiki kwa watanzania kupitia vyombo vyenu vya
habari.
2. ACT Tanzania ni nini?
Ndugu Wanahabari,
ACT
� Tanzania ni kifupi cha maneno: Alliance for Change and Transparency,
yaaani Umoja wa Mabadiliko na Uwazi. Ni chama kipya cha siasa
kilichoanzishwa kwa lengo mahsusi la kuwaleta pamoja watanzania
wanaoamini kwamba nguvu ya pamoja inahitajika katika kuleta mabadiliko
ya kweli katika nchi hii, na kwamba uwazi na uadilifu ni tunu ambazo
taifa hili linazihitaji sana kwa sasa na baadaye.
3. Itikadi na Misingi ya ACT Tanzania
ACT
Tanzania ni chama kinachoaamini katika demokrasia jamii na chenye
shabaha kuu ya kupigania na kusimamia mabadiliko na uwazi nchini
Tanzania. ACT-Tanzania inaamini kuwa mabadiliko yoyote katika jamii
lazima yainufaishe jamii husika, na kwamba wananchi wenyewe ni lazima
washiriki katika kuleta mabadiliko hayo kwa uwazi na uzalendo. Mwongozo
wa sera za ACT-Tanzania ni maendeleo shirikishi na kuhakikisha uwepo wa
uongozi adili katika ngazi zote.
ACT Tanzania inaongozwa na misingi mikuu mitano ifuatayo:
i) Uzalendo
ACT-Tanzania
inaamini kwamba kila mwananchi ana wajibu wa msingi kabisa wa kutoa
mchango wake katika jamii na Taifa kwa ajili ya kuhifadhi ustawi wa nchi
kwa ajili ya kizazi cha leo na cha baadaye. Ili wananchi waweze kutoa
mchango huu kwa dhati na kwa moyo, ni muhimu mazingira yawepo ya
kuhakikisha kwamba wananchi wanaipenda nchi yao. Kwa msingi huu,
ACT-Tanzania itajenga mazingira mwafaka ya wananchi kuipenda nchi yao
ili wajitoe kikamilifu katika kuijenga na kuilinda. ACT-Tanzania
itajenga mazingira yatakayoongeza uzalendo wa wananchi kwa kuhakikisha
uwepo wa uwazi, ulinzi na utumiaji bora wa rasilimali za taifa na
uadilifu wa viongozi.
ii) Usawa
ACT-Tanzania
inaamini katika usawa katika yyanja zote. Tunaamini kwamba mafanikio ya
mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla yatatokana na bidii katika kazi.
Kwahiyo, ACT Tanzania kitapigania kuwepo usawa wa fursa na mazingira
mazuri kwa wote katika kuhakikisha kwamba kila mtu na kila kundi katika
jamii linakuwa na fursa sawa ya kufanya kazi za kujiajiri au kuajiriwa,
na kwamba kipato kitokanacho na kazi halali ndicho kitakuwa kipimo cha
mchango wake katika jamii na taifa.
iii) Uadilifu
Uadilifu
katika maisha binafsi na katika jamii utakuwa ndio msingi na mwongozo
mkuu wa viongozi na wanachama wa ACT-Tanzania. ACT-Tanzania inaamini
kwamba uadilifu ndio msingi na nguzo kuu ya mapambano dhidi ya rushwa na
maovu mengine katika jamii.
iv) Uwazi na uwajibikaji
ACT
Tanzania inaamini katika uwazi kwenye mambo yote ya kijamii na kitaifa.
Hivyo basi viongozi na wanachama wa ACT-Tanzania wana wajibu wa
kupigania uwazi katika mambo yote wanayofanya kwa ajili ya umma.
Sambamba na uwazi, ACT- Tanzania inaamini kwamba kila mwananchi na
kiongozi mwenye dhamana katika umma ana wajibu katika jamii na Taifa kwa
ujumla na ni jukumu lake kutekeleza wajibu huo bila kinyongo. Aidha,
mwanachama na kiongozi atokanaye na ACT Tanzania anapaswa kuwajibika kwa
maneno na matendo yake katika utumishi au nje ya utumishi wa chama au
taasisi yeyote ya umma. ACT Tanzania inaamini kwamba bidii katika kazi
ndiyo njia pekee ya kujipatia maendeleo.. Hivyo basi wajibu mkuu wa
mwanachama wa ACT Tanzania utakuwa ni: BIDII KATIKA KAZI.
v) Demokrasia ya Kweli
ACT-Tanzania
inaamini demokrasia ndiyo msingi wa kujenga fikra pevu na kueneza uhuru
wa mtu, jamii na Taifa kwa ujumla. Hivyo basi, viongozi na wanachama wa
ACT-Tanzania watapigania uwepo wa demokrasia ya kweli katika kila
ngazi, ndani na nje ya chama. Kila jambo lenye maslahi mapana katika
chama na katika umma litaamuliwa kwa njia ya kidemokrasia ya moja kwa
moja au kupitia kwa wawakilishi waliochaguliwa.
4. Taarifa ya Kazi na mipango ya mbele
� ACT Tanzania imekwisha kukamilisha rasimu ya awali ya Katiba ambaye iliwezesha kupata usajili wa muda
�
Zoezi la kuandikisha wanachama katika mikoa kwa ajili ya kuomba usajili
wa kudumu kwa mujibu wa sheria limekwishakamilika. Tumewapata wanachama
katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar. Hata hivyo, tumechagua
mikoa kumi ambayo tungependa msajili akahakiki kama sheria inavyotaka.
�
Baada ya kukamilisha zoezi la kuandikisha wanachama, wiki hii kabla ya
Ijumaa tutapeleka fomu na mahitaji mengine husika kwa Msajili wa vyama
ili aweze kupanga ratiba ya zoezi la uhakiki.
� Mara baada ya msajili kutoa usajili wa kudumu kwa muda atakaopanga, tutafanya uchaguzi wa kwanza mkuu
�
Kama itampendeza msajili akatupatia usajili wa kudumu mapema,
tunatarajia kushiriki kwa nguvu zote katika chaguzi zote ndogo
zitakazojitokeza, uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu
mwakani.
5. Shukrani
� Napenda
kuchukua nafasi hii kuwashukuru waratibu wote wa zoezi zima la
uandikishaji wanachama waliojitolea kwenye mikoa na wilaya mbalimbali
katika kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa kwa wakati uliopangwa.
�
Natoa wito kwa wanachama na wapenzi wa chama popote walipo waendelee
kukichangia chama kwa nguvu zao, muda wao, taaluma zao na kwa kila hali
kadri uwezo unavyomruhsu kila moja wetu.
�
Nawashukuru sana wataalam na watafiti wetu mbalimbali ambao wamekuwa
wakijitolea kutumia utaalam wao kutushauri katika maeneo mbalimbali ya
utafiti, uongozi, sera, raslimali, usimamizi wa fedha, mawasiliano,
sheria, sayansi ya siasa, na kadhalika.
6. Wito kwa wanachama na watanzania
Tunatoa wito kwa kila mwanachama, mfuasi na mpenzi wa ACT-Tanzania popote walipo nchini kuhakikisha kwamba:
�
wanazingatia misingi ya chama iliyoanishwa hapo juu katika shughuli zao
zote. Wakukumbuke kila mara kwamba lengo kuu la chama hiki ni kupigania
na kusimamia mabadiliko na uwazi katika kila ngazi. Tungependa kila
shughuli ya chama iwe shirikishi na wazi kwa wanachama na wananchi kwa
ujumla.
� anafanya kazi kwa bidii katika kukijenga chama na kushiriki maendeleo katika jamii aliyomo,
akizingatia
kwamba chama hiki kinaamini kwamba bidii katika kazi ndiyo njia pekee
ya kujipatia maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla. Hivyo,
kila mwanachama ahakikishe anatoa mchango wake katika kukijenga chama na
kuleta maendeleo katika jamii husika aliyomo.
�
Tunawakaribisha watanzania wote popote walipo na wanaoamini katika
misingi tuliyoainisha hapo juu kujiunga na ACT Tanzania. Kila mtanzania
anayejiunga na chama hiki akumbuke kuchukua wajibu wake katika kukijenga
chama popote pale alipo. Na akumbuke wajibu mkuu kwa mujibu wa chama
hiki kuwa ni: BIDII KATIKA KAZI.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki ACT-Tanzania, ahsanteni kwa kunisikiliza!
Kadawi Lucas Limbu,
Mwenyekiti wa Taifa
ACT Tanzania.
No comments:
Post a Comment