Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 4 March 2014

OKWI, KIIZA WAIFUATA CRANES ZAMBIA

Hamis Kiiza

Shirikisho la Soka la Uganda (Fufa) limetibua maandalizi ya Kikosi cha Yanga kinachojiwinda na mechi ya  marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly baada ya washambuliaji Emmanuel Okwi na Hamis Kiiza kujiunga na timu yao ya Taifa (The Cranes).

Okwi na Kiiza, waliondoka nchini jana asubuhi kwenda kujiunga na Kikosi cha timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) kinachojiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Zambia (Chipolopolo) utakaopigwa kesho.

Kuondoka kwa wachezaji hao kunamaanisha kwamba maombi ya Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, kwa uongozi wa Fufa hayakuwa na mafanikio, baada ya awali rais huyo kuahidi kuzungumza na bosi mwenzake ili wasiwajumuishe washambuliaji hao.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana, zinaeleza kwamba wachezaji hao watajiunga na Kikosi cha Yanga, keshokutwa jijini Cairo, Misri.

Kikosi cha Yanga kinatarajia kuondoka nchini kesho usiku kuelekea Cairo kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa dhidi ya Al Ahly unaotarajiwa kupigwa Jumapili Machi 9, mwaka huu.

"Timu itaondoka nchini Jumatano usiku, lakini Okwi na Kiiza tutakutana nao huko huko (Cairo) siku ya Alhamisi," kilisema chanzo chetu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Kimataifa, Seif Ahmed 'Magari', alisema maandalizi ya timu yao yanaendelea vyema na wanaamini kila mchezaji anajua jukumu walilonalo katika mchezo wa marudiano.

Kiongozi huyo alisema klabu yao imejipanga kuhakikisha mwaka huu wanaweka rekodi mpya kwenye michuano hiyo inayoandaliwa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) kila mwaka, kwa kuwaondoa Waarabu na kusonga mbele.

Wawakilishi hao pekee wa nchi waliosalia katika mashindano ya kimataifa, wameingia kambini jana jioni kwenye Hoteli ya Bahari Beach na wanafanyia mazoezi Uwanja wa Boko Veterani.

Yanga ilipata ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Al Ahly uliofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini, bao ambalo lilizamishwa kimyani na nahodha wao, Nadir Haroub 'Cannavaro'.

Kutokana na maandalizi ya mchezo huo, TFF iliamua kuwaondoa wachezaji wa Yanga waliokuwa wameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) ambayo itashuka dimbani jijini Windhoek, Namibia kesho dhidi ya wenyeji wao (Brave Warriors).

Makamu Rais wa Fufa, Mujib Kasule, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ufundi ya shirikisho hilo, alisema jana beki wao anayekipiga Marekani, Henry Kalungi na kiungo Tony Mawejje wataikosa mechi hiyo lakini Kiiza na Okwi wataongoza safu ya ushambuliaji.

“Kalungi aliomba visa Afrika Kusini na hawezi kusafiri kwa sababu hajapata hati yake na Mawejje, ambaye alijiunga na Haugesund FC ya Norway hivi karibuni, yuko 'bize' sana na timu yake mpya," alisema Kasule.

Alisema wachezaji wa ndani ya Uganda walisafiri usiku wa kuamkia jana kwenda Ndola, wakati mapro walitarajiwa kujiunga na timu nchini Zambia jana.
CHANZO: NIPASHE     

No comments:

Post a Comment