Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tabora Mjini, Moshi Nkomkota (60), ameshambuliwa kwa kukatwa mapanga katika masuala yanayohusishwa na siasa.
Akiongea na waandishi wa habari katika Hospitali ya Mkoa wa Tabora, Kitete, Nkonkota alisema kuwa majira ya saa 1.30 usiku juzi, maeneo ya Mihogoni wakati akienda msikitini kusali sala ya Isha, alikutana na watu watano ambao walitega kamba ili aanguke.
Alisema walipoona hajaanguka walimvamia akiwa kwenye pikipiki yake na kuanza kumshambulia kwa mapanga na marungu na kumjeruhi vibaya kichwani.
Alisema aliokolewa na wasamaria wema baada ya kusikia purukushani hizo na watu hao walitokomea mbugani.
Muuguzi katika hospitali hiyo,Yohana Yindi, alisema kuwa mwenyekiti huyo alifikishwa majira ya saa 2.30 usiku akiwa ametapakaa damu kutokana na majeraha ya kichwani na mikononi.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Juma Bwire, alikiri kutokea kwa tukio hilo.
Alisema shambulio hilo linatokana na masuala ya kisiasa na kwamba jeshi hilo linafanya uchuguzi ili kuwabaini watu waliofanya unyama huo.

SOURCE: NIPASHE JUMAPILI
No comments:
Post a Comment