Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 4 April 2015

WATOTO 95,588 WAFANYIWA UCHUNGUZI WA AFYA


Na Hastin Liumba, TaboraJUMLA ya watoto 95,588 wenye umri chini ya miaka 15 mkoani Tabora wamefanyiwa uchunguzi wa afya ikiwemo maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) katika kipindi cha mwaka 2003 hadi Desemba 2014.



Kati  watoto hao wasichana wakiwa 48,678 na wavulana 47,910.

Meneja wa Shirika lisilo la kiserikali la Elizabeth Graser Pediatric Aids Foundation (EGPAF) mkoani Tabora Dr Alphaxard Lwitakubi alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na Mratibu wa Mawasiliano wa shirika hilo Mercy Nyanda.

Alieleza EGPAF chini ya ufadhili wa mashirika ya CDC na USAID nchini Marekani imekuwa mstari wa mbele kuwezesha zoezi la upimaji wa VVU kwa hiari kwa watu wote ikiwemo kuhamasisha akina mama wajawazito kuhudhuria kliniki mapema ili kutambua afya zao.

Alisema kwa kipindi chote hicho cha miaka 11hadi kufika mwezi desemba mwaka jana jumla ya watoto wadogo 95,588 walifanyiwa uchunguzi wa afya zao ikiwemo kupimwa maambukizi ya VVU mara tu baada ya mama zao kujifungua.

Aliongeza tangu EGPAF ianze kazi mkoani hapa imetoa msukumo mkubwa wa kuhakikisha akina mama wajawazito wote wanahamasishwa kuhudhuria kliniki ya uzazi mapema na kufanyiwa uchunguzi wa afya zao ikiwemo kupimwa maambukizi ya VVU.

Akieleza mafanikio ya jitihada mbalimbali zilizofanywa na shirika hilo Dr Lwitakubi alieleza EGPAF kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na serikali ya Mkoa wa Tabora wamefanikisha uchunguzi wa afya za watoto wachanga 10,442 kupitia mpango wa EID (Early Infant Diagnosis).

Aliongeza katika watoto waliochunguzwa 3,458 walibainika na maambukizi ya VVU na 9,109 hawakuwa na maambukizi na katika hao 531 waliingizwa katika mpango wa ART katika kipindi cha kuishia desemba 2014.

Aidha alibainisha ni muhimu sana kujua afya za watoto punde tu wanapozaliwa ili nao waanzishiwe huduma ya matibabu na matunzo kwani ni rahisi kwa watoto hao kushambuliwa na magonjwa nyemelezi kuliko watu wazima.

Lwitakubi alisisitiza ni muhimu sana watoto wachanga waletwe kliniki ili kupimwa mapema kwani  50 ya watoto wanaozaliwa na maambukizi ya VVU wasipopata matibabu mapema wengi wao hufariki kabla ya kutimiza miaka 2 na wengine hufariki katika umri wa miaka 5.

No comments:

Post a Comment