Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Thursday, 16 April 2015
MCHUNGAJI AELEZA KIINI CHA KUPOROMOKA MAADILI
Na Hastin Liumba, TaboraBAADHI ya viongozi waliopewa dhamana ya kuongoza watu katika utumishi wa umma au taasisi binafsi yameendelea kuporomoka siku hadi siku kutokana na kuharibika kwa mifumo ya kusikia, kutenda na mienendo na kukosa hofu ya Mungu.
Hayo yamebainishwa na Mchungaji Martin Philip wa kanisa la TAG mkoani Tabora alipokuwa akizungumza na mwandishi wa gazeti hili mara baada ya kumalizika kwa ibada iliyofanyika katika la TAG Kitete.
Mchungaji Philip alieleza kuendelea kuporomoka kwa maadili ya waumini, viongozi wa serikali na wale walioko katika utumishi wa umma na jamii kwa ujumla hapa nchini na duniani kote kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa hofu ya Mungu mioyoni mwa watu jambo ambalo limesababisha kuharibika kwa mifumo ya kusikia.
Alisema Mungu alipomwumba Adamu alimwekea mifumo mitatu ya kiutendaji ambayo ni mfumo wa kusikia anapoambiwa jambo, mfumo wa kutenda au kutendea kazi kile anachoambiwa na mfumo wa maadili au mwenendo mzuri, lakini baada ya Adamu kumkosea Mungu, mifumo hiyo yote iliharibiwa na shetani.
Alieleza baada ya Adamu kupotoka hofu ya Mungu ndani yake iliondoka hata hakuwa msikivu tena wala kutenda lile zuri kama alivyoelekezwa badala yake mwenendo wake wote ulibadilika, na hivi ndivyo ilivyo hivi leo, shetani ameharibu mifumo ya watu wengi ndio maana sio wasikivu tena, wanatenda yasiyompendeza Mungu na jamii kwa ujumla.
"Ndugu zangu tunayo nafasi ya kuponya mifumo yetu ya usikivu, utendaji na maadili yetu, Mungu yuko tayari kutusamehe tukikubali," alisema Mchungaji.
Aidha alibainisha kutokana na ukukosekana kwa hofu ya Mungu wanadamu wengi sasa wamebadilika sana mkubwa kwa mdogo awe mwanakwaya au muumini wa kawaida, awe kiongozi au mtendaji serikalini, mfumo wa utendaji na maadili yao sio yale yaliyokusudiwa, hata wakiambiwa hawasikii, damu ya Yesu ipo kwa ajili ya kututakasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment