Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 9 January 2015

COASTAL UNIONI KUKIPIGA NA MOMBASA COMBAIN KESHO


NA MWANDISHI WETU,TANGATIMU ya Coastal Union “Wagosi wa Kaya” kesho wanatarajia kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Mombasa Combain ikiwa ni kukipa makali kikosi hicho kabla ya kucheza mechi zake zinazofuata za Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.


Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani kuanzia saa kumi jioni ikiwemo wadau mbalimbali wa soka kutakiwa kujitokeza ili kuweza kushuhudia mchezo huo.

Ofisa Habari wa Coastal Union, Oscar Assenga amesema kuwa mechi hiyo ni sehemu ya kuhakikisha kikosi hicho kinajiimarisha zaidi kila idara kabla ya mchezo wake na Polisi Morogoro.

Assenga amesema kuwa maandalizi ya kuelekea mchezo huo yamekamilika kwa asilimia kubwa na Mombasa Combain wanatarajiwa kutua leo jijini hapa tayari kwa ajili ya mechi hiyo itayochezwa kesho kuanzia saa kumi jioni.

Hata hivyo aliwataka wapenzi wanachama na mashabiki wa soka kuhakikisha hawakosi fursa hii adimu kuja kuishuhudia timu yao ikicheza kwenye uwanja wake wa nyumbani kabla ya kuanza mechi za Ligi kuu zinazofuata.

Wakati huo huo,Kikosi cha timu ya Coastal Union kinaendelea na mazoezi kila siku kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly na sasa kipo tayari kuweza kuikabili timu yoyote ile itakayokutana nayo na kuweza kupata matokeo mazuri.

No comments:

Post a Comment