Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 13 January 2015

WAZEE WALIA NA HALI NGUMU YA MAISHA, WAOMBA SERIKALI NA WAHISANI KUWANUSURU

Na Mwandishi Wetu, Arumeru

WAZEE  Wilaya ya Meru wameomba ,Serikali na wahisani  kuwasaidia kukabiliana na hali ngumu ya maisha inayokabili ikiwa inachangiwa na mabadiliko ya tabia nchi ,ambapo wamelazimika  kuacha shughuli za kilimo walizokuwa wanazitegemea.

Wazee hao wakizungumza katika kijiji cha Sakila ,Kilombero wamedai kuwa  maisha yao kwa sasa yanategemea msaada kutoka kwa wasamaria wema  ambapo   wamedai kuwa Taasisi ya Sakila Hope for Elderly imekuwa ni mkombozi wao kwa zaidi ya miaka 5 kupitia wadau wengine wa maendeleo .
Bibi Sara Noel alisema kuwa anapata nguvu na kuona maisha yanaendelea kutokana na huduma wanayopata kutoka kwa wasamaria kupitia Shirika la Sakila Hope for Elderly.
“Sisi tunashukuru angalau tunapata msaada lakini sote tunajua kuwa kuna kundi kubwa la wazee wanaoteseka  wakikabiliwa na hali ya kukataliwa na jamii zao ,ni muhimu sasa ukawepo  mpango wa  kitaifa wa kuwasaidia wazee”alisema Bi Noel
Mratibu wa Taasisi ya Sakila  Hope  for Elderly  Humphrey Mafie  alisema kuwa wazee wengi katika  siku hizi wanateseka na hata jamii zao zinawatenga na kuwaona ni mzigo.
 Akigawa misaada ya vyakula ,nguo na mahitaji mengine kwa wazee 246 wanaolelelewa na taasisi hiyo katika eneo la Meru  ,Mafie alisema kuwa  idadi kubwa ya wazee wenye umri mkubwa wametelekezwa na familia zao na kugeuka kuwa omba omba katika jamii .
Aidha aliongeza kuwa wazee wengi ambao hutegemea kilimo wameathiriwa zaidi na mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi kufuatia kukosekana kwa mvua.
 Alisema mazingira hayo yamewafanya wazee waishio vijijini kuwa na hali mbaya zaidi kwani wengi wameachwa na vijana ambao wamekwenda katika maeneo mengine kutafuta fursa za kiuchumi. 
“Umefika wakati wa jamii  kuanza mjadala kuhusu namna ya kuwatunza wazee ,hawa wazee ni hazina  ,wengi wamelitumikia taifa na jamii zao hivyo ni muhimu familia kuwajali na kuwatunza” alisema Mafie.
Wakizungumzia misaada hiyo kwa niaba ya Wazee wenzake   Ndetaniso Ndewario alishukuru Shirika la kuhudumia wazee pamoja na kampuni ya Sigara kwa kuwakumbuka na kuwasaidia.
“Tunashukuru tumepata nguo vyakula  na hata msaada wa kila mwezi wa chakula na mahitaji mengine tunayopata ikiwemo ya huduma za kiafya” alisema Ndewario.
Naye afisa mahusiano wa kampuni ya Sigara Tanzania ambao ndio wametoa msaada  huo wenye thamani ya shilingi milioni  10  Martha Saivoye alisema kuwa kampuni hiyo imetoa msaada kwa wazee hao kama moja ya majukumu yao ya kusaidia kijamii.
Kwa upande wake mlezi wa taasisi hiyo ya kuwatunza wazee wasiojiweza ,Mchungaji Amos Baruti alisema kuwa taasisi hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa ya kumudu kusaidia wazee wengi wasiojiweza.
“Hili kundi la wazee wasiojiweza linaongezeka kila kukicha,hatuna rasilimali za kuweza kuwasaidia  hivyo ni muhimu serikali na wadau mbalimbali wakatuunga mkono “alisema  Mchungaji Baruti.
Alieleza kuwa wamejenga kambi maalum ya kuwatunza wazee ambayo itakuwa na uwezo wa kuwatunza wazee 24 itakapokamilika.
“Kambini tayari tuna wazee sita ,lakini ujenzi wa makazi hayo utakapokamilika tutaweza kuwahudumia wazee 24 tu na idadi nyingine itategemea misaada itakayopatikana kupanua mradi”alisema Mchungaji Baruti.

No comments:

Post a Comment