Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 16 January 2015

OLE WENU MSIOPENDA MAZOEZI


Je ulijua kama watu wengi barani Ulaya wanakufa kwa kukosa kufanya mazoezi ikilinganishwa na idadi ya watu wanaokufa kutokana na ugonjwa wa kisukari?

Kwamba ukosefu wa mazoezi unaua mara mbili ikilinagishwa na ugonja wa kisukari? Basi ikiwa ulikuwa huna habari , habari ndio hiyo.
Watafiti waligundua hili kutokana na utafiti wao walioufanya kwa mwaka mmoja kuwachunguza watu 300,000.
Watafiti kutoka chuo kikuu cha Cambridge walisema kwamba vifo 676,000 vinavyoripotiwa kila mwaka vinatokana na watu kukosa mazoezi ikilinganishwa na vifo 337,000 vinavyotokana na uzito au unene wa kupindukia.
Walisema kwamba ikiwa watu wataamua kutembea tu kwa dakika 20 kila siku itakuwa na manufaa makubwa sana kwa mwili.
Wataalamu wanasema mazoezi yana manufaa sana kwa watu wenye uzani wowote ule.
Mojawapo ya sababu za watu kunenepa kupita kiasi au 'Obesity' huwa ni kukosa mazoezi.
Hata hivyo, inajuikana kwamba watu wanaokuwa wembamba pia kupita kiasi wanakabiliwa na changamoto nyingi za kiafya ikiwa pia watakosa kufanyisha mwili mazoezi.
Na pia watu wanene kupita kiasi ambao hufanya mazoezi wanakuwa katika hali nzuri ya kiafya.
Utafiti huo, ulilenga kuonyesha athari za kukosesha mwili mazoezi.
Baadhi ya magonjwa yanayowaandama watu wanokosa kufanya mazoezi ni pamoja na maradhi ya moyo ingawa kisukari ndio ugonjwa ambao watu wanene sana wako katika hatari ya kuugua.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment