Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 9 January 2015

MWANABLOGU ACHAPWA VIBOKO HADHARANI


Mwanablogu nchini Saudia amechapwa viboko hadharani kwa madai ya kutusi dini ya Kiislamu.

Raif Badawi ambaye alianzisha mtandao kwa jina ''Liberal Saudi Network'' alihukumiwa kifungo cha miaka 10 msimu wa joto uliopita.
Mahakama pia iliagiza acharazwe viboko 1000.
Amechapwa viboko hivyo katika mji wa Jeddah.
Ilieleweka kwamba angetandikwa viboko hamsini na kwamba alitarajiwa kuchapwa viboko zaidi wiki zilizofuatia.
Mwanablogu huyo alichapwa viboko licha ya wizara ya maswala ya kigeni nchini Marekani kutaka kuondolewa kwa adhabu hiyo walioitaja kama ya kikatili.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment