Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 9 January 2015

UN YAKEMEA MSHAMBULIZI YA ALBINO


Umoja wa Mataifa umekemea wimbi la mashambulizi dhidi ya Watu wenye ulemavu wa ngozi, Albino, baada ya tukio la kutekwa kwa mtoto wa miaka minne mjini Mwanza, kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Mwakilishi wa UN nchini humo Alvaro Rodriguez ameitaka Serikali ya Tanzania kuzidisha juhudi za kupambana na vitendo vya unyanyapaa dhidi ya albino.
Akiwa katika ziara kanda ya ziwa, Mjumbe huyo wa UN amekemea kutekwa kwa binti mdogo na kutoa wito kwa serikali kufanya kila iwezalo kumuokoa na kumkutanisha na Familia yake.
Mtoto Pendo Emmanuel alitekwa akiwa nyumbani kwake Kijiji cha Ndami baada ya Watu kadhaa wakiwa na mapanga kuvamia makazi yao tarehe 27 mwezi Desemba mwaka jana.
Polisi wamesema Watu 15 akiwemo Baba yake wamekamatwa wakihusishwa na tukio la kutekwa kwa mtoto huyo.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment