Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 15 January 2015

HUDUMA ZA UMMA HAKUNA TEMEKE, KISA MSIBA!

 Tangazo katika Ofisi za Idara ya Elimu (Msingi) katika Manispaa ya Temeke kuonyesha kwamba hakuna huduma zozote kwa sababu ya msiba.

Msiba wa mmoja wa wafanyakazi wa Idara ya Elimu Msingi katika Manispaa ya Temeke umesababisha kusimamishwa kwa huduma zote za umma na kufungwa kwa ofisi leo hii.

BrotherDanny Blog ilishuhudia msururu wa wazazi waliofika kwenye eneo la ofisi hizo na kurudishwa na walinzi getini kwamba ofisi zimefungwa kwa kuwa kuna msiba.
"Tumewaambia ofisi zimefungwa, huko hakuna hata mtu mmoja... someni tangazo hapa," alisema kwa ukali mmoja wa walinzi wa kike kwenye geti hilo.
Ama tangazo lililobandikwa kwenye geti katika ofisi hizo linaeleza kwamba, hakutakuwa na huduma zozote kwenye idara hiyo hadi Jumanne Januari 20, 2015, hali ambayo inawalazimu wazazi waliokuwa wakiwatafutia uhamisho watoto kusubiri mpaka Jumanne.
tangazo lenyewe lilisema: "...Idara ya Elimu Msingi inatangaza kwamba leo Alhamisi tarehe 15/01/2015 hakutakuwa na huduma ya uhamisho kwa wanafunzi pamoja na huduma nyingine za kiofisi, hii ni kutokana na msiba uliotokea hivyo watumishi  watakuwa msibani na baadaye katika maziko, huduma zitarudi katika hali ya kawaida siku ya Jumanne tarehe 20/01/2015. Ofisi inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza. UTAWALA."

My take: Ni kweli suala la msiba ni nyeti sana, lakini hivi ni sahihi kusimamisha huduma zote za umma katika ofisi ya umma badala ya kuacha hata mwakilishi mmoja, hasa ikizingatiwa kwamba huduma za uhamisho (kwa mfano) zinafanyika mara mbili tu kwa wiki (Jumanne na Alhamisi) na sasa watoto wanapaswa kuwa darasani?

Daniel Mbega

No comments:

Post a Comment