Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 19 January 2015

ARSENAL YAWASHANGAZA MABINGWA WA EPL

Santi Carzola
Santi Carzola alifunga bao moja na kutengeza jengine na kuisadia Arsenal kuicharaza Man City mabao 2-0 nyumbani Manchester.

Ushindi huo wa Arsenal pia ulisitisha msururu wa kutofungwa wa Man City wa mechi 12.
Mchezaji wa Uhispania Santi Carzola aliyekuwa moto wa kuotea mbali dhidi ya Mancity alifunga mkwaju wa penalty baada ya beki wa Arsenal Nacho Monreal kuangushwa katika eneo la hatari na beki Vincent Kompany.
Man City
Arsenal iliongeza bao la pili katika kipindi cha pili baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na Santi Carzola kuwekwa wavuni na Olivier Giroud.
Matokeo hayo yameiwacha City ikiwa na alama 5 chini ya viongozi wa ligi Chelsea.
City na Arsenal walitoka sare ya 2-2 wakati walipokutana kwa mara ya kwanza katika uga wa Emirates mnamo mwezi Septemba.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment