Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 9 January 2015

TFDA YATEKETEZA VIPODOZI

MAMLAKA ya chakula na dawa TFDA, kanda ya kaskazini imeteketeza vyakula, vipodozi na dawa zenye thamani ya shilingi  8,825,500, vyenye uzito wa kilogram 167.

Meneja wa kanda ya kaskazini wa mamlaka ya chakula na dawa, TFDA,Damas Matiko, amesema bidhaa hizo zimekamatwa katika msako ulioendeshwa na mamlaka hiyo ya chakulka na dawa,TFDA, kwenye maduka mbalimbali katik mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.

Amesema kuwa bidhaa hizo zimekamatwa mwezi Novemba na Desemba mwaka huu 2014, katika msako unaolenga kuondoa bidhaa zisizofaa  kwa matumizi ya binadamu maduka yote yanayuza bidhaa hizo.

Bidhaa hizo ambazo zimeteketezwa kwenye jalala kuu la halmashauri ya jiji la Arusha lililopo Muriet kata ya Sokon one Desemba 31 mwaka 2014.

Matiko,amesema msako huo unatokana na sheria ya  chakula ,dawa  na vipodozi ya mwaka 2014 inayoagiza mamlaka ya chakula na dawa TFDA, kuondoa sokoni bidhaa zote ambazo hazifai kwa matumizi ya binadamu kutokana na kutokukidhi matakwa ya sheria.

Katika zoezi hilo vyakula vilivyoteketezwa ni vyenye uzito wa kilogram 86.7 vyenye thamani ya shilingi  4,362,000, dawa zenye uzito wa 12.695 kilogram zenye thamani ya shilingi  1,482,500  na vipodozinyenye uzito wa kilogram 68.029 vyenye thamani ya shilingi 2,981,000.

Bidhaa hizo zina mapungufu mbalimbali ikiwemo kutokusajiliwa na mamlaka ya chakula na dawa TFDA,kuuzwa vikiwa vimekwisha muda wake wa matumizi.

Pia bidhaa hizo kutokuwa na taarifa za kuonyesha lini imetengenezwa muda wa mwisho wa matumizi, kutokuwa na lugha zinazofahamika ambazo ni Kiingereza na Kiswahili, kutokuwepo na taarifa ya bidhaa kwenye vifungashio (lebo) hivyo havina ubora unaotakiwa.

Vipodozi hivyo ni pamoja na  vile ambavyo vina viambato vya sumu aina Zebaki (Mercury) zikiwemo sabuni aina ya Jaribu ambazo zina sumu hiyo ya zebaki na zilishapigwa marufuku nchini.

Matiko amesema bidhaa hizo zina madhara makubwa kwa watumiaji  kwa kuwa vinaathiri viungo vya uzazi, maini, kusababisha magonjwa ya kansa, magonjwa ya ngozi, magonjwa ya matumbo (kuharisha), kubabuka mwili na ngozi, ikiwemo mzio (alegy) na hivyo kusababisha gharama kubwa  ya matibabu kwa mulaji.

Akawataka wafanyabiashara kufuata sheria  kwa kuingiza bidhaa ambazo zimesajiliwa ambazo hazina madhara kwa walaji.

Ameongeza kuwa sheria ya chakula ,dawa na vipodozi ya mwaka 2003 inataka kulindwa kwa afya za walaji ,kwa kula na kutumia bidhaa zisizo na madhara ya kiafya na mwili.

Kwa upande wake afisa afya na mazingira kutoka ofisi ya Halmashauri ya Jiji la Arusha, Monica Ngonyani, amewataka watu kuuepuka kula vyakula na kutumia vipodozi vyenye  madini ya Zebaki, kwa kuwa vina madhara makubwa katika afya na mwili wa mlaji.

Amesema kula vyakula ambavyo havina ubora na wala havijathibitishwa na mamlaka ya chakula na dawa TFDA, vina madhara makubwa ya kiafya na kimwili ambapo mlaji hupawa na magonjwa mbalimbali kutegemea na aina ya chakula, vipodozi au dawa aliyotumia.

Amewaomba watu wanaonunua bidhaa kwenye maduka ya kuuza bidhaa mbalimbali ikiwemo vyakula, dawa na vipodozi kukagua kwanza bidhaa husika kabla ya kununua ili kuepuka kupata madhara makubwa yanayotokana na matumizi ya bidhaa hizo.

No comments:

Post a Comment