Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 7 January 2015

CCM YATABIRI NDOA YA UKAWA


Na Mwandishi Wetu, MERUCHAMA cha Mapinduzi kimesema kuwa Umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA)utaisha mwakani mwezi February kwa kuwa baadhi ya viongozi wa umoja huo wengi wao wana matarajio ya kuwania nafasi ya urais.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi taifa Abadlah Bulembo wakati akiongoza maelfu ya wanachama wa CCM Wilaya ya Meru kumsimika na kumuingiza kazini rasmi Kamanda wa vijana wa wilaya hiyo John Palangyo.

Bulembo alisema kuwa mpaka sasa kuna dalili lakini pia taarifa za kuvunjika kwa ndoa hiyo ya ukawa ambayo ilianza rasmi kwenye bunge la katiba lilimalizika mjini Dodoma hivi karibuni.

Akitoa sababu mbalimbali ambazo zinafanya ndoa hiyo ya ukawa iweze kuangamia Bulembo alisema ni pamoja na wengi wao kutamani nafasi ya kuongoza hasa kwenye suala zima la uraisi lakini pia hata katika nafasi za uongozi.

"jaribuni kuangalia kwenye huo UKAWA nani ambaye hatamani kuwa Raisi na pia nani ambaye hatamani kuona kuwa hasimamishi mgombea na mimi napenda kusema kuwa wasijitambe kwenye majukwaa mbalimbali kuwa eti wanapenda hilo halipo kabisa"aliongeza Bulembo.


kutokana na hilo aliwataka wananachi kuhakikisha kuwa kwa sasa wanachambua mambo kwa kina na wasikubali kudanganyika kwani wakati mwingine wapo baadhi ya wana siasa ambao wanatumia nafasi zao za siasa na kisha kupotosha umma.

katika hatua nyingine kamanda mpya wa Wilaya hiyo ya Meru John Palangyo alisema kuwa tayari CCM ina mipango mbalimbalo ya kuweza kuwakomboa wananchi hususani kwenye mahitaji muhimu

Palangyo aliyataja mahitaji hayo kuwa ni pamoja na sekta ya elimu, afya, uchumi ambapo kama hivyo vyote vitaweza kutekelezeka basi vitachangia maendeleo kwa kiwango cha juu

Alimalizia kwa kuwataka wanachi kuachana na makundi mbalimbali ambayo yanaweza kuwagawa lakini pia hata kuhatarisha chama hicho na badala yake wawe kitu kimoja katika kulijenga taifa la Tanzania.

No comments:

Post a Comment