Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 26 January 2015

TANZANIA KUHODHI LIGI YA MPIRA WA WAVU


Tanzania imechaguliwa tena kuwa wenyeji wa michuano ya mpira wa wavu ya mataifa ya Afrika (All Africa Games) itakayofanyika mapema mwezi wa nne mwaka huu.

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa shirikisho la mpira wa wavu nchini (Tava) kuchaguliwa kuwa wenyeji wa michuano mikubwa barani Afrika kwa nchi za ukanda wa tano.
Tanzania, kati kati ya mwezi ujao (Februari 16-18) itakuwa wenyeji wa michuano ya mpira wa wavu kwa nchi za kanda ya 5 Afrika na kwa mujibu wa Rais wa Tava, Augustino Agapa, wanajiandaa pia kualika timu kwa ajili ya michuano hiyo ya mataifa ya Afrika.
“Hivi karibuni nilikuwa Misri katika mkutano wa marais wa vyama vya wavu kutoka nchi za kanda ya 5 na tumepewa heshima ya kuwa wenyeji”, alisema Agapa.
Timu kutoka nchi za Kenya, Burundi, Somalia, Rwanda, Ethiopia, Djibouti na wenyeji Tanzania zitashiriki michuano hiyo ya wavu ya ufukweni, ambao bingwa atashiriki michuano ya kombe la Afrika (Africa Cup) itakayofanyika Septemba nchini Congo Brazzaville ili kupata timu itakayoshiriki michuano ya Olimpiki mwakani mjini Rio de Janeiro, Brazil.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment