Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 13 January 2015

WAKULIMA BINAFSI WA TUMBAKU WAONYWA


Na Hastin Liumba,TaboraCHAMA  kikuu cha  wakulima wa zao la tumbaku kanda ya magharibi (WETCU)  kimefanya  mkutano wa uchaguzi wa wajumbe wa bodi  ambapo Mkandala Gabriel  Mkandala amechaguliwa kuwa mwenekiti mpya kwa kura 401.



Katika uchaguzi huo Mkandala alishinda nafasi hiyo kwa kura  401 za ndiyo kati ya  418 zilizopigwa huku 16 zikiwa za hapana  na moja ikiharibika kwani hakuwa na mpinzani.

Uchaguzi huo umefanyika chini ya uenyekiti wa Mossi Chongelo  kaimu mrajisi wa vyama vya ushirika nchini kunafuatia kusimamishwa kwa bodi iliyokuwepo kuondolewa mwezi marchi 2013 kwa tuhuma za ubadhirifu wa mali za chama.

Nafasi ya makamu mwenyekiti imechukuliwa na Msafiri Ngassa kwa kura 253 akiwabwaga wapinzani wake  Abel Willison aliyepata kura 131  huku Rajab Hamis akiambulia kura 51 kati ya zilizopigwa 426.

Wengine waliochaguliwa kuwa Wajumbe  wa bodi ni Kabansi Mayagillo, Rajab Hamis, Abel Willison, Athanas Vallentino, Izaki Jakobo na Phillipo Pascal huku nafasi moja ya mjumbe kutoka Urambo ikibaki wazi kwa  vile kati  ya walioomba  hakupatikana aliyekidhi vigezo vya kugombea.

Akizungumza mara baada ya uchaguzi huo mwenyekiti mpya  amewaonya wakulima wa kujitegemea  na kuahidi kuwachukulia hatua kali wanaojaribu kuua vyama vya msingi vya ushirika.

Mkandala  ambaye anashika  wadhifa huo kwa miaka mitatu ijayo  amesema hatosita kuwachukulia hatua kali za kisheria wakulima wa kujitegemea endapo hawatazingatia sheria  ya ushirika inavyosema.

Amewaonya wakulima hao wasijaribu  kujihusisha na kuu vyama vya ushirika atakayethubutu kufanya hivyo atapambana naye.

Akizungumza katika mkutano huo kaimu mrajisi wa vyama vya ushirika nchini Mossi Chongelo ameitaka bodi hiyo mpya itekeleze matakwa ya wanachama kwani wao ndiyo wamekabidhiwa hiyo dhamana.

Hali kadhalika amewashauri  wanachama wa vyama hivyo kujiendeleza kielimu ili kuendana na matakwa ya sheria mpya ya ushirika namba 6/2013 ambayo inawataka viongozi kuwa elimu ya zaidi ya kidato cha nne.

Mara baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi Deogratias Ruganyika  aliwataka wanaushirika kutoa ushirikiano kwa viongozi hao wapya ili waweze kuwatumikia ipasavyo.

Katika hatua nyingine aliyekuwa mwenyekiti wa muda wa badi hiyo Hassan Wakasuvi alionyesha kukelwa kwake na sheria hiyo mpya ya ushirika hasa katika uombaji nafasi za uongozi.

Wakasuvi alisema kuwa sheria hiyo inawaona ni watu wazuri wakati wa uzalishaji mazao lakini baadaye wanapotaka nafasi za uongozi wanakuwa wabaya pale inapowawekea masharti magumu.

No comments:

Post a Comment