Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 13 January 2015

COASTAL YAANZA KUANDAA SILAHA ZA KUIANGAMIZA POLISI MORO

Displaying KIKOSI.jpg
Kikosi cha Coastal Union kilichocheza mechi ya kirafiki na Mombasa Kombaini na kutoka sare ya kufungana bao 1-1,Mkwakwani.
Displaying VIONGOZI COASTAL.jpg
Viongozi wa Coastal Union wa kwanza kushoto ni Meneja wa Coastal Union,Akida Machai,Katibu Mkuu Kassim El Siagi,Mjumbe wa Kamati ya utendaji Coastal Union Salim Bawazir wakifuatilia mchezo huo.
Displaying WAAMUZI NA WACHEZAJI.jpg
Mshambuliaji wa Coastal Union,Godfrey Wambura akipatiwa huduma ya kwanza mara baada ya kuumia kwenye mchezo huo.
Displaying DSC06009.JPG
Kocha Mkuu wa Coastal Union, Mkenya James Nandwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika mechiu hiyo. (Picha zote kwa Hisani ya Coastal Union).

NA MWANDISHI WETU, TANGATIMU ya Coastal Union imesema kuwa umuhimu wa timu hiyo kufanya vizuri kwenye mechi yao na Polisi Morogoro itakayochezwa wikiendi ijayo ni mkubwa kutokana na kuimarishwa kwa safu mbalimbali kwenye kikosi hicho.
Kocha Mkuu wa timu hiyo, James Nandwa  aliyasema hayo mwishoni mwa wiki mara baada ya kumalizika mechi ya kirafiki kati yao na Mombasa Kombaini iliyochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani na kumalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1.

Kwenye mechi hiyo, Coastal Union ndio ilikuwa ya kwanza kuweza kupata bao lao kupitia Rama Salum dakika ya 5 lililotokana na penati baada ya mshambuaji wa Coastal Union,Behewa Sembwana kuangushwa eneo la hatari na Omari Sharifu wa Mombasa Kombaini na mwamuzi wa mechi hiyo Isihaka Shirikisho kuamuru ipigwe penati hiyo.

Bao hilo lilidumu mpaka timu zote zinakwenda mapumziko ambapo kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa timu zote kushambulia kwa zamu na kuonyesha kandanda nzuri na la kuvutia.

Wakionekana kucheza kwa umakini mkubwa baada ya kufanya mabadiliko kwa baadhi wa wachezaji wao, Coastal Union waliweza kuendeleza wimbi la mashambulizi langoni mwa Mombasa Kombaini huku wachezaji wake wakikosa kosa mabao ya wazi kwa kupiga mashuti yaliyokuwa yakigonga mwamba na kurudi uwanjani.

Kutokana na shambulio hilo,Mombasa Kombaini nao waliweza kujipanga vilivyo na kuanza kucheza kwa umakini hali iliyowasaidia kufanikiwa kuandika bao la kusawadhisha kwenye dakika ya 47 kwa njia ya penati kupitia Khalid Jumaa dakika ya 47 lililotokana na Nahodha wa Coastal Union,Mbwana Kibacha kuunawa mpira eneo la hatari.

Alisema kuwa kikubwa zaidia anachojivunia ni kuwa na kikosi kizuri na tayari alishaelewa nini cha kufanya ili kuweza kupata mafanikio kila mchezo ambao wanakabiliana nayo kwenye michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara.

   “Timu yetu ni nzuri hivyo anachokifanya ni kuhakikisha wachezaji wanajitambua kwa dhamira ya kufanya makubwa kwenye mechi zao za Ligi kuu soka Tanzania bara hapa nchini “Alisema Kocha Nandwa.

Alisema kuwa mchezo huo ni kipimo tosha kwa timu hiyo kabla ya kuwavaa maafande wa Polisi Morogoro ikiwa ni muendelezo wa michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara hapa nchini.

No comments:

Post a Comment