Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 3 January 2015

RAGE ATOA MISAADA WA SHS. 2.7 MILIONI KWA WAHANGA WA MVUA

Ismail Aden Rage

Na Hastin Liumba, Tabora
MBUNGE wa jimbo la Tabora mjini Ismail Aden Rage ametoa msaada wa Shs milioni 2.7 kwa wahanga 27  waliobomokewa nyumba zao kata ya Tumbi kufuatia mvua kubwa iliyonyesha wiki iliyopita.


Akiongea na waandishi wa habari Rage alisema amefikiwa hatua hiyo baada ya kuguswa kama mbunge na msaada aliotoa ni sh 100,000 kwa wahanga 27.


Alisema fedha hizo zitawasadia wahanga hao kufanya ukarabati wa nyumba zao ambazo zinahitaji kurekebishwa sehemu mbalimbali.

Alisema katika wahanga hao wapo wahanga wawili, mmoja kama mbunge atamjengea kufuatia nyumba yake kuanguka yote na hadi kukamilika kwake itagharimu kiasi cha sh milioni 1.8.

Aidha aliongeza kuwa mhanga mwingine Joha Maganga yeye chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Tabora mjini wameamua pia kumjengea nyumba nyingine na gharama yake itajulikana hapo baadaye.

Rage alipongea pia jitihada za mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tabora mjini Abrahaman Moshi Nkonkota kwa kujitolea Turubai Nane kwa wahanga hao wakiwemo baadhi ya madiwani ambao nao wameshiriki kutoa pole kwa
wahanga hao.

“Haya ni matatizo yanayotuhusu sote hivyo ni vyema watu na taasisi mbalimbali wakaungana nasi kusadia ndugu zetu hawa.” alisema.

Katika hatua nyingine mbunge huyo aliwashukuru wananchi wa wilaya ya Tabora mjini kwa kuwapa kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

No comments:

Post a Comment