Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Friday, 9 January 2015
TEMBO ZAIDI 20 WAUA SIKONGE
Na Hastin Liumba, SikongeZAIDI ya Tembo 20 wamevamia makazi ya watu na wilayani Sikonge mkoani Tabora na kuharibu mazao, kujeruhi na kuua mtu mmoja.
Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili Afisa Mtendaji wa kata ya Tutuo Mrisho Haruna Kilundumya alisema tukio hilo limetokea siku ya Jumanne asubuhi ambapo tembo hao walivamia kitongoji cha Ikungu kijiji cha Mitowo na kuzusha hofu.
Mrisho alitaja maeneo yaliyovamiwa ni kata za Tutuo, Mole na Kisanga.
Alisema baada ya tembo hao kuonekana kijijini hapo wananchi walianza kuwapigia kelele ndipo tembo walianza kuwashambulia ambapo Kulwa Jilala Manoti (35) alidondoka na kukanyagwa na tembo mgongoni na kufariki papo hapo.
Kilundumya alieleza kuwa tembo hao ambao wanadhaniwa kuwa walitokea katika pori la hifadhi ya Ugalla na Uyumbu katika wilaya ya Urambo na kupita katika vijiji vya Kidete na Mole Mlimani majira ya usiku kabla ya kutokea katika kijiji hicho na kuelekea kijiji cha Mwamayunga kata ya Kisanga na kujeruhi mtu mmoja aliyekuwa anachunga ng’ombe.
Aidha tembo hao kijiji cha Muungano katika kata ya Tutuo ambako walivamia mashamba ya mihogo na kuiharibu vibaya kabla ya kuondoka eneo hilo.
Kilundumya aliutaarifu uongozi wa wilaya na Maofisa wa Wanyamapori mjini Tabora ambao walifika katika eneo la tukio kujionea uharibifu na kwa ajili ya taratibu zingine za kudhibiti wanyama hao.
Uongozi wa wilaya hiyo umewataka wananchi wanaoishi katika maeneo hayo kuwa watulivu wakati Maofisa wa wanyamapori wakiendelea na taratibu zingine za kudhibiti wanyama hao ili wasiendelee kuleta madhara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment