Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 13 January 2015

MSIWATAFUTE VIONGOZI WA SERIKALI WAKATI MNA SHIDA NA HARAMBEE - MCHUNGAJI

 
Na Mwandishi Wetu, Arusha
IMEELEZWA kuwa tabia ya baadhi ya taasisi za dini kuwakwepa viongozi wa dini na kisha kuwatafuta wakati wakiwa na uhitaji ni chanzo mojawapo cha kusababisha hata hekima ndani ya uongozi wao kuweza kupungua kwa kiwango kikubwa.


Viongozi wa dini watakiwa wawe na utaratibu wa kukaa na hawa viongozi wa ngazi zote na hata wale wa asasi binafsi kwenye jamii na kisha kuwaombea baraka lakini pia kuwapa maneno ya hekima ambayo yataweza kuwasaidia katika uongozi wao.

Kauli hiyo imetolewa na Mchungaji Nakambetwa Shackademas kutoka katika kanisa T.A.G Unga Limited jijini Arusha wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mikakati ya kanisa hilo kwa jamii kwa msimu huu wa mwaka 2015

Mchungaji huyo alidai kuwa umefika wakati sasa kwa tasisi za dini kuweza kujua na kutambua kuwa wao ndio wasiamimizi wakuu wa hawa viongozi hasa wale waliopo kwenye madaraka hivyo kuna umuhimu sasa wa kuwa nao bega kwa bega.

Alifafanua kuwa endapo kama taasisi za dini zitaweza kuunga na kisha kuwa kitu kimoja basi zitaweza kufanikisha kwa kiwango cha juu hata mapungufu yaliopo kwenye nchi kwa sasa kwani tayari watakuwa wamepewa baraka za taasisi za dini

Pia alisema kwa taasisi za dini hazipaswi kuwatafuta viongozi hao wakati wakiwa na shida hasa Harambee bali wanatakiwa kuwatafuta nakisha kuweza kuwashauri juu ya mambo mbalimbali ambayo yanaitesa nchi ya Tanzania.

Katika hatua nyingine alisema ili kutekeleza suala hilo tayari wana mikakati ya kuanza kuwaita sasa viongozi hao na kisha kuwapa elimu pamoja na semina ambazo zitaweza kuwasaidia katika uongozi wao.

Mchungaji huyo alisema kuwa wanamini kwa kuwakutanisha viongozi  wa ngazi za chini hadi zile za kimataifa wataweza kuwasaidia na pia wataweza kuwapa mbinu mbadala za kuwa na maadili mema pamoja na hekima ambayo inajitosheleza kwenye jamii.

“Tumedhamiria kuweza kuwaita hawa viongozi wa serikali, sekta binafsi, waje hapa na kisha kuweza kuwapa maarifa mbalimbali ambayo yataweza kuwasidia na kwa kufanya hivi tunaamini kuwa tutasaidia jamii ambayo inategemea zaidi misaada kutoka kwao”aliongeza.

No comments:

Post a Comment