Na Hastin Liumba,Uyui
JUMUIYA ya Umoja wa akinamama wa (UWT) wilaya ya Uyui mkoani Tabora, wamepongezwa kwa kujitokeza kugombea katika nafasi chaguzi za Serikali za mitaa vitongoji na Vijiji kwa kupata ushindi.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mariamu Kashandago alisema hayo katika kikao cha kawaida cha kutoa taarifa ya uchaguzi katika jumuiya hiyo ya wilaya ya Uyui mkoani hapa.
Kashandago alisema amefurahishwa na akinamama kujitokeza kwa na akina baba kuwaruhusu wake zao kugombea katika nafasi za vitongoji na vijiji.
Aidha Kashandago aliwaambia akinamam hao mwaka wa 2015 waendelee kujitokeza kugombea nafasi za Udiwani na Ubunge bila kusita na wahakikishe wanahamasisha akinamama wenzao kushiriki kukamilifu.
Mwenyekiti huyo alimpongeza Mbunge wa Viti maalumu Munde Tambwe kwa kujitolea kutoa vifaa vya mradi wa kufyatulia matofali ili waondokane na hali ya ombaomba.
Aliendelea kusema kuwa kujitolea ni kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi na sio utajili,hivyo mwenyekiti huyo amewataka viongozi na asasi zisizokuwa za Kiserikali wajitokeze kuichangia Jumuiya hiyo.
Nae katibu wa jumuiya hiyo Zinduna Kisamba aliwakabidhi wanajumuiya kadi za bima wajumbe wote wa wilaya ya Uyui mkoani hapa.
No comments:
Post a Comment